Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,471
- 33,012
NIMKUMBUKAVYO BI. SHARMILA (1942 - 2025)
Siku mbili tatu zilizopita kuliwekwa katika mitandao makala ya marehemu Shakila mwandishi akieleza historia yake.
Pamoja na makala ile kulikuwa na picha mbili ya Shakila na ya Sharmila.
Kwa bahati mbaya mwandishi wa makala akaandika kuwa picha zote hizo mbili ni za Shakila ilhali moja ya mwanamke aliyevaa baibui tena la ukaya ni Bi. Sharmila.
Nilifahamiana na Bi. Sharmila ndani ya Bandari ya Tanga jirani na ofisi ya Port Engineer, Abdallah Mwinyi.
Jirani na ofisi ya Port Engineer marehemu Bi. Sharmila alikuwa akiendesha biashara yake ya chakula.
Mara nyingi nilikuwa nikipita na kumuona pale nikienda kumuona Port Engineer lakini sikupata kuzungumza na yeye wala sikujua kama huyu ni Sharmila muimbaji maarufu katika miaka ya 1970.
Ikasadifu siku moja nikakutana na Mhandisi Abdallah Mwinyi pembeni Kibanda cha Bi. Sharmila na Abdallah akanifahamisha kwake.
Ikawa sasa kila nipitapo pale nitasimama kumtolea salamu.
Siku moja nilipopita akaniambia, "Bwana karibia usifanye haraka nimekuletea mchumba."
Akanijulisha kwa bint mdogo kiasi miaka 10 hivi.
Bi. Sharmila akanijulisha kuwa ni mjukuu wake shule zimefungwa kaja kumsaidia kazi katika biashara yake.
Nikamsifia bint kwa uzuri wake nikamwambia basi mie nataka awe mchumba wangu.
Bi. Sharmila akawa anacheka mjukuu wake akinyanyua mabega yake juu ishara ya kuniambia hanitaki.
Lakini kila nikipita pale na kumtazama Bi. Sharmila moyo wangu ukisononeka jinsi muziki nchini kwetu usivyowanufaisha wasanii.
Nikifikiria santuri zake zilizokuwa kwa miaka na show alizofanya nk. nk.
Mara ya mwisho kabla sijaondoka Tanga nilikutana na Bi. Sharmila kwenye soko maarufu Tanga likijulikana kama "Soko la Wazungu."
Ilikuwa asubuhi na Bi. Sharmila alikuwa amekwenda kununua vitu kwa ajili ya biashara yake ya chakula.
Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi.
Amin.