Kwanza mleta uzi wewe mwenyewe Dalali.
Umeshindwa kupost na kuanishia uzalishaji wako.
Kwa kukusaidia tu,kama upo Jiji la Dar,na kama ni mkulima,basi wakulima wenzio 90% wanatumia madalali.Na 10% hufanya bisahara wao wenyewe.
Na ndio maana ukienda kariakoo na masoko makubwa ya kushusha mizigo kuna watu pale huwa hawatoki siku zote wapo pale na ikifika saa tano sita huwaoni.Wale ndio Madalali wenye kuchukua mzigo shambani na kupelekea wanunuzi ambapo wao mnapata bei kisha wao wananunua kwa jumla na kumuuzia Mfanyabiashara wa mwisho.Bila dalali kwenye mazao ya kilimo kwa shamba hilo utatafuta wateja hadi udate.