Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Mimi si muumini wa kanisa la ufufuo na uzima lakini ni mkristo. Siku moja nilifika pale kanisani. Ukifika pale unapoingia upande wa kushoto kuna banda limejengwa kama ghorofa likiwa limewekewa chuma za mataaluma kama zile za reli kama nguzo zake. Sasa wanaposali kule juu huwa wanasali huku wanatembea na kuruka ruka. Niliona lile banda linayumba sana kutokana na watu waliokuwa kule juu kusali huku wakiruka ruka na kucheza. Nilipoangalia vizuri zile chuma nikaona kwa chini zimeshaliwa na kutu kiasi kwama kuna siku isiyokuwa na jina inaweza kutokea ajali ya lile banda kudondoka wakati kwa chini kuna watu wamekaa kwani lile kanisa ni finyu lakini waumini ni wengi sana.
Ninaomba uongozi wa kanisa uchukue tahadhari kwani ukiangalia uimara wa zile chuma na mzigo wa watu kule juu ni kwamba zile chuma znazidiwa na wakati huo huo kwa upande wa chini huwa kunakuwa na waumini wakiwa wanasali sasa likija kuanguka litaua watu wengi sana. Tusingoje mpaka litokee la kutokea kama kule Nigeria ndipo tuanze kuunda tume. Naomba pia uongozi utafute sehemu nyingine yenye nafasi kwani pale ni padogo kutokana na wingi wa waumini wanaokuja kusali pale kwani pia kuna sehemu wameunga unga tu lakini kuna bonde. Vile vile eneo la parking ni dogo kiasi kwamba waumini wanapaki barabarani. Majeshi majeshi! Majeshi ya Bwana!