Huyu Bamedi leo kanikomesha aise.
Nilikuwa kaunta napata Moja baridi Moja uvuguvugu, ghafla akatokea mwamba, yule mwamba kwa sauti ya majivuno na yamajigambo si akamwambia yule Bamedi:
We Changu mbele si akamalizia na Doa, chukua bia kumi unywe uku akitoa wallet na kulipia ule mkojo wa Filauni.
Alivotoka yule mwamba kama hatua 3 hivi, si nikamfata yule bamedi nikamkonyeza akaja, nikamwambia:, kumbe wewe inakulipa sana eti? Yani huyu Popoma kakupombekesha muda mchache hivi!?
Unataka kujua tusi aliloniachia huyu Bamedi!?
Alinambia: kama vipi mpelekee ulambe Bingo na wewe.
Dah! Nilitamani nimrukie aise.