Nina wasiwasi maisha kuwa magumu zaidi na ukosefu wa ajira kuongezeka awamu hii

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Watanzania wamejenga matumaini makubwa sana juu ya awamu ya hii ya tano kuleta mageuzi makubwa hasa katika maisha ya kawaida ya wananchi, lakini ipo hatari ya matumaini haya kutopatikana na hatari zaidi pale jamii itakapofikia hatua ya kuona ufisadi ni bora maana maisha yao yalikuwa mazuri lakini sasa mbona maisha yanakuwa magumu?

Hakuna anayeweza kukubali kuwa mambo kwenda vizuri inaweza kuleta maisha magumu na mambo yaliyokuwa yakienda vibaya ilileta maisha kuwa mepesi kwao. hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ndicho kipimo cha uzuri au ubaya wa misimamo ya serikali.

Maisha ya kawaida ya mwananchi yanategemea vitu vitatu;
1. Mahitaji ya wananchi hawa ambayo yanatengeneza ajira kwa watu wengine.

2. Hali ya uwezo wa wananchi kumudu gharama za mahitaji yao ambayo inaungana na kipengele cha kwanza kutengeneza soko.

3. Ni uzalishaji ambao unahakikisha upatiukanaji wa suluhisho la mahitaji ya watu.

Kitu kimoja kikikosekana katika hivyo hakuna ajira na panapokuwa hakuna ajira maana yake watu hawapati kipato na kwa kuwa hakuna anayeweza kujihudumia mahitaji yake yote basi maisha yanakuwa magumu kwa watu kukosa kupata huduma au kukosa uwezo wa kumudu mahitaji yao.

Kinachonipa wasiwasi ni mipango ya serikali kuonekana kutaka kuendesha uchumi kwa staili ya mabibi zetu ambao walikuwa wanachukua fedha na kununua mashamba huku wao na watoto wao wakiishi maisha magumu lakini wakitumia kipato cha familia kununua rasilimali zenye ambazo mbele ya safari mashamba hayo yanakuja kuwa na thamani lakini yakiwanufaisha wajukuu na sio mabibi na mababa.

Au tunaweza kusema serikali inaonekana kutaka kuendesha uchumi unaoendeshwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sasa ya kuwekeza katika miradi ya kupata faida katika mda mrefu na kushindwa kulipa madeni au mafao ya wafanyakazi wanaostaafu kwa sasa.

Dira ya mipango inaonekana kujikita katika kuweka miundo mbinu ambayo returns zake sio katika kipindi kifupi kijacho cha miaka mitano, kulipa madeni na pia kupunguza mchango wa wahisani katika bajeti yetu.

Wasiwasi wangu ni kuwa fedha itakuwa ngumu katika mzunguko na hii itasababisha wananchi wengi kukosa uwezo wa kumudu kulipia mahitaji yao.

Wananchi wengi wanapokosa kumudu kulipia mahitaji yao kutaathiri uzalishaji kwa kuwa uzalishaji unategemea soko ambalo ni uwezo wa kununua wa wananchi dhana ya kudhani tunaweza kutengeneza uchumi wa viwanda kama mkombozi inaweza kuwa na uchungu mkali kwa wananchi na wakaichukia dhana hiyo kwa sasa kutokana na aproach.

Bado dhana hiyo inaweza kutokuzaa matunda mbeleni kutokana na
1. Kama ambavyo bibi anaweza kutumia fedha yake na kusacrifice maisha mazuri akawekeza katika rasilimali lakini umasikini huu ukawafanya mababa wasiwape malezi mazuri wajukuu na wanapokuwa wanakuta mashamba yenye thamani lakini wanayauza kwa bei za kutupa kutokana na kutokuwa na maandalizi ya kutumia rasilimali hizi kwa faida na hivyo wanaona kuyatoa ili kupata mkate wa siku.

2. Jamii ikichukia misimamo ya sasa ya inaweza kuona ufisadi ndio siasa safi na jamii ikarudi katika siasa za kila anayepewa madaraka anatumia kwa tumbo lake na kuitia hasara jamii na hivyo jamii isije kufaidi rasilimali zinawekezwa sasa na wajukuu wakaendelea kuishi maisha magumu kama wazazi wao.

Ki mtizamo wangu jamii inatakiwa kutambua kuwa kujenga uchumi, kwa kuwa mahitaji ya wananchi yako palepale basi kunabaki kunategemea mambo makuu mawili kujenga uwezo wa wananchi kumudu gharama za maisha na kuzalisha kukizi mahitaji ya wananchi.

Kama kufanya maandalizi ya wananchi kuzalisha kutaathiri uwezo wa wananchi kumudu gharama basi maandalizi hayo hayatakuwa na maana kwa kuwa hata vitakavyozalishwa havitakuwa na soko na maandalizi hayo hayatakuwa na maana maana wazalishaji wataacha kuzalisha kwa kukosa soko hata kama miundombinu ipo.Kama kuwezesha wananchi kutaathiri miundombinu ya zalishaji ni wazi kuwa wananchi watakuwa na uwezo wa kunua lakini wazalishaji watashindwa kuzalisha kwa kuwa miundo mbinu hakuna.

Kwa kuwa mzunguko wa fedha unapita kwa wananchi unaenda serikalini kupitia kodi na kurudi kwa wananchi. kitendo cha serikali kuchukua fedha nyingi hizi za kodi na kuziweka katika kulipa madeni na kuwekeza katika miradi isiyorudisha fedha hizo kwa wananchi haraka kutafanya mwaka kwa mwaka fedha inayozunguka kupungua na hivyo kuathiri uwezo wa wananchi kumudu gharama.

Hii itaathiri ajira, itaathiri uzalishaji na hayo yakiathirika mapato ya serikali pia yatapungua, nadhani suluhisho ni kuwekeza katika miradi mikubwa kiasi, kuwekeza katika miradi yenye returns haraka kiasi, kuchochea sekita zote ili kila penye opportunity ya kutoa ajira itoe ajira itafanya watu wengi kuwa na uwezo wa kumudu gharama, hii itasababisha kuongezeka kwa ajira maana uzalisha unategemea uwezo wa kulipa wa watu, hii itasabisha serikali kuongeza kipato kwa kupata kodi nyingi kutoka transactions nyingi zinazofanyika, kuongezeka kwa mapato mwaka hadi mwaka ndiko kutajenga uwezo wa serikali kwenda ikitanua ujenzi wa miundo mbinu ya uzalishaji zaidi.
 
maisha magum sana kitaa,mwakan lazima home kulima nshastukia hiki kipindi cha magu heri kulima tu ntapata mtaji kuniboost mtaji wa mwaka keshokutwa
 
Hali itatengemaa baada ya miaka 2. Kwa sasa ni tufunge mikanda ya mkia wa Taa
Miaka miwili ni michache sana. Kwa hali iliyokua imefika Tanzania sio rahisi hali kuwa kwenye mstari kwa mida huo
 
ajira zaidi ya 75k mwaka ujao wa fedha

ndugu yangu ajira hazitengenezwi na serikali bali ajira zinatengenezwa na "transactions" kukiwa na opportunities za transactions nyingi maana yake watu wengi wanakuwa na uwezo wa kuingia katika transactions hizo kutoa huduma au bidhaa na hizo ndizo ajira.

kukiwa na transactions nyingi wakati serikali inapata mapato yake kupitia kodi za transactions inakuwa serikali mapato yataongezeka na hapo ndipo inakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi na kutoa huduma nyingi zaidi.

lakini kama serikali itafanya maamuzi ya kwenda ikikusanya kodi inaingiza kwenye miundo mbinu asilimia kubwa wakati asilimia kubwa ya fedha hizo zinaenda kuchukua vifaa na wataalamu kutoka nje ni fedha kidogo sana itakuwa ikirudi kwenye mzunguko na hii itaathiri transactions.

yawezekana mwaka ujao 75K wakaajiriwa lakini withini miaka mitano ijayo ugali wa maisha utakuwa umepanda sana na vipato wanavyopata watu vimekuwa vidogo kulinganisha na mahitaji.

vipato vikiwa vidogo maana yake watapunguza manunuzi na je zile bidhaa watazoacha kunuanua waliokuwa wakiziuza watapata ajira au watapoteza?

kama hao hawauzi je serikali itatoa wapi kodi?
 
maisha magum sana kitaa,mwakan lazima home kulima nshastukia hiki kipindi cha magu heri kulima tu ntapata mtaji kuniboost mtaji wa mwaka keshokutwa

kwanza ukafanye tathmini inaonekana una mda mrefu hujaenda kijijini ukaona uliowaacha wanalima wakoje.

lakini kumbuka ninyi mlioko mijini ndio wateja wa wakulima sasa ninyi yakiwashinda mijini unadhani ukienda kijini utalima kumuuzia nani? maana yake watu wa mijini maisha yanavyokuwa magumu wa vijijini yatakuwa magumu zaidi maana wateja wao watapungua na aliyezoea kununua bila kuuliza bei watakuwa wakilialia ili kupunguziwa. kimsingi biashara ni wateja na mambo yakiwaendea vibaya wateja wako na wewe unakuwa na hali tete zaidi.

kama ulivyoona kipindi cha mdororo wa uchumi ulivyotokea kule na sisi tukaathirika ndivyo unavyotokea mijini na vijinini wakaathirika labda ukalime kula tu.
 
Hali itatengemaa baada ya miaka 2. Kwa sasa ni tufunge mikanda ya mkia wa Taa

unaongea kama vile kinachobadili mambo ni mda pekee.

hapa tuwekane wazi kuwa mfano kuna mpango huu ambao ukitekelezwa ndani ya miaka miwili tutapata nafuu kutokana na hili ambalo litaanza kuzaa matunda.

mimi nasema hali itakuwa mbaya kwa sababu mizunguko ya fedha ilikuwa mingi inategemea fedha ambazo zilikuwa zinapita njia chafu kwa serikali kupata hasara. sasa unapoanza kufunga njia hizi chafu mizunguko ya fedha inaathirika.

kulitakiwa kuwe na program ya haraka kutengeneza mizunguko ya fedha mingine kupitia njia halali lakini sasa inaonekana mizunguko inafungwa na fedha zinazokusanywa zinafungwa katika uwekezaji wa mda mrefu kama miundo mbinu.

yaani fedha zinazoingia serikalini nyingi hazirudi kwa wananchi kuzunguka tena na zile zinazorudi zinakuwa kidogo kusababisha mizunguko mingine kukosa pesa na kufunga na huko wenye kupata riziki zao huko watakoma. baada ya wao kukoma serikali haitapata mapato

sasa ni kitu gani unachokiona kuwa ndani ya miaka miwili mambo yatakuwa mazuri wakati mambo yanategemea kuzunguka kwa fedha na mzunguko unaonekana kuwa na shida ya kutokuwa endelevu?
 
kwanza ukafanye tathmini inaonekana una mda mrefu hujaenda kijijini ukaona uliowaacha wanalima wakoje.

lakini kumbuka ninyi mlioko mijini ndio wateja wa wakulima sasa ninyi yakiwashinda mijini unadhani ukienda kijini utalima kumuuzia nani? maana yake watu wa mijini maisha yanavyokuwa magumu wa vijijini yatakuwa magumu zaidi maana wateja wao watapungua na aliyezoea kununua bila kuuliza bei watakuwa wakilialia ili kupunguziwa. kimsingi biashara ni wateja na mambo yakiwaendea vibaya wateja wako na wewe unakuwa na hali tete zaidi.

kama ulivyoona kipindi cha mdororo wa uchumi ulivyotokea kule na sisi tukaathirika ndivyo unavyotokea mijini na vijinini wakaathirika labda ukalime kula tu.
daah mkuu kweli but natak tu kupunguza matumizi mana nliweka watu shamba so narud mwnyw kusimamia aisee mjin biashara zimekua ngum
 
Nilisha wai sema humu ndan tena nilipo ona Magu anawatoa Noma wafanyabiashara nikajua bongo tumekwisha! Nawaambien Maisha yatakuwa magumu kuliko unavyofkiri, wanye akili wanajua bado hatua chache sana mbwembwe ziishe na bongo kwake itakuwa chungu
Nawashauri jamani tuacheni kulalamika tufanye kazi! Hamna atakayekuletea mahitaji bila kufanya kazi
 
ndugu yangu ajira hazitengenezwi na serikali bali ajira zinatengenezwa na "transactions" kukiwa na opportunities za transactions nyingi maana yake watu wengi wanakuwa na uwezo wa kuingia katika transactions hizo kutoa huduma au bidhaa na hizo ndizo ajira.

kukiwa na transactions nyingi wakati serikali inapata mapato yake kupitia kodi za transactions inakuwa serikali mapato yataongezeka na hapo ndipo inakuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi na kutoa huduma nyingi zaidi.

lakini kama serikali itafanya maamuzi ya kwenda ikikusanya kodi inaingiza kwenye miundo mbinu asilimia kubwa wakati asilimia kubwa ya fedha hizo zinaenda kuchukua vifaa na wataalamu kutoka nje ni fedha kidogo sana itakuwa ikirudi kwenye mzunguko na hii itaathiri transactions.

yawezekana mwaka ujao 75K wakaajiriwa lakini withini miaka mitano ijayo ugali wa maisha utakuwa umepanda sana na vipato wanavyopata watu vimekuwa vidogo kulinganisha na mahitaji.

vipato vikiwa vidogo maana yake watapunguza manunuzi na je zile bidhaa watazoacha kunuanua waliokuwa wakiziuza watapata ajira au watapoteza?

kama hao hawauzi je serikali itatoa wapi kodi?
75k serikalini
15k bomba la gesi -litaingiza hela-
3k kujenga bandari tanga -pato kwa taifa-
50k viwanda vya kati kuhonda morogoro kihonda -miaka 2 ijayo, pato kwa taifa-.
.
.
.
.
5k viwanda vya mbolea
.
.
.
mfanyakazi mmoja anahudumia wastani wa watu 5. mategemeo ni malofa 4m kuboreshewa maisha kwa miaka 5 ya awali.
 
Nawashauri jamani tuacheni kulalamika tufanye kazi! Hamna atakayekuletea mahitaji bila kufanya kazi

yaani wewe ndio huelewi kabisa.

kazi unayofanya inategemea mwenye shida aliye na uwezo wa kukulipa ndio umfanyie shughuli anayotaka alafu akulipe.

sasa tunasema huu utaratibu wa serikali kuziba fedha zilizokuwa zikipita njia haramu lakini zinaingia kwa wananchi hapo wanapozipata wanawapa wengine kwa kununua mahitaji yao na hawa wanapozipata wanagawa kwa wengine, maana yake zinaanzia njia chafu lakini zinaanza kutembea katika biashara za kawaida kwenye jamii.

ukiziba mianya hii ile misululu yote iliyokuwa nyuma ya fedha hizi imekata ingawa yenyewe ilikuwa halali.

sasa umekata mrija uliokuwa ukileta fedha chafu umeleta mrija gani umaoleta fedha safi ili misululu hii iendelee maana kazi katika misululu hii zinategemea fedha hizi zilizokuwa zikipita.

fedha kama hazipo ndio kazi hakuna.

sasa wewe unapiga porojo fanyeni kazi kulipwa nini? maana tukikueleza mizunguko ya fedha inayosababisha watu wafanye kazi imekata?

kibaya zaidi ni fedha hizi sasa zinatumika kwenye miradi ya ujenzi ambako asilimia kama 75 ya fedha hizo za ujenzi zinaishia kwenda nje ya nchi. yaani katika hali ya huko nyuma kama serikali ilikuwa ikikusanya bilioni 800 kwa mwezi na sasa inakusanya 1300. maana yake mwezi unafuata hii bilioni 500 ambayo serikali haikukusanya iliendelea kuzunguka ikitengeneza ajira kwa watu. katika hizo mia nane kiasi kikubwa kilirudi katika mzunguko pia hivyo ungekuta mzunguko uko stable kila mwezi bilioni mia nane zinapatikana. hawa jamaa walipokuwa wakiona mambo yanataka kwenda mrama wanakimbia kukopa ili waendelee kubaki palepale.

kwa sasa wanakusanya zote 1300, na wamepunguza utegemezi wa nje lakini wanataka kuongeza kasi ya miradi ya maendeleo. miradi inayopangwa inatumia fedha nyingi kuwekeza na kurudisha ni taratibu maana yake mizunguko ya ndani itaathirika kiasi cha kusababisha kupunguza ajira. hivyo kiasi ambacho serikali itakuwa ikikipata kupitia kodi kitaenda kinapungua kwa sasa kutokana na transactions kupungua.

uwezo wetu wa kupata mashine, bidhaa, huduma na kadhalika unatokana na kiasi cha fedha za kigeni tunazozipata. kama kiasi kiko palepale unapanga miradi mingi ya kutegemea vitu vingi kutoka nje maana yake ni kuporomosha shilingi ingawa nasema fedha kupungua.

nakumbuka tangu primari wanafundisha ukutaka kuimarisha uchumi punguza imports ongeza exports sasa hili lina maana gani? au ni kufikiria tukijenga kitu fulani tutafanya hiki tufanya hiki tutaongeza kile bila kuanza kubalansi sasa kuwa tangu sasa manunuzi yetu ya nje hayatazidi mapato yetu ya fedha za kigeni.

na wakaenda mbali zaidi huko shule ya msingi kuwa inabidi kununua mashine na sio bidhaa kwa maana kama ukiuza korosho, ukauza madini nunua mashine na sio bidhaa ili utumie fedha kidogo kununua mashine na kuanza kuzalisha.
 
Mie naombea azidishe mbinyo mpaka kila mtu awe anakula jasho lake halali!
 
Mwandishi umeandika pointi kabisa, lakini napingana na wewe pale unaposema wanainchi wataona bora ufisadi
lakin tukija kwenye ukweli hakuna yule mwananchi wa chini kama mimi aliyekuwa ananufaika moja kwa moja na ufisadi mafisad ni wachache halafu wanaficha fedha nje ya nchi, labda kama unazungumzia wananchi hawa walioathirika na utumbuaji majipu...!!
 
75k serikalini
15k bomba la gesi -litaingiza hela-
3k kujenga bandari tanga -pato kwa taifa-
50k viwanda vya kati kuhonda morogoro kihonda -miaka 2 ijayo, pato kwa taifa-.
.
.
.
.
5k viwanda vya mbolea
.
.
.
mfanyakazi mmoja anahudumia wastani wa watu 5. mategemeo ni malofa 4m kuboreshewa maisha kwa miaka 5 ya awali.

unajua unalisema kama ni utani na kulichukulia kama neno la kuwakejeli wenye siasa tofauti na wewe neno lofa lakini in real sense inawezekana sote watz ni malofa.

kama tuna mali nyingi na hatuwezi kuzitumia kupata maisha mazuri, tunabaki kupigana vijembe vya siasa wakati tunaendelea kupata shida huo ndio ulofa.

kuwa na miradi mikubwa kama hii si jambo baya lakini ni kwa nini tufanye miradi mikubwa na miradi midogo yenye impact kwenye jamii moja kwa moja na matokeo ya haraka.

mfano chukulia sekita ya nguo, hebu nenda kariakoo au watazame watu unaowaona na ujilize nguo walizovaa asilimia kubwa zimetoka wapi? achilia mitumba. ni kwa nini tusiwe na programu za kuondoa nguo za nje katika soko letu kwa kuangalia kuwa tukiagiza vyerehani na vifaa kidogo vya ushonaji tunaweza kujikuta kwa mwaka katika sekita ya mavazi itakuwa fedha za kigeni tunazopeleka nje kununua vifaa hivyo ni kidogo kuliko kununu nguo kila siku.

tunawafukuza vijana waende wakalime wakati wanaolima wenyewe wamechoka kwa nini tusibadilishe viwango vya kodi katika vyerehani viwe chini, kodi kwenye nguo za nje ziwe juu alafu tuwapatie vijana wetu kutoka veta mitaji waanze kushona nguo.

ulofa ndio unaotufanya tufikiri kijana akosome veta cherehani alafu arudi kijijini kulima wakati huo aliyesoma veta malyasia ndiye anatushonea nguo hapa.

serikali ndiyo yenye jukumu la kutengeneza mazingira haya ambayo yanacreate opportunity kwa watu lakini wao wameacha bidhaa ya nje inachukua wateja wa ndani wao wanabaki kuongea tu na kudhani ni lazima waanzie viwanda katika ngazi za juu sana.

kanunue kitambaa kwa sasa ushone nguo alafu ulinganishe na nguo ya nje yenye ubora huo uone kipi bei iko juu? nguo ya nje bei iko chini lakini jiulize kama ukinunua nguo ya hapa, kama kitambaa kimetengenezwa hapa na ukabana soko la pamba wakanunua hapa maana yake kuna asilimia imeenda kwa mkulima, kuna asilimia imemwajiri mtanzania katika kiwanda cha kutengeneza kitambaa, kuna asilimia imemwajiri mtanzania katika kutengeneza nguo, kuna asilimia imemwajiri mfanyabiashara muuza nguo, na serikali kote huko imepata kodi. bado fedha hiyo inaendelea kuzunguka kutengeneza ajira kwa wengine maana kila aliyepata mgao wake naye anaenda kufanya manunuzi.

lakini ukinunua nguo nje fedha yamkulima, fedha ya ajira za viwanda zote unapeleka nje na ndio kwaheri. unabaki na kodi serikali inayoweka kwenye nguo na fedha ya mfanyabiashara wa nguo tu.

hivyo mzunguko mwingine unapoanza watanzania kwa kununua nguo ya hapa tunakuwa na nguo ambayo unayo wewe na fedha asilimia kubwa iko kwa watanzania ikizunguka lakini kwa nguo ya nje fedha nyingi inakuwa imepotea wakati tunabaki na fedha kidogo na nguo.

raisi maepiga kelele sana wakati wa kampeni eti kwa nini hatuzalishi hata njiti za meno, kwa nini hatuzalishi vitambaa vya jasho.

tulitegemea awawezeshe watanzania kupitia mitaji, atumie viwango vya kodi kuwalinda wazalishaji wa ndani.

kuna watanzania wanatengeneza friji tulitegemea katika mpango wake wa viwanda ni kusema nataka huyu anazalisha friji ateke soko la ndani la friji na wa nje watajazia pale ambapo hawezi.

tunalalamika kila siku sido ni kiini macho. kuna watu ni wajasiliamali wako chini ya sido wanataka kuzalisha bidhaa lakini sido inafanya michezo ambayo watu wanabaki kuzalisha bidhaa zisizo nasoko kama eti bidhaa za mianzi.

tuna matunda kwa nini tusitumie sido kuunda vikundi vya vijana kuzalisha juisi kutumia matunda yetu. lakini sido inauza chupa ya kufangashia juisi shilingi mia tano wakati chupa yenye juisi shilingi mia saba.

kuna veta zinafundisha kutengeneza viatu kwa nini serikali isitengeneze program za kuwawezesha vijana hawa kuteka soko la viatu la ndani ambalo nikubwa na linaweza kutoa ajira za kutosha.

sisi sera za viwanda tunafikiria mitaji mikubwa hatuangalii viwanda kama uzalishaji na uzalishaji huu ndio tunatakiwa kuuchukua watanzania wenyewe waanze kuzalisha bidhaa hizi na ndani ya miaka kadhaa hawa watu wanaoingia wataenda wanakua na kufika huko pa kuwa na viwanda vikubwa.

tunategemea wageni waje kujenga viwanda vya bajaji, pikipiki sio kuja kupaki maji kwenye makopo.

na serikali ikiwekeza katika uzalishaji wa bidhaa hizi ambazo tunaziona ni kero na ambazo zitatusaidia kuimarisha uchumi wetu kwa fedha zetu za kigeni kubaki kufuata vitu vikubwa tusivyoweza kuzalisha tu.
 
Mwandishi umeandika pointi kabisa, lakini napingana na wewe pale unaposema wanainchi wataona bora ufisadi
lakin tukija kwenye ukweli hakuna yule mwananchi wa chini kama mimi aliyekuwa ananufaika moja kwa moja na ufisadi mafisad ni wachache halafu wanaficha fedha nje ya nchi, labda kama unazungumzia wananchi hawa walioathirika na utumbuaji majipu...!!

hujanielewa na ukinielewa hutaenda kwenye hadithi.

sasa wewe kila siku unafanya kazi zako unapata kipato. tumetoka katika mazingira ambayo tuliambiwa wafisadi walikuwa wanatunyonya lakini wakati huo unafanya kazi zako unapata kipato unajitosheleza.

sasa akaja mwingine akasema amedhibiti mafisadi lakini wewe huku chini kupata fedha inakuwa ngumu watu hawana fedha na mfano kama una duka watu wakiwa na fedha ndio wanakuja kununua lakini kwa kuwa hawana fedha hawaji sasa utabaki kuongea hadithi za mafisadi au utasema mimi nataka maisha ambayo nafanya shughuli napata kipato.

matokeo katika maisha ndio yatafanya watu waone ni mfumo gani unafaa na sio hadithi tena.
 
Mie naombea azidishe mbinyo mpaka kila mtu awe anakula jasho lake halali!

hilo hatulikatai lakini hawa wanaminya tu, walitakiwa kuminya mifereji haramu na huku wakichimba mifereji halali.

yaani ni kama tunaongozwa na idara ya polisi ambao kazi yao ni kukamata waarifu tu. kasi tunayoisikia katika kutumbua majipu tuisikie katika sekita zote zilizokuwa zimelala na watanzania wakionekana wavivu kumbe refa hajitambui kusimamia kanuni za mchezo.

na huyu refa ajitambue kazi yake si refa tu kutoa kadi nyekundu bali sheria za mchezo anatunga yeye, kocha ni yeye, mdhamini ni yeye na ni kocha mchezaji ambaye ikibidi anaingia uwanjani anacheza.
 
Back
Top Bottom