mbegubora29
Kama una NGUVU za kuwamudu wote wawili.
Kama una uhakika UTAFANYA UADILIFU baina yao.
Kama una kipato cha kuwatosheleza wote.
Oa tu!
Wanawake wachoyo sana,kwa wanawake wenzao.
Wanajijua wao ni wengi na wanaume ni wachache.
Bado hawataki kushea.
Yaani wengi wako tayari kuona baadhi yao wakikosa raha/utamu kisa hawapendi kushirikiana.
Yaani wengi wako tayari kuona wenzao wanakufa kwa kiu ilhali wao wana chemchem.kisa hawataki kushea.
Iko hivyo,hata wanaume nao wangekuwa wengi kuliko wanawake,
Wanaume nao wangeshea wanawake.ila BAHATI nzuri hako hivyo.
Wapo wanawake waelewa,
Wenye huruma kwa wanawake wenzao,
Wanaowapenda wanawake wenzao,
Wanapenda nao wapate raha/stara na utamu wa ndoa.
Wanashirikiana katika ndoa.
Naamini na mkeo anaweza kuwa kwenye kundi hili.
Usichepuke,
Usizini,
Usilete watoto wa nje ya ndoa.
Usilete maradhi ndani ya ndoa!
Oa!