Nimjuavyo Paulo Makonda: CHADEMA take care

Nimjuavyo Paulo Makonda: CHADEMA take care

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
2,994
Reaction score
1,770
Salaam WanaJamvi,

Kuna thread humu JF inayomhusu Paul Makonda mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM.

Huyu Bwana ni Msomi wa Chuo Kikuu, sina uwezo wa kujua alikuwa nasomea digrii gani pale Ushirika lakini alikuwa kiongozi wa Vijana pale MUccobs.

Aliwahi kuandaa kongamano kubwa la vijana kwa kulipa sura ya siku ya UVCCM na pia Kumuenzi Mwalimu Nyerere pale kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi. Ilikuwa ni Mwaka 2009. Mimi nikiwa ni miongoni mwa Vijana wa UVCCM Kipindi hicho.

Kwenye Kongamano hilo walikuwepo watu wafuatao;
  • Nape Nnauye
  • Reginald Mengi
  • Amos Makala (ambaye alikuwa mgeni rasmi)
  • Engineer Sytella Manyanya
  • Harison Mwakyembe
Wengine walioalikwa walikuwa ambao hawakuhudhuria ni Anne Kilango, Samwel Sita, na Christopher Olesendeka.

Nadhani waheshimiwa wote hao mnawafahamu na mirengo yao. Pia kwa fikra za karibu, labda ukimuondoa Mzee Mengi hao wote ni wazee wa CCJ.

Kuonyesha kuwa huyu bwana ana mapenzi makubwa na fedh, alipewa fedha za maandalizi kiasi cha tsh 7m na Makala, 5m na mzee Mengi na Tsh 4 na Mzee Ndesamburo. Sisi kama UVCCM kipindi hicho tukijisafirisha wenyewe kutoka kwenye wilaya zetu.

Wakati mkutano unaendelea, baada ya wageni waalikwa kujitambulisha akiwemo Nape, Mengi, engineer, Harrison, tulisikia mngurumo mkali wa chopa.

Kwa wanaoijua Jiografia ya Moshi, Chuo cha Ushrika kipo juu mlimani kidogo, hivyo unaliona bonde la Kiborloni kwa chini vizuri mahali ambapo ndipo mitaa ilipo hotel ya Keys.

Baada ya Mgeni Rasmi kuanza kuhutubia vijana, huku Makonda mwenyewe akiwa bize na simu yake, Chopa lile lilikuja likatua uwanjani kwa mbwembwe likiwa limemleta Mzee Ndesamburo. Tukio ambalo lilikatisha Hotuba ya Amos Makala.

Baada tu ya kutua, Mzee Ndesa akapanda jukwaani akiwashambulia vilivyo wakina Makala.

Baada ya tukio hilo, ndilo lililofungua jina la Makonda kwenye media za hapa nchini na kujikuta ni miongoni wa mastaa hapa TZ. Tukio ambalo lilichoma TZS 6m, pesa za UVCCM mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kwenda Dar kwenye media kumkanusha Makonda kuwa sio kiongozi wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro.

Sasa huyo ndio Paulo Makonda, bingwa wa kuchonganisha watu na Mjasiriamali wa kisiasa. CDM mna hiyari ya kumchukua na kumfanya maarufu zaidi.
 
Mbona mnatahadharisha sana CDM hawezi kwenda NCCR ama CUF? Kwani CDM wanapotoa kadi huwa wanakipimo cha kudetect dhambi za mtu?

Tuwaache wanasiasa wafanye siasa!
 
Uwongo mwingine bwana!

Chopa ya Ndessa Bin CHADEMA kwenye mkutano wa UVCCM wapi na wapi??

Hebu thibitisha zaidi kwa vielelezo hususani picha za tukio. Vinginevyo hii ni pumba.
 
Ni tukio la mwaka 2009, sijui kuwa hata simu nilikuwa nayo mda huo ninayo mpaka sasa. Lakini Makonda ni member humu aje akanushe, nape pia ni memba humu aje anikanushe . ila kongamano hilo lilikuwa ni mtego ili jamaa atengeneze fedha zake
 
Mbona unaleta hilo swala leo baada ya kutofautiana? Cursorily looking at your thread, inaonekana ni hofu ile ile tu inayowaandama ccm dhidi ya chadema. Inavyoonekana Makonda ni mahiri sana huko ccm na mnayafahamu makeke yake, sasa mnajua fika kuwa akitua chadema mambo yatakuwa hatari. Nikutoe wasiwasi, Chadema hakiogopi mtu na hakina tabia hiyo. Kamamakonda anataka kuja mwache aje afanye siasa kwa uhuru lakini akijua kuna mipaka yake si kama huko CCM.

Na asifikiri eti akija huku atakabidhiwa cheo kama huko ccm tunavyojua kuwa mwenyekiti anahaha kumtafutia shonza nafasi ya ukuu wa wilaya ilimradi tu kuwaonyesha vijana walioko upinzani kuwa ukiingia ccm mambo yanyooka bila kujua kuwa huko ni kukiua chama.

Makonda njoo jiunge na makamanda! Chadema wanajua kudhibiti watu wa tabia unayojaribu kumsingizia Makonda. Tusubiri Nape naye aseme ni Makonda ni oil chafu!! CCM bwana! Muda utaamua......
 
Chadema ni chama makini kila mtu anakiri hata hao wazee wa ccm,mmemsikia, Kingunge akitoa yake jana. Huyo aje na kama atakuwa mnafiki Chadema watamjua mapema sana na kujua cha kufanya. Makeke ya Shibuda yako wapi? chezea CDM wewe!
 
Mbona unaleta hilo swala leo baada ya kutofautiana? Cursorily looking at your thread, inaonekana ni hofu ile ile tu inayowaandama ccm dhidi ya chadema. Inavyoonekana Makonda ni mahiri sana huko ccm na mnayafahamu makeke yake, sasa mnajua fika kuwa akitua chadema mambo yatakuwa hatari. Nikutoe wasiwasi, chadema hakiogopi mtu na hakina tabia hiyo. Kamamakonda anataka kuja mwache aje afanye siasa kwa uhuru lakini akijua kuna mipaka yake si kama huko ccm. Na asifikiri eti akija huku atakabidhiwa cheo kama huko ccm tunavyojua kuwa mwenyekiti anahaha kumtafutia shonza nafasi ya ukuu wa wilaya ilimradi tu kuwaonyesha vijana walioko upinzani kuwa ukiingia ccm mambo yanyooka bila kujua kuwa huko ni kukiua chama. Makonda njoo jiunge na makamanda! Chadema wanajua kudhibiti watu wa tabia unayojaribu kumsingizia Makonda. Tusubiri Nape naye aseme ni Makonda ni oil chafu!! CCM bwana! Muda utaamua...

MKUU MIMI sio CCM kama unavyojaribu kuniona. Namuoelezea makonda hivyo kwa sababu nanfahamu, kuna watu wanateseka, Moshi kwa ajili ya kongamano lile (mtu anayeweza kukueleza Ubaya wa Makonda ni Amrani Kesi aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Mjini).

Ni kweli Makonda ni mjenga hoja mzuri na ana ushawishi ingawa wenzake MUccobs wanamwona kama tapeli wa kisiasa. Hofu yangu asije akaingia CDM akatu keep busy kumchnguza huku tunaacha M4C.

Ili M4C i move tupende tucipende nguvu ya vijana ni Muhimu. ndo maana mpaka sasa wanaoeneza M4C ni vijana kama kina lema, mawazo, bananga na wengine wengi. Huyu kwa sababu tayari ni maarufu automaticaly chama kitamuweka humo ajichanganye na wenzake kina Bananga.

Labda nikuulize swali moja tu Bananga ana madaraka gani huko CDM. na ana muda gani tangu atoke CCM. Hivi kama bananga akaamua kuifanyia kazi CCM wakati huu M4C inasambaa atashindwa nini?

Tusijidanganye kuwa eti mtu maarufu kutoka chama kingine anapojiunga na chama kipya anarudi kuanza chini.

Wanafanya hivyo ili waweze kuendelea kuwa juu. Wawe wanakutana na makamera ya waandishi wa habari.
 
Nini kilichomfukuzisha CCM huyu kijana ?

Paul Makonda ni kada wa damu ya kijani, kama mjuavyo makada wa damu ya kijani huwezi kuwatenganisha na ujasiriamali wa kifisadi .So kama alipiga fedha kwa kongamano ni jadi yao .
Paul ndio alikuwa Katibu wa CCJ (nipo tayari kurekebishwa kama cheo sio hicho ,but alikuwa frontliner na Mpendazoe ).
Paul alidisco MUCCoBS yakafanywa mazingaumbwe akarudia Mwaka wa kwanza coz nyingine ya B.A in Community Economic Development mwanzo alikuwa anasoma B.A CMA .Ila niliona kwenye page yake ya Fb kama alienda kusoma UDOM (wenye data watazishusha ).

KIFUPI PAUL NI MJASIRIAMALI MWENYE HIBA YA DAMU YA KIJANI
 
kuna chanzo changu cha habari nafuatilia kwa karibu kubaini nafasi yake,kuthibitisha kuwa naye ni mtumwa wa magogoni-TISS/UWT ni vema pia CHADEMA kuwa na angalizo na watu kama hao maana kwa sarakasi ndio wenyewe, mnafikri jamaa yupo vile na stress kibao kumbe yupo kikazi kweli kweli.
 
Nini kilichomfukuzisha CCM huyu kijana ?

Paul Makonda ni kada wa damu ya kijani, kama mjuavyo makada wa damu ya kijani huwezi kuwatenganisha na ujasiriamali wa kifisadi .So kama alipiga fedha kwa kongamano ni jadi yao .
Paul ndio alikuwa Katibu wa CCJ (nipo tayari kurekebishwa kama cheo sio hicho ,but alikuwa frontliner na Mpendazoe ).
Paul alidisco MUCCoBS yakafanywa mazingaumbwe akarudia Mwaka wa kwanza coz nyingine ya B.A in Community Economic Development mwanzo alikuwa anasoma B.A CMA .Ila niliona kwenye page yake ya Fb kama alienda kusoma UDOM (wenye data watazishusha ).

KIFUPI PAUL NI MJASIRIAMALI MWENYE HIBA YA DAMU YA KIJANI
KAKA Paulo Makonda amesoma MUCCoBS,KOZI YA B.A.CED(Community Economic Development) Alimaliza mwaka jana,Ni member wa MUCCoBS na Ni msomi toka MUCCoBS,Msimchafue huyu ARIFU!
 
Back
Top Bottom