Nimfanye Nini Fisadi Huyu?

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
706
Waheshimiwa,

Mimi ni mwana JF wa siku nyingi, ila kwa leo najitokeza kwenu kwa jina langu halisi. Kuna sababu ambayo inanifanya niwe muwazi na mkweli kabisa. Ni mimi mwenyewe, wala si mtu mwingine yeyote.

Niandikavyo hii post niko nyumbani, Moshi, nikitokea Arusha, ambapo nilienda juzi kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Nane wa Leon H. Sullivan. Jina hilo, kinyume na firka na mazoea ya Watanzania wengi, linatamkwa "Salivan" kama "Samit", yaani, "Sullivan", ikiwa sawa na "Summit". Cha ajabu ni kwamba Watanzania wanatamka ipasavyo neno "Summit", lakini inapokuwa kwa "Sullivan" wanatamka "Sallivan", ambalo ni makosa.

Nimejitokeza leo kwenu kuwauliza, kuna mtu ambaye kwa mtazamo wangu ni fisadi (sio tu fisadi, ila ni dhulumati). Ni mtu ambaye wote humu ndani mnamfahamu na kumheshimu, kwa hiyo naomba kuuliza: Nimlete humu ndani tumjadili, au nimsamehe nimwachie Mungu, anilipe haki yangu? Nitazingatia ushauri wenu.

Asanteni.

./aziz mongi
 
Back
Top Bottom