CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,065
Ni miaka mingi sana nchi yetu haijafanikiwa kutatua moja kwa moja uhaba wa walimu nchini, zaidi walimu wapya wameendelea kuajiriwa kila mwaka na idadi wa walimu tarajali imeongezeka siku hadi siku... wengi wamejiuliza je ni kweli walimu hawatoshi? hao wanaoajiriwa kila mwaka wanaenda wapi? SASA NATUMBUA JIPU
ukweli ni kwamba upangaji wa walimu katika shule umetawaliwa na uhuni mkubwa, walimu wanapangwa shule kwa kujuana, utakuta wilaya moja kuna shule (hususani zile za mjini au karibu na barabara) zina walimu wa kutosha (wakike wakiwa wengi) huku shule nyingine zikiwa na walimu wachache (na nyingine hazina mwalimu hata mmoja wa kike) nitaandika siku nyingine kwanini walimu wa kike wengi wanapangwa karibu na halmashauri lakini kwa leo hebu niendelee kupasua hili jipu....
sasa wakati ajira za walimu zikitangazwa walimu wanapokuja kuripoti wanakuja na "vimemo" tayari wanapangwa shule za town na vijijini wanapangwa wale wanyonge... hivyo kama jipu hili lilisipotumbuliwa ipasavyo shule nyingi zitaendelea kuwa na walimu wachache daima na milele.......
jipu nimelipasua najua kuna walioumia lakini hebu tumsaidie raisi wetu haya majipu...
kwa yule ambaye anabisha afanye utafiti wake wakati wa ajira mpya za walimu 2016