Nimuoe nani?

Plato

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
420
94
Nashindwa kufanya maamuzi.nisaidieni mawazo.yanisaidie kufanya maamuzi. Nina wasichana 2,mmoja ni mchumba wangu,uchumba wetu una miaka 3 sasa,na tumetoa zaidi ya mahari.nilimpromisse kumuoa mwaka kesho akasema atanisubiri na amefanya hivyo.ninampenda sana.nadhani naye ananipenda.lakini upande mwingine rafiki yangu wa miaka mingi(msichana) mhitimu wa university ambaye aliachana na boyfriend wake na akakaa zaidi ya mwaka bila uhusiano.ikatokea tumezoeana sana ndg zake wengi wakanijua tukawa kama ndugu.mwaka jana nikiwa na mchumba tayari tukaanza kuwa na mahusiano ya mapenzi.akawa anaongea kuwa anaridhika nami hata nikimuoa kwani ananifahamu.sasa imetokea akapata mimba,na yeye kafurahi kwamba si nitamuoa.hajui habari za mchumba wa tangu kabla yake.mimba ina miezi 4 sasa.UTATA: Nimuoe nani kati yao,inaniwia vigumu kuvunja promisse kwa mchumba aliyenivumilia kwa miaka 3 sasa,wakati huohuo inaniwia vigumu kumtelekeza niliyempa mimba na kubadili maisha yake.pili nafikiri nn kitatokea kwa uamuzi wowote nitakaochukua.kwangu limekuwa zito,nishaurini.asante
 
Mshahara wa dhambi ni mauti. Unakiri kabisa huyo mshichana alikusubiri tena ukaanzisha uhusiano na mweingine, he kweli wanaume mna mambo duniani huyu lol huoni hata aibu kuzungumza hivyo. wewe tayari sio mwaminifu hupendezi hata kuoa mmoja wapo hufai
 
Nashindwa kufanya maamuzi.nisaidieni mawazo.yanisaidie kufanya maamuzi. Nina wasichana 2,mmoja ni mchumba wangu,uchumba wetu una miaka 3 sasa,na tumetoa zaidi ya mahari.nilimpromisse kumuoa mwaka kesho akasema atanisubiri na amefanya hivyo.ninampenda sana.nadhani naye ananipenda.lakini upande mwingine rafiki yangu wa miaka mingi(msichana) mhitimu wa university ambaye aliachana na boyfriend wake na akakaa zaidi ya mwaka bila uhusiano.ikatokea tumezoeana sana ndg zake wengi wakanijua tukawa kama ndugu.mwaka jana nikiwa na mchumba tayari tukaanza kuwa na mahusiano ya mapenzi.akawa anaongea kuwa anaridhika nami hata nikimuoa kwani ananifahamu.sasa imetokea akapata mimba,na yeye kafurahi kwamba si nitamuoa.hajui habari za mchumba wa tangu kabla yake.mimba ina miezi 4 sasa.UTATA: Nimuoe nani kati yao,inaniwia vigumu kuvunja promisse kwa mchumba aliyenivumilia kwa miaka 3 sasa,wakati huohuo inaniwia vigumu kumtelekeza niliyempa mimba na kubadili maisha yake.pili nafikiri nn kitatokea kwa uamuzi wowote nitakaochukua.kwangu limekuwa zito,nishaurini.asante

Kwa kweli ulichofanya ni kituko,ndio maana unaona waliochangia wote hawakuficha hasira zao kwako.
Kwa kweli umemsaliti mchumba wako aliyejitoa na kukusubiri kwa muda mrefu,ingawa umekiri kwetu hujasema lolote juu yake (naamini bado hajui) embu ona si hatari hiyo...lakini pia unamuweka mtoto wako mtarajiwa kwenye mazingira mabaya...nobody can tell you now nani umuoe.
Binafsi ninachoweza kusema kwanza take time uongee nao kila mtu kwa wakati wake ili kila mmoja ajue nini kinaendelea upande mwingine then ujue kila mmoja amelichukuliaje hilo suala na nini maamuzi yake from there unaweza kuwa kwenye nafasi ya kuamua.
Lakini lazima ukubali kwamba at last utamuumiza sana mmoja kati yao au wote,na lawama zote unapaswa kuzibeba wewe.
 
Wewe huna ustaarabu. Utawaharibia wote maisha yao. Kama ulifika kujitambulisha ukweni bado ukampa Mimba mwingine, hata yeye akae tayari ukiamua kumuoa, utaendelea kugawa mimba kwa wengine huko nje.
 
Yaani we jamaa hovyo sana hivi ukoje wewe??? Umeshatoa mahari bado unachakachua nje na mimba juu?? Wewe mwanaume mubaya sana SIJAFURAHI
 
tafuta dini inayoruhusu uoe wote uongeze na mwingine,

marytina unaonekana kukasirishwa kweli!
kiukweli jmaa hapa amebugi.hadi nashindwa kumshauri.
kikubwa chakufanya hapa ni kuangalia mapenzi yapo wapi? na kwa muibu wake anampenda sna mchumba wake.so oa huyohuyo.
 
Multiple choice;
a). Waoe wote kwa maana umejitakia kwa tamaa zako, na uwe tayari kumuongeza na mwingine....! Lakini ujue kuwa kila mwanaume akiwa na wanawake wawili, basi pembeni ana mume mwenzie.....!

b). Waache wote, na hivyo pia uwe tayari kuendelea na maisha ya ukapera daima huku ukiwa na laana zisizo na suluhisho hadi motoni.....!

c). Kaa kimya, kwa maana when the time is over, it will tell who you have to marry.....! Na kwa vyovyote uaminifu hautakuwepo kwenye ndoa hiyo daima maishani mwako....!

d). Yote hayo yakikushinda basi jiue aidha kwa sumu au kwa kamba, ili wote wakukose na uzikwe ukiwa na amani kama ndio kusudio lako....!
 
unatakiwa kuwathamini wanawake na kuwatreat vizuri na sio kama ulivyofanya ndio maana watu wanakushukia kama hivi.
wa kumuoa hapo ni yule ulietoa mahari kwao na amekusubiri miaka yote hii.
watu hawaoi mimba au kwa huruma ila unaoa mke kaka.
nawasilisha
 
Kaka, inaonekana kwako msamiati kinga ulikukwepa kabisa. Unakula kavu, ulipima na huyo uliyempa mimba? Unacheza makida kwa mamba mwenye njaa kaka. Naungana na wengine mzigo wako huo, kumbuka maamuzi yoyote utayochukua ni kilio kwa hao wasichana. Hukuthamini utu wao wala utu wako. Tubu, fanya toba ya kweli, muombe Mungu kwa Imani yako akusamehe.
 
Multiple choice;
a). Waoe wote kwa maana umejitakia kwa tamaa zako, na uwe tayari kumuongeza na mwingine....! Lakini ujue kuwa kila mwanaume akiwa na wanawake wawili, basi pembeni ana mume mwenzie.....!

b). Waache wote, na hivyo pia uwe tayari kuendelea na maisha ya ukapera daima huku ukiwa na laana zisizo na suluhisho hadi motoni.....!

c). Kaa kimya, kwa maana when the time is over, it will tell who you have to marry.....! Na kwa vyovyote uaminifu hautakuwepo kwenye ndoa hiyo daima maishani mwako....!

d). Yote hayo yakikushinda basi jiue aidha kwa sumu au kwa kamba, ili wote wakukose na uzikwe ukiwa na amani kama ndio kusudio lako....!

Konakali,
Hapo kwenye bold ndugu yangu umefika mbali. Hakuna dhambi isiyosamehewa mbele za Mungu, akijiua ni tiketi moja kwa moja jehanamu. Ningekuwa mimi ningetubu kwanza kwa Mungu kwa madhambi hayo kisha niombe uongozi wake ndipo nijue nini nifanye.
 
Multiple choice;
a). Waoe wote kwa maana umejitakia kwa tamaa zako, na uwe tayari kumuongeza na mwingine....! Lakini ujue kuwa kila mwanaume akiwa na wanawake wawili, basi pembeni ana mume mwenzie.....!

b). Waache wote, na hivyo pia uwe tayari kuendelea na maisha ya ukapera daima huku ukiwa na laana zisizo na suluhisho hadi motoni.....!

c). Kaa kimya, kwa maana when the time is over, it will tell who you have to marry.....! Na kwa vyovyote uaminifu hautakuwepo kwenye ndoa hiyo daima maishani mwako....!

d). Yote hayo yakikushinda basi jiue aidha kwa sumu au kwa kamba, ili wote wakukose na uzikwe ukiwa na amani kama ndio kusudio lako....!

Nimeipenda hiyo D ndio suluhisho lake
 
Pole sana kwa kujiingiza kwenye shimo na kushindwa kujitoa.
oa aliyekuwa anakusubiri kwa muda wote na tayari umeshamtolea mahari na umekiri kwa kinywa chako unampenda sana.
pia mweleze mapema yote yaliyotokea na umwombe msamaha na kwa upande wa dada mwenye mimba ongea nae kumweleza unamchumba na utalea mtoto lakini hakuta kuwa na mawasiliano zaidi ya hapo.
 
Oa mchumba alafu akijakugundua umezaa na mwanamke mwingine kipindi cha uchumba wenu alete varangati...au hata kutaka muachane!!Au oa mjamzito nae akijagundua alikua kiburudisho tu wakati yeye alidhani ndo kila kitu nae aanzishe varangati lake...uwezekano wa yeye nae kutaka muachane upo!!Sugua kichwa...ulivyokua unawachanganya ulidhani ni sifa ehh?Mijanaume mingine bwana!
 
Oa MCHUMBA aliyekusubiria Ila JUA ya kuwa hata huyo utakaemuoa akijua una mtoto nje ya ndoa, itakuwa balaa... Hivyo nakushauri mweleze UPUUZI wako wote ulioufanya kwa huyo aliyekuwa na Boi frendi akaachana nae, wewe ukachukua.
 
:lol::lol::lol: ndo ukome..wakati unafanya uliyoyafanya mbona hukuja JF kutuarifu??
 
Oa mchumba alafu akijakugundua umezaa na mwanamke mwingine kipindi cha uchumba wenu alete varangati...au hata kutaka muachane!!Au oa mjamzito nae akijagundua alikua kiburudisho tu wakati yeye alidhani ndo kila kitu nae aanzishe varangati lake...uwezekano wa yeye nae kutaka muachane upo!!Sugua kichwa...ulivyokua unawachanganya ulidhani ni sifa ehh?Mijanaume mingine bwana!

Taratibu Lizzy Jamani!! Give him a brake.
 
Back
Top Bottom