Nina mashaka na kipimo cha MRDT

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
2,633
Reaction score
5,615
Ndugu,

Hicho ni kipimo cha haraka cha kupima Malaria. Na kimepigiwa promo sana na Serikali
na sasa kinatumiwa karibu kila mahali.

Shida niliyogundua , wengi wakipima kwa kipimo hiki huwa -VE ilhali homa wa nasikia. Na ukienda kupima na kile kipimo cha zamani cha slide na microscope inakuwa +VE wadudu wanaonekana mtu anatumia dawa na anapomaliza.
Nina experience ya watu zaidi ya 10 wamepata na kadhia hii.

Vipi nini wadau mna imani na kipimo hiki?
 
Truth Matters,
Unaweza ukawa sahihi, kama ni msomi read this... kama huwezi soma abstract inatosha kama unaelewa kiingereza and some few scientific words
 

Attachments

Mkuu,

Unaijua prevalence ya malaria hapa Tanzania kwa sasa?

MRDT inapima malaria antigen. Ni vigumu sana, na haiwezekani, MRDT isome negative halafu kwenye slide uwakute hao Malaria parasites.

Ili uwe na uhakika na kipimo unachokitumia, run control kwa kila kit unayoifungua and make sure unaangalia factors nyingine zinazoweza kukupa false (positive au negative) results hazipo.

Sio kila homa ni malaria.
 
Hospital nyingi zinatumia Duo anapima MRDT na Darubini
 
Hospital nyingi zinatumia Duo anapima MRDT na Darubini
Nadhani ni kwa sababu wanataka tu kuongezea mapato na au hawajiamini. MRDT ni nzuri zaidi ya slide.

Ili kupata majibu sahihi kwenye MRDT unahitaji kuwa na basic knowledge tu ya jinsi ya kuitumia na uhakikishe una-run control. Control iki-pass maana yake unaweza kuyaamini majibu yako.

Ili upate majibu sahihi kwenye glass slide lazima uhakikishe:
• Unaadaa vizuri slide
• Microscope unayoitumia iwe vizuri
• Msomaji pia awe competent

This makes MRDT more suitable over glass slide.

Hata hivyo; MRDT ni qualitative test, inakuambia tu kama kuna malaria au haipo. Kama MRDT itasoma positive ndio utumie slide kujua idadi yao, maana njia ya slide ni quantitative.

Ila all in all, MRDT ni nzuri zaidi, na itakusaidia kuendelea na slide kama itakuwa positive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…