Nina wasiwasi na "uwaminifu" wa w/kazi wa tigopesa

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,134
833
Hivi wanajamvi kuna mtu amewahi kukosea kutuma pesa kwa wakala wa tigopesa (akamtumia wakala mwingine) halafu akapiga simu tigo na kufanikiwa kurudishiwa??

Mimi hawa jamaa wamenichosha kwa kweli!!

Kuna rafiki yangu ambaye ni wakala wa tigopesa, Mpesa na Airtel-money nilimuomba anitumie elfu 50. Akanitumia kwa tigopesa. Tarehe 25 mwezi wa pili nikampigia anitumie namba yake ya "Kiwakala" nimrudishie, jamaa akanitumia ya Mpesa bila maelezo. Mimi pasipo kujua ilikuwa ya Mpesa nikadhani ni tigopesa kama aliyotumia kunipa hela. Kuirusha katika tigopesa kwa kutumia hiyo namba ikaenda kwa wakala mwingine. Lol, ngoma sasa ni kuirudisha hiyo fedha!!

Taratibu za tigopesa: Eti haiwezekani kuirudisha kama wakala huyo hana kiasi kinachofika hiyo elfu 50! Kubwa zaidi kila nikiwapigia simu jibu lao ni moja tu, 'huyo wakala hana hela yakutosha (inayofika kiasi ulichotuma cha elfu 50), endelea kutupigiapigia uwe unaulizia, utakapopiga tukakuta ana kiasi hiko tutakurudishia.' Toka tar 25 mwezi wa pili hakuna siku wakala kafikisha elfu 50!!!! Ndiyo maana nina wasiwasi na "uwaminifu" wa hawa w/kazi, nahisi hizi ndizo sehemu zao za "kupiga" mshiko. Ukiwauliza wakuambie basi kama huyo "wakala" katika transactions zake amewahi hata kufikisha hiyo elfu 50 katika historia yake wanakuambia hatuwezi kukuambia! Sasa hamuwezi kuniambia na hapohapo mnataka niendelee kupiga simu kuulizia, Je kama transactions zake ni za elfu mbili si nitakuwa napiga simu hadi "kiama"!!!

WanaJF wenye uzoefu na hili niwaombeni muumwage uzoefu wenu kwa hili, nahisi upo uwezekano wa kuwa na watu wengi wenye matatizo kama haya. Na kama ni "Ndivyo" kuna haja ya kuchukua hatua kuwamwagia watu unga wao.

[Nawasilisha]
 
Hao wanapiga pesa tuu...
Kama unabisha poteza iyo laini nenda kaulize kusajili unaambiwa eti inakumbuka ulikua na pesa kiasi gani kama unataja salio dogo na ulikua na kubwa kinachobaki chao si uhuni huo...
 
Back
Top Bottom