habari za uzima wananzengo Nina mpango wakuanzisha biashara ya asali mbichi
[emoji117] Nataka nijue upatikanaji wake kwa Bei ya jumla
[emoji117]Bei yake ili na Mimi nikiingia mtaani nisambaze bidhaa nipate faida
[emoji117]Kama Kuna mtu anaconnection tuwasiliane Dm
Nb napatikana mwanza
Kwa uzoefu wangu unaweza kupata asali kutoka mojawapo ya mikoa hii: Singida, Tabora, Njombe na Katavi. Huko ndiko nina uzoefu nako zaidi. Bei ya asali inategemea na msimu.
Msimu wa Asali hutegemea na kalenda ya nyuki. Kwa ufupi bila kukuchanganya sana, msimu wa asali hutegemea na mkoa husika ila mara nyingi ni kipindi cha mwisho wa mvua za vuli, ama mwanzo wa kiangazi, ama pale unapoona maua kwenye miti yameanza kupungua na matunda yameanza kutengenezwa kwenye miti.
Bei ya asali kama nilivyosema hutegemea na msimu na vilevile mkoa husika. Mara nyingi asali inauzwa kwa ndoo ya lita 20 ambapo bei inaweza kuwa kati ya Tsh 100K mpaka 150K, pengine hufika mpaka 200K.
Ushauri:
1. Asali kama ilivyo biashara nyingi za bongo kumejaa madalali. Hivyo kuwa makini usiwe mwepesi sana wa kufanya biashara kwa njia ya simu na kutuma pesa yako bila kufika mwenyewe.
2. Changamoto ya asali watu huweka maji na wengine huichemsha ili kuongeza ujazo/uzito. Hivyo kuwa makini ili usinunue asali feki ukapata hasara.
3. Kama ni mgeni sana, nakushauri ufanye utafiti wa kutosha kabla hujaanza hasa ujue asali nzuri ni ipi na unaitambuaje na upate connection nzuri kutoka vijijini moja kwa moja.
4. Ukitaka upate faida nzuri inabidi ufanye packaging vizuri na tafuta angalau brand yako mwenyewe.
5. Kwa ushauri zaidi unaweza kutembelea ofisi za watu wa maliasili makao makuu ya Wilaya yako. Huko utapata ushauri zaidi ikiwamo masuala ya vibali n.k
Kila la kheri Mkuu. Hopefully umepata mwanga japo kidogo.