Nina wasiwasi na January Makamba

Nina wasiwasi na January Makamba

Hivi wanajamvi, mbona wakati mwingine hamueleweki!

Hivi ni mgombea gani asiyekuwa na udhaifu? Tangu baadhi ya viongozi na wasio viongozi watangaze nia ya kuwania nafasi mbalimbali humu mnakuja na mijadala inayokatisha tamaa. Sijaona hata siku moja kati yao mnamsifia kwa weledi na uwezo. Wote ni wabaya mbele zetu, Hivi tunahitaji aina gani ya kiongozi mwenye tabia, uwezo tofauti na waliojitokeza?

Mimi namchukulia J Makamba kama kijana mtanashati, mwenye uwezo kiakili, mbunifu na mwenye kuijua dunia ya leo inayoendelea kwa kasi sana. Sasa masuala mengine yanatafsiriwa kama chuki binafsi dhidi yake na kama yupo mnyoofu kwa asilimia 100 basi mleteni humu jamvini tumjadili.

VIVA MAKAMBA VIVA KIJANA! Keep it up!
 
Hahahahaaaa.......umenichekesha sana! You actually believe twaweza surveys? Weren't January Makamba and Juma Mwapachu (former EAC sec gen) the guests of honor? What did you expect?!
Let them go out to the streets and ask the common wananchi.
I'll give you a simple task. Just visit all online forums and newspaper comment sections and see how many Tanzanians actually favour this EAC thing. Start with this very thread. I believe you are the first to somehow agree!
Sisemi kwamba Tanzania isiwe EAC. lakini tusilazimishwe kukubali vitu ambavyo vitasababishia hasara taifa letu, kama vile hiyo single tourist visa!

@msemakweli

Wewe msemakweli gani uliye muongo kiasi hichi? Naona takwimu zimekusuta, sasa ukaamua kugombana na watoa takwimu! Umeshindwa hoja.

Eti nisome comments za online forums kweli? Hizo ndizo representative sample za waoni ya Watanzania kweli? Yaani umenisikitisha na kunidhalilisha sana, nitaishia na post hii maana kuendelea kujadiliana na wewe tena kunanifanya na maana na mimi nionekane mjinga.

Kwa taarifa yako, utafiti wa "Sauti za Wananchi" inayofanywa na Twaweza hauna mfano wake barani Afrika. Sio kazi ya kubahatisha ya kusoma utumbo mitandaoni. It is the best nationally representative mobile survey on the continent, na katika suala hili walipiga simu na kupata maoni ya Watanzania zaidi ya 1,400 kutoka kila kona ya Tanzania Bara na kuyachambua.

Soma utafiki kamili hapa kabla ya kubwabwaja bwabwaja hapa http://www.twaweza.org/uploads/files/Integration-EN-FINAL.pdf
 
Mtu aliepata Div IV O'Level (alisoma Forrest Sec Morogoro) na akaenda kusoma vyuo vya uchochoroni Marekani hana ujanja wa kung'amua mambo. Kaingizwa mkenge kwa tamaa ya kupata urais.
Mmmh!!! Nadhani wewe unatakiwa kuichukia hiyo hali uliyonayo ya CHUKI + WIVU
 
Na ni hapo hapo, alipojinyea akiwa form two.

eti nikisema mtu kajinyea mods wanaondoa post utafikiri wao hawanyi.

kwa sababu kujisaidia ni mtu kwenda MSALANI, kujisaidia hadharani tena kwenye nguo zao mwenyewe, yaani ka vile wanavyofanya watoto kwenye pumpers ni kujinyea huko.

na sio kwamba ni mbaya, labda ye ndo anapenda.
kama sijakosea wewe ni kabila fulani. Hawajishughulishi kutafuta maisha ila kazi yao ni KUPONDA wenzao tu sababu ya WIVU. Ukiona mtu amefikia ngazi fulani ya uongozi au maendeleo basi Amini kuwa Mungu ameruhusu yeye kuwa pale. FANYENI KAZI
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni mmoja wa supporters wake ila naomba kama atasoma hii thread basi aliangalie hili.

Kwenye twitter aliahidi kuiingiza Tz kwenye EAC kikamilifu, na anadisitiza tusitake things slowly kama ilivyo desturi ya Tz.

Wakenya wamempongeza sana juu ya hilo. juzi kati pia alienda Kenya na kupokelewa vizuri.

My take ni kuwa Tz huwa haiungi mkono mambo ambayo hayana faida kwake ovyoovyo kama ile single tourism visa.

Namwomba January atuhakikishie watanzania kuwa maslahi ya taifa letu yatakuwa salama endapo atatwaa madaraka mwakani.

Mbona mimi naona kwenye ishu ya EAC aliongea vizuri tu. Hebu cheki makala hapo chini.

"According to the report, which was based on political, economic, cultural and social concerns of citizens from all partner states, concerns were raised about differences in land tenure systems of partner states and loss of land due to free movement and rights of establishment within the bloc.

"A political federation is possible in future and not now. We have to learn from the lessons that led to the collapse of the EAC in 1977 and avoid forcing things because a second failure will be extremely costly," said Makamba.

Makamba, however, noted that Tanzania was committed to the EAC ideals, and would want to take a leading role in their realisation under an environment of mutual respect among member states."

Endelea kusoma.
Standard Digital News - Transforming EAC into a political federation unrealistic, says Tanzania?s presidential hopeful January Makamba
 
@msemakweli

Wewe msemakweli gani uliye muongo kiasi hichi? Naona takwimu zimekusuta, sasa ukaamua kugombana na watoa takwimu! Umeshindwa hoja.

Eti nisome comments za online forums kweli? Hizo ndizo representative sample za waoni ya Watanzania kweli? Yaani umenisikitisha na kunidhalilisha sana, nitaishia na post hii maana kuendelea kujadiliana na wewe tena kunanifanya na maana na mimi nionekane mjinga.

Kwa taarifa yako, utafiti wa "Sauti za Wananchi" inayofanywa na Twaweza hauna mfano wake barani Afrika. Sio kazi ya kubahatisha ya kusoma utumbo mitandaoni. It is the best nationally representative mobile survey on the continent, na katika suala hili walipiga simu na kupata maoni ya Watanzania zaidi ya 1,400 kutoka kila kona ya Tanzania Bara na kuyachambua.

Soma utafiki kamili hapa kabla ya kubwabwaja bwabwaja hapa http://www.twaweza.org/uploads/files/Integration-EN-FINAL.pdf
Single tourist visa ina manufaa gani kwa Tanzania?
We ishia hapo lakini nakwambia kitu as important as regional cooperation of this level kinahitaji full participation ya wananchi. Yaani siyo kijisurvey cha watanzania 1400 yet nchi hii ina watu zaidi ya million 45!
Jambo lolote lisilowafaidi watanzania likataliwe tena kwa nguvu zote! Just coz ni 'twaweza survvey' doesnt mean the fact that some of the EAC projects are at loggerheads with Tanzanian national interests should be overlooked.
Always Tanzania kwanza halafu EAC baadaye na siyo vice versa!
 
Mbona mimi naona kwenye ishu ya EAC aliongea vizuri tu. Hebu cheki makala hapo chini.

"According to the report, which was based on political, economic, cultural and social concerns of citizens from all partner states, concerns were raised about differences in land tenure systems of partner states and loss of land due to free movement and rights of establishment within the bloc.

“A political federation is possible in future and not now. We have to learn from the lessons that led to the collapse of the EAC in 1977 and avoid forcing things because a second failure will be extremely costly,” said Makamba.

Makamba, however, noted that Tanzania was committed to the EAC ideals, and would want to take a leading role in their realisation under an environment of mutual respect among member states."

Endelea kusoma.
Standard Digital News - Transforming EAC into a political federation unrealistic, says Tanzania?s presidential hopeful January Makamba
Mkuu asante kwa jibu lako zuri na la kiungwana. Nilitaka tu nitahadharushe kuwa asije akashawishiwa kukubali mikataba mibovu itakayofaidi nchi zingine zaidi kuliko Tz. Lakini inaonekana yuko sahihi.
Tuendelee kumuombea kijana mwenzetu mtanashati na msomi!
 
Hahahahaaaa.......umenichekesha sana! You actually believe twaweza surveys? Weren't January Makamba and Juma Mwapachu (former EAC sec gen) the guests of honor? What did you expect?!
Let them go out to the streets and ask the common wananchi.
I'll give you a simple task. Just visit all online forums and newspaper comment sections and see how many Tanzanians actually favour this EAC thing. Start with this very thread. I believe you are the first to somehow agree!
Sisemi kwamba Tanzania isiwe EAC. lakini tusilazimishwe kukubali vitu ambavyo vitasababishia hasara taifa letu, kama vile hiyo single tourist visa!

Political culture au niseme economic culture ya WaTZ/Wabongo ni kwamba tu WOGA sana wa kufanya mabadiliko au kujaribisha njia mbadala kwa kila kitu. Kila siku tunaimba (kama zilivyo nyimbo nyingi) wimbo wa 'ujasiriamali' lakini tunasahahu kuwa moyo wa ujasiriamali ni kuwa tayari to take risk. Sisi tunaogopa tukifanya mabadiliko (yaani kuacha kufanya yale yale kwa namna ile ile, watu wale wale, fikira zile zile) ili tusilete VITA, ili WaKenya wasituibie ardhi yetu, waGanda wasichuku ajira zetu, nk. "Watuache twende polepole" Profesa wa Kichina aliwahi kutamka katika hotuba zake. Tunaongozwa na falsafa ya kijadi ya waswahili ya 'polepole ndio mwendo', ama 'haraka haraka hiana baraka'. Wenzetu Wakenya na Waganda hawatakaa watusubiri. Badala yake watatimua mbio, na kutwambia nyie nendeni polepole na mtakapokuwa tayari basi mtatukuta MBELE! Upolepole ni ugonjwa kama ebola ya kiuchumi na unatutafuna sana. Hatutaki kufikiria nje ya hilo boksi la WOGA na UPOLEPOLE.
Ninaelewa ni utamaduni ambao ni zao la watawala wetu kuedekeza ufisadi. Maana wananchi hawawezi kujenga moyo wa kuwaamini watu wanaowangoza. Kila anayetokea wanamwona kama fisadi. Anakuja kutufisadi.
 
Bwana msemakweli

Unachosema hapo juu hakiendani na scientific polling ya Watanzania iliyofanywa na Shirika la Twaweza mwezi uliopita juu ya swala hili, ambao asilimia 82% wanapendelea single tourism visa ya Afrika Mashariki.

Anachosema January Makamba kwamba Tanzania inabidi itoe uongozi na mwelekeo (leadership) katika mambo ya Jumuiya ni jambo linaloendana na maoni ya wananchi wengi. Sera za sasa za Serikali ndizo ambazo zinakinzana na matakwa ya wananchi. Soma zaidi:

More than half of citizens approve of the following proposals

  • A single tourist visa for the region (82% approve)
  • Ability to travel across the region with a national identity card (82% approve)
  • Joint infrastructure projects (78% approve)
  • Free movement of labour (69% approve)
  • A common passport (67% approve)
  • Tax free trade (58% approve)
  • A single currency (55% approve)

Eight out of ten citizens (80%) think Tanzania should remain in the East African Community (EAC). In addition, nine out of ten (85%) approve (or strongly approve) of greater integration with Kenya and Uganda in particular. Six out of ten citizens also support increased integration with Rwanda (62%) and Burundi (59%).

Aside from supporting integration, citizens broadly believe the impact of the East African Community will be positive. The strongest vote of confidence is economic, twice as many citizens think that the EAC will have positive impact (42%) as compared to negative (20%) on the economy of the country. Similarly more citizens think the EAC will have a positive rather than negative impact on security (37% against 20%), politics (35% versus 25%) and culture (33% versus 24%).

SOURCE: Let?s build one house! What Tanzanians think about the East African Community :: Uwazi :: Publications :: Twaweza.org
Huo utafiti umefanyika kwa watanzania waishio kenya au? Maana sijawahi sikia walau jirani yangu kunidokeza kuhusiana na hilo, sasa sijui hiyo idadi ya 8 out of 10 inakujaje
 
Last edited by a moderator:
Kazi yako ni kuchambua WATU ,huyu YUKO hivi na vile,matusi na kejeli,Je,vidole vinavyokuuliza wewe,umewahi kujiuliza wewe ni nani??- Wewe Kesha mitandaoni ukitukana na kukejeli WATU,-Mungu anapowafungulia milango ya mafanikio UTABAKI unashangaa na roho yako mbaya,endeleeni kusajili majina bandia iLi mtukane na kukejeli VIZURI hapa JF ,mwisho wa siku utaisoma namba kimyakimya Mungu anapowatendea maajabu hao unaowatukana na kukawakejeli,Tukana sana-maana inakusaidia kupunguza stress ZAKO,pengine isingekuwa JF ungekuwa ulishajinyonga kwa msongo wako wa mawazo,maana stress ZAKO unazimalizia JF ukitukana na kukejeli WATU-Janauary Yusuf Makamba -Kama Mungu amemuandikia kuwa Rais,porojo ZAKO hapa JF,hazitamzuia,Kejeli ZAKO,dhihaka ZAKO,Nyongo yako,wala sii CHOCHOTE Kama Mungu amemuandikia ,So komaa na porojo wakati mwenzako anachanja Mbuga za maisha yake.
 
Hivi wanajamvi, mbona wakati mwingine hamueleweki!

Hivi ni mgombea gani asiyekuwa na udhaifu? Tangu baadhi ya viongozi na wasio viongozi watangaze nia ya kuwania nafasi mbalimbali humu mnakuja na mijadala inayokatisha tamaa. Sijaona hata siku moja kati yao mnamsifia kwa weledi na uwezo. Wote ni wabaya mbele zetu, Hivi tunahitaji aina gani ya kiongozi mwenye tabia, uwezo tofauti na waliojitokeza?

Mimi namchukulia J Makamba kama kijana mtanashati, mwenye uwezo kiakili, mbunifu na mwenye kuijua dunia ya leo inayoendelea kwa kasi sana. Sasa masuala mengine yanatafsiriwa kama chuki binafsi dhidi yake na kama yupo mnyoofu kwa asilimia 100 basi mleteni humu jamvini tumjadili.

VIVA MAKAMBA VIVA KIJANA! Keep it up!

Alifanya nini? Ana weledi gani? kama ni utanashati wako akina mapedeshee kibao, sie tunataka uwezo na historical background yake, hebu weka CV yake tuanzie hapo!
 
Political culture au niseme economic culture ya WaTZ/Wabongo ni kwamba tu WOGA sana wa kufanya mabadiliko au kujaribisha njia mbadala kwa kila kitu. Kila siku tunaimba (kama zilivyo nyimbo nyingi) wimbo wa 'ujasiriamali' lakini tunasahahu kuwa moyo wa ujasiriamali ni kuwa tayari to take risk. Sisi tunaogopa tukifanya mabadiliko (yaani kuacha kufanya yale yale kwa namna ile ile, watu wale wale, fikira zile zile) ili tusilete VITA, ili WaKenya wasituibie ardhi yetu, waGanda wasichuku ajira zetu, nk. "Watuache twende polepole" Profesa wa Kichina aliwahi kutamka katika hotuba zake. Tunaongozwa na falsafa ya kijadi ya waswahili ya 'polepole ndio mwendo', ama 'haraka haraka hiana baraka'. Wenzetu Wakenya na Waganda hawatakaa watusubiri. Badala yake watatimua mbio, na kutwambia nyie nendeni polepole na mtakapokuwa tayari basi mtatukuta MBELE! Upolepole ni ugonjwa kama ebola ya kiuchumi na unatutafuna sana. Hatutaki kufikiria nje ya hilo boksi la WOGA na UPOLEPOLE.
Ninaelewa ni utamaduni ambao ni zao la watawala wetu kuedekeza ufisadi. Maana wananchi hawawezi kujenga moyo wa kuwaamini watu wanaowangoza. Kila anayetokea wanamwona kama fisadi. Anakuja kutufisadi.

Na waendelee basi. Sisi hatujawakataza. Sio lazima watusubiri. Mi naona kwanza issue nzima ya EAC ni upumbavu, the earlier we realise it the better. Kama ni kujenga One stop border posts tuzijenge basi pia Zambia na Msumbiji, kama ni kupunguza gharama za kupiga simu na ticket za ndege iwe ni kwa jirani zetu wote na siyo Kenya na Uganda tu. Yale mambo ambayo yataumiza nchi basi yapingwe kwa nguvu zote. Tanzania iendelee kushirikiana na majirani zake wote na siyo wachache tu! Ila political federation ni absolute NO!
We huoni wakenya ethiopia wapo, somalia wapo, south sudan wapo na wanajaribu kupush ili nchi hizo nazo ziingie EAC. Yote hayo ni kwa maslahi yao! Hii EAC ya sasa imekaa kuwafaidi wachache tu.
 
Back
Top Bottom