Hivi mikia ni kina nani jamani?
usiongee kitu bila ya kuwa na uthibitisho nacho azam wanayo mipango ya academy na wameanza kuitekeza hao hapo juu ni Wachezaji waliofaulu kujiunga na klabu ya Azam fc katika mpango wa kuendeleza vipaji chini ya miaka14 wakiendelea na mazoezi leo kwenye uwanja wa azam complex chamazi \
source: azam official fb page
Na michuano ya shirikisho wamefikia 4 bora..eti? Na tatizo lingine viongozi type yako mkuu. Azam ina wachezaji wangapi kutoka kwenye hii accademy?
hivi wewee kwa akili zako azam imeanzishwa lini?? leo hii ina uwanja wake ina academy ipo kwenye kugombania nafasi ya ubingwa imekuwa mabingwa kimbe la mapinduzi still yote hayo yamefanyika ndani ya kipindi kifupip sana wakati timu ambazo zina zaidi ya miaka 50 zimeshindwa kufanya alafu bado unawabeza,huoni kwamba katika miaka 7-8 ijayo inaweza kutupleka mbali??? kweli watz tunaongozwa sana na hisia katika kufikiria baada ya kutumia common sense tu
hujui unalolisema ww academy huioni hapo nimekuwekea mpk picha unataka usaidiweje sasa!!!We unaongelea kombe la mapinduzi lenye timu hizi hizi za kuunga unga..ndio uipimie mafanikio team!!
Huku kwenye accademy ndipo walipotakiwa kuanza. Vinginevyo mwaka mwingine tena..team ile ile ama nyingine itakwamia mahali pale pale..tutakutana hapa kwa kejeli na vijembe..kisha mwaka mwingine tena..team ile ile ama nyingine itakwamia mahali pale pale.......................
Baada ya mechi ya jana kati ya Yanga na Al Ahyl..ambayo imehitimisha ndoto za Yanga kwenye michuano hii mikubwa barani Afrika, sasa ni wakati wa kukaa chini na kutafakari. Kejeli za 'Mtani jembe' hazitatufikisha popote, zaidi sana mwaka mwingine tena tutashuhudia team nyingine au ile ile ikikwama mahali pale pale kisha tutarudi na kejeli na mwaka mwingine tutashuhudia team ile ile au nyingine ikikwama mahali pale pale..and that will keep on circling. .
Kinachoisibu Yanga, Simba, Azam na wengineo ndio hicho hicho cha team ya taifa. Hakuna jipya. Hakuna mafanikio ya haraka haraka..tuwekeze kwenye accademy za kisasa kwanza. Fedha nyingi tunazotumia kupata makocha wa kigeni ziwekezwe kupata walimu bora wa hizo accademy. Bila hili na huu mfumo wa professional watatu tu wa kigeni ndio kabisaa tusahau kuvuka hata raundi ya kwanza...
Chekechea zinamsaidia mwanafunzi pale atakapoingia darasa la kwanza angalau anajua kuimba ..a, b, c, d... Elimu bora ya msingi inamsaidia mwalimu wa sekondari na mwanafunzi, hivyo itamsaidia profesa chuoni kumfundisha mwanafunzi huyo. Sasa iwapo mwanafunzi karuka ruka kote huko kisha umuweke chuo kikuu halafu unamfundisha Civil Engineering na apate first class..kweli!!???? Basi hivi ndivyo tufanyavyo kwenye soka.
.
Hebu lala kwanza. Ukiamka soma upya nilichokiandika.
hivi huwa unaelewa unachoandika au unaandika unachoelewa??
umesema kinachoisibu yanga,simba na azam zote hazina academy na mafnikio hayaji kwa haraka tuwekeze kwenye vipaji nimekwambia azam ina academy na nimekuonyesha picha za wachezaji wa under 14 waliofanikiwa kujiunga na azam fc chamanzi na nimekuonyesha picha zao still huelewi embu niambie nikusaidiaje uelewe kwamba aza wameanza kuwekeza kwenye soka la watototo
"Kinachoisibu Yanga, Simba, Azam na wengineo ndio hicho hicho cha team ya taifa. Hakuna jipya. Hakuna mafanikio ya haraka haraka..tuwekeze kwenye accademy za kisasa kwanza. Fedha nyingi tunazotumia kupata makocha wa kigeni ziwekezwe kupata walimu bora wa hizo accademy. Bila hili na huu mfumo wa professional watatu tu wa kigeni ndio kabisaa tusahau kuvuka hata raundi ya kwanza."
Kinafanana na unachodai nimesema? Unaelewa maana ya kuwekeza au? Nikusaidie kwa kukusonda swali lingine..tunaposema serikali iwekeze kwenye elimu ina maana serikali haina shule?
unaongea kitu kilekile katika maneno tofauti.karibia nitachoka kukuelimisha sasa maana naona huelewi,
klabu ndo zinapaswa kuwa na academy za watoto na wala sio timu ya taifa,umesikia wapi timu ya taifa ina academy,timu ya taifa inachagua wachezaji iwe wa academy au wakubwa kutoka katika klabu nyinu=gine zenye mfumo huo na hili swala TFF walisshalisema lifanyiwe kazi na klabu zote kwa maana kila klabu ya ligi kuu lazima iwe na academy sema utekelezaji wake ndo unasua sua so jaribu kuwa muelewa unapooleweshwa sio kila kitu lazima upinge hata unapoambiwa fact.
Nilijua nakurahisishia kumbe ndio nakupoteza. Basi ngoja nikupeleke kwenye mkondo ambao watu conservative wanataka.: Haya umeeleza point nzuri sana. Haya mawazo yako ndio yanatakiwa yawepo kwa viongozi wa soka. Big up sana mkuu.
unakataa kukubali fact unaleta porojo what i was trying to say hapo juu ni kwamba ulichosema sawa kuhusu kuendeleza klabu za academy,na azam washalionyesha hilo so klabu nyingine zinapaswa ziige mfano huo.(tumeshindwa kuelewana kwenye kitu kidogo tu)
Ok.....