Nimeshindwa kumuelewa mke wangu, yaani ni kosa kutokutwa na meseji za kucheat?

Wanawake wakati mwingine hata hujui wanatafuta nini maana inakuwa kama anatafuta sababu akushushe lawama ili aondoke maana hata hujui. Mume anakuheshimu, haongei na hiyo michepuko mbele yako wala hajakupunguzia kitu unataka nini kuchokonoa mambo kwenye simu. akikuacha? kesho unarudi tena kwake hapo hapo hata power huna tena. siri hii kwa wanawake nawapa, mwanamme hapendi kufuatiliwa sana wala gubu hata kama unahisi anamchepuko potezea kuwa kawaida tu na kuhakikishia mume hata kuacha kamwe atazunguka huko kwako hata ondoka lakini ukianza gubu tu mume ataichukia nyumba na ataanza kuona nje kuzuri sababu sipati gubu maana mchepuko anajuwa jamaa ana mke hakuna jipya wala sileti vineno wewe mume akirudi home kelele tu basi ujuwe unachimba kaburi hata kama alikuwa anakupenda ataanza kuwaza tofauti.
Mume wako amepata mke hasa. Kama una rafiki au mdogo wako mwelewa kama wewe plz tuwasiliane.
 
We utakuwa mzee wa Mark all=>Delete all
Sasa shemeji anakosa pa kuuliza huyu nani.
Uwe unaacha hata za promosheni na za matapeli ili atolee povu humo
 
Simu yangu kipindi cha nyuma nilikuwa siweki password. Mpaka siku moja nilipoibiwa halafu mwizi akaanza kuomba zitumwe pesa kwenye namba fulani akitumia simu yangu.

Hapo nikaona niwe naweka password. But pia kwa sasa hizi simu ni kama laptop. Tunahifadhia docs muhimu n.k. so naweka na pia password nampa aifahamu siyo kesi.

Nmeenda oga kumbe yeye kaamua kufanya ujasusi kwenye simu yangu nmerudi namkuta amenuna.sikuelewa sababu.but nikaona mwendelezo wa kununa na hasira ni mkubwa ndo kumuuliza nini kisa.

Ananambia najifanya mjanja na delete msg za mapenzi kwenye simu. Haiwezekani akose msg hata moja ha kuonesha nina mchepuko. Mimi mhuni nliye na uzoefu sana kiasi kwamba siachi alama. Amekagua simu nzima hajakuta text toka kwa mchepuko.

Yaani amekasirika kutokuta kuna ushahidi kuwa nachepuka akaenda mbali kusema ndio maana najifanya kumpa password sababu kila kitu kipo well organized. Nimewaambia michepuko mida fulani wasipige wala kutuma text.

Anasema ni bora mke wa rafiki yake alikuta msg za mchepuko kwenye simu ya mumewe. Ila mimi hata alama siachi jinsi nlivyo mzoefu.

Nimeshangaa sana. Yaani ni kosa kutokutwa na msg za kucheat? Hawa wanawake ni ngumu kuwaelewa kabisa. Ovess.
Anataka ugomvi wa kulazimisha huyo!
Sasa ebu fanya mpango aikute halafu tuone atafanyaje...🤐😎
 
Hahahaha...
Nimecheka sana... Embu weka picha ya huyo mwanamke tuone anafananaje....

Shunie njoo usome hii... ati kwa nini simu inakaa mbali na binadamu...
 
Hata mie nimewahi ulizwa mbona sikuti sms za wanawake kwenye simu yako?utakuwa unani cheat kwa siri sn ww.Akazua ugomvi,wakati mimi sina mwingine zaidi yake na nimeridhika na vitu anavyonipa vyote.Hawa watuuu!
 
Simu yangu kipindi cha nyuma nilikuwa siweki password. Mpaka siku moja nilipoibiwa halafu mwizi akaanza kuomba zitumwe pesa kwenye namba fulani akitumia simu yangu.

Hapo nikaona niwe naweka password. But pia kwa sasa hizi simu ni kama laptop. Tunahifadhia docs muhimu n.k. so naweka na pia password nampa aifahamu siyo kesi.

Nmeenda oga kumbe yeye kaamua kufanya ujasusi kwenye simu yangu nmerudi namkuta amenuna.sikuelewa sababu.but nikaona mwendelezo wa kununa na hasira ni mkubwa ndo kumuuliza nini kisa.

Ananambia najifanya mjanja na delete msg za mapenzi kwenye simu. Haiwezekani akose msg hata moja ha kuonesha nina mchepuko. Mimi mhuni nliye na uzoefu sana kiasi kwamba siachi alama. Amekagua simu nzima hajakuta text toka kwa mchepuko.

Yaani amekasirika kutokuta kuna ushahidi kuwa nachepuka akaenda mbali kusema ndio maana najifanya kumpa password sababu kila kitu kipo well organized. Nimewaambia michepuko mida fulani wasipige wala kutuma text.

Anasema ni bora mke wa rafiki yake alikuta msg za mchepuko kwenye simu ya mumewe. Ila mimi hata alama siachi jinsi nlivyo mzoefu.

Nimeshangaa sana. Yaani ni kosa kutokutwa na msg za kucheat? Hawa wanawake ni ngumu kuwaelewa kabisa. Ovess.

Jasusi kakutana na CIA
 
Na ndio mbinu iliyodumisha ndoa za wazee wetu mpaka wamezeeka pamoja. Mzee hata kama katoka safari, haendi home direct! Ataweka kituo sehemu, then anampa mkoba au koti kijana atangulize nyumbani. Then baadae yeye ndio anakuja.

Sasa sisi wa siku hizi ni kuwindana kama ngedere mara unapekua simu, mara unarudi nyumbani ghafla, ukisafiri unasema narudi jumanne halafu unarudi jumatatu ghafla... kuna watu mpaka wamefunga cctv kwa siri nyumbani. Mwisho unachokitafuta unakipata kweli halafu unaanza kulia lia
Wasiojiamini wanahangaika sana kwenye ndoa.
 
Hii ya mzee kutoka safari anafikia kijiweni anampa koti na mikoba kijana apeleke home yeye anakuja bakadae umenikmbusha mbali sana.

Hivi hawa wazee walikuwa hawawamisi wake zao?
 
Ukiona hivyo ujue Mkeo anaye mchepo wake na anampenda sana sasa anajistukia kwanini wewe huna ili ngoma iwe droo!! Wanawake wana akili sana.

Hata mi naona yaani.! Anatafuta equalizer ili mtoke sare sare..! Wanawake sio wajinga na wapuuzi kama unavyohisi. They’re very smart mimi huwa sichukulii masiala sentensi yoyote akitokea ametamka. Ni Nyoka
 
Back
Top Bottom