Nimeshapata mchumba

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298

1)Mapenzi ni kuyaenzi,upate ane kupenda
awe ndio wako mwenzi asoweza kukutenda,
Mwili ulintia ganzi,ukamua mbali kwenda
Usinisumbue tena,nimeshapata mchumba.




2)Mwana huyo ni mzuri,***** amemfunda
Mtoto hana kiburi,na siwezi kumtenda
Kwake mimi ni jasiri,nishaapa kumlinda
Usinisumbue tena,nimeshapata mchumba


3)Anayajua mapishi,hata yale ya mlenda
Siyo wewe ni mbishi,mchana kutwa waranda
Kwenu huwafurahishi,tabia imekuganda
Usinisumbue tena,nimeshapata mchumba.


4)Ulivunja yangu posa,vipi waniganda ganda
Ukamua kunitosa,na kwenu ukaniponda
Eti kisa sina pesa,nasimiliki kibanda
Usinisumbue tena,nimeshapata mchumba.



5)Wewe mwanamke gani,kwa umbea unakonda
Nani akuweke ndani,ulisutwa toka Bunda
Ulinumiza moyoni,na kunitia kidonda
Usinisumbue tena,nimeshapata mchumba.



6)Hujui choma mandazi,hata kupika bumunda
Naogopa fumanizi,mchumba atanidunda
Yetu ndoa huu mwezi,tena tarehe ya kenda
Usinisumbue tena,nimeshapata mchumba.





SHAIRI -NIMESHAPATA MCHUMBA
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
 
asikusumbue tena, umeshapata mchumba
ameikosa bahati, ilipangwa na muumba
kuwa nawe maishani, kwa hiyari si kuomba
muache apumzike, umpende ulonaye.

kumponda ex wako, si jambo la kiungwana
mapenzi mlishindwana, haifai kuchambana
uishi maisha yako, hilo ndilo la maana
muache apumzike, umpende ulonaye.
 
Back
Top Bottom