Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,808
- 6,500
Dah ukiwa na tamaa mara moja wanakuliza hawa jamaa' lakini je hawa jamaa wanashirikiana na makampuni ya simu? Kwa sababu msg wameonitumia leo haina namba ila imeandikwa MOI sijaelewa ni kampuni au nini?
Sikiliza nafsi yako inakwambia nini. Maana naona kama unamzuka wa kushiri ili utapeliwe.
inaelekea una bahati ya kutapeliwa. Sasa ukitaka uwe salama jinyamazie kimya la ukitaka kubahatisha kutapeliwa basi wee fuata maelekezo yao.
Hawa jamaa huwa wananunua package ya contact za wateja wa simu kutoka kwa wanafanyakazi wa kampuni ya simu, benki ambao sio waaminifu kwa kuwalipa pesa kidogo tu.
Matapeli Wakituma ujumbe kama huo kwa wateja laki moja, hawawezi kukosa kati ya hao ambao wanataka utajiri wa haraka na kutoa details zao zaidi au kutoa pesa.
Hapo naweza kubaliana na wewe mkuu maana sijawahi kuona ujumbe kama huo kwenye simu ya bibi yangu naishi nae'na mimi ndio msomaji wa sms zake,ila kwangu ni kawaida kabisa kutumiwa hizo
Mwingereza ndio anaandika hivi?
MOI
YOUR MOBILE NUMBER HAS BEEN WON 1,000,000 POUNDS FROM BLACKBERRY UK,KINDLY CONTACT DR GEORGE IMMEDIATELY ON bbuklive@w.cn TO REDEEM
Kumbuka katika maisha nothing comes for free. This is principle, It's too good to be true.