Hayo mambo ni ya kupanga pamoja (mutually) ili kila upande uridhike. Suala la kupangiwa tu na mkeo linaonesha namna jinsia KE inavyotumika vibaya kunyanyasa ME hasa kwenye masuala ya unyumba.
Nakushauri, keti chini na mkeo hasa wakati mmetulia. Napendekeza iwe usiku wa manane. Kabla ya kwenda kulala mtaarifu mkeo kwamba una jambo ungependa kujadiliana nae,hivyo usiku utamwamsha muongee.
Kisha mweleze namna unavyompenda na kuithamini ndoa yenu na hivo kutokua tyr kuona inatiwa doa la kukosa uaminifu kwa suala dogo tu la unyumba. Mweleze kwa upendo kwamba pamoja na mambo mengine,umemuoa kwajili ya kutimiziana haja zenu ikiwemo unyumba. Hivyo mtu pekee mwenye dhamana hiyo ni yeye tu.
Mweleze pia kama dini ni mhimu kwa maisha yenu wote, lkn mhimu zaidi ni ndoa yenu. Na tendo la ndoa ni mojawapo ya ibada takatifu. Hivyo mungu anaemwadubu hatosikia dua zake ikiwa hakutendei wewe haki.
Kwa hayo machache, naamini atakuelewa.!!!