M'mafia wa Tz
Member
- Oct 25, 2012
- 6
- 0
Nini mana ya kupiga kura kwa sisi wafrika?.....kaa tafakari utagundua mana ya kupiga kura kwa mwafrika ni kumpa ulaji ambao hajawahi kuufikira katika maisha yake kabla hajachaguliwa kua kiongozi(Kumpa tiketi ya kwenda kutatua matatizo yake binafsi na si ya nchi).Na ndio mana viongozi wengi wa jamii ya kiafrika wamekua wakiwadhalau sana wananchi wakisahau kua wapiga kura ndo walio wapa dhaman ya kuwaongoza na kosa lingine ni kwa mpiga kura kumruhusu kiongozi wake ajione yeye ni mtu na mpiga kura ni kitu.siasa nzuri ni pale mpiga kura anakua(si kwamba anapewa) mamlaka ya kumuondoa madarakani akishindwa kutumiza wajibu wake.kwa bahati mbaya sana sisi waafrika ni watu imara sana kulalamika lakini ni dhaifu sana kuwawajibisha viongozi kupitia vyombo walivyovichagua wenyewe kama mahakama n.k Hali hii imekua ikiwapa ujasusi viongozi na kujiona bora zaidi.
Nimeshangazwa na bunge la leo huko dodoma ambapo wana propose madaktari kutoka india waje kupima afya za wabunge.Nachojiuliza hii mamlaka wameitoa wapi ya kuafanya hivyo wakati mtanzania wa leo hata kumuona daktari wa hapahapa ni ishu na adimu na wanatuona mabwege kiasi gani mpaka wawe huru kupanga tu wanavyotaka?.Nikapata jibu kwamba dhana ya kumpa kura kiongozi ni sawa na kumpa tiketi ya kwenda kufanya matanuzi ana anasa za ajabu.
Tushirikiana wananchi wote kuindoa hii dhana.