Nimueleweje na nifanyaje?

Samahani kwa kukushutumu , nisamehe sana.

Usijali...

Sasa nifanyaje kama keshaniacha? Si aniambie basi ili nielewe .

Endelea na maisha yako na taratibu nawe anza kumtoa moyoni...kama utakuwa na nguvu basi waweza mueleza wazi kuwa mapenzi yenu yafike ukomo.

Hapa ndio huwa nashangaa sana kuhusu sisi binadamu yaani hata sijui tukoje ...

Usishangae bali shukuru kuwa umeitambua hii hali mapema...kuna namna nyingi za kuachana na hii ni njia mojawapo itumikayo haswa unapoona yule uliyenaye hana thamani na bado anaendelea kufanya ghasia!!!
 
Jina langu hilo hapo juu!

Wala usihofu, huo muda wa kuchezea maisha ya watu, badala ya kuyahangaikia yangu yasikimbie, nautoa wapi!

Hapo sasa shukurani.
 

Asante sana kwa ushauri . Nashukuru.
 
Jamani Asanteni kwa ushauri we nu kwa Kweli Mungu awabariki sana. Kama hujato ushauri please feel free wapendwa . Asanteni sana Nawapendeni wote . Barikiwa wote .
 

Hata mtu aweje mkarimu kama hajali hisia zako huyo mtu siyo mkarimu, kumbuka you are responsible for your happiness don't allow anyone to control how you feel, a relationship is to complement you and not fulfill you.

Tatizo kubwa la baadhi ya wanawake ni kuzani kuwa wanamajibu ya wanaume, unawasiwasi na hali yake then what?
Unataka uambiwe nini hapo? Wakati kila kitu kinasomeka clear...Na baadhi ya wanawake wanaamini sana masikio yao kuliko utashi wao. Kwanini ufikirie wewe ndio umemkosea na sio yeye? Hapo utakuta unahangaika kumpigia simu hata kwenu haupigagi kihivyo unamaliza hela kwa sms ambazo ungekuwa unasms wengine wanaokujali hata familia yako. Acha hizo stress za kujitafutia.

NB: Umeshauriwa hapo juu achana na huyo mtu, fanya yako, wengine wakibembelezwa sana ndio wanaharibu zaidi ila ukimpotezea atajua kuwa you know your value, kama wako atarudi tu kama sio hata ukisms na kuemail utatangwa maji kwenye kinu. Relax the best is ahead of you.
 

Asante mpendwa! Good lesson.
 
Pole! Ukiona hivyo huyo mtu ana mpenz wake! na ww ni mchepuko!
 
Pole! Ukiona hivyo huyo mtu ana mpenz wake! na ww ni mchepuko!

Asante . kama ni Kweli hayo uyasemayo, Basi Mungu atamlipa kwa Yale aliyoyapanda. Nashukuru Mungu hatujawahi kufanya tendo lolote la ndoa nilimuambia mpaka ndoa na akakubali hivyo .
 

we bibie vp? Inamaaa kama kusoma hujui hata picha huoni?!
Soma alama za nyakati. Kijana mpole mcha Mungu na mcheshi ameshaingia mitin
 
Miwanaume ndo ilivyo hapo ushakosea sana,inavyoonekana kwake umekufa,hawa watu haitakiwagi wajue kama unampenda sass hayo ndo malipo yake! Kifupi hiyo ndo style alotumia kukuachaa kubali matokeo Fanya kama amekufa HV tuone itakuwaje
 
Ndugu yangu hata mimi yalinipata kama yako kwa kifupi huyo kaka amekuacha,ila inauma sana sana sana ni bora anaekwambia kuliko anaekuacha kimya kimya ni ukatili sana,presha zilinisumbua sana niliugua ila namshukuru mungu sasa nimekaa vizuri ,nakuombea Mungu akujalie upate mwengine atakaeziba pengo najua utapata shida sana mapenzi yanauma, ila utasahau.
 
Ama kweli wewe ni mkweli maana umeongea ukweli mtupu,uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
 
Dada pole sana, huyo mtu ivoonekana ana mke. Pengine haishi nae au mchumba ambae wako mbali. Kama unavojua, likizo ni muda wa kutulia na familia au na mtu unaempenda.

Kwahiyo ili kuepusha mengi na kupata ulcers bure, jiongeze tu.

Kuprove hilo kama anamtu, likizo ikiisha atakuja na sababu kibao utashangaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…