Nimepata chama cha kujiunga nacho

Nimepata chama cha kujiunga nacho

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Tangu kuzaliwa kwangu,zaidi ya miaka 30 iliyopita, sijawahi kuwa na chama cha siasa. Ingawa nimekuwa mfuatiliaji wa siasa tangu shuleni na chuoni,sijawahi kuwa na kadi ya chama chochote cha kisiasa. Sababu ni moja:sikuwa nimejiandaa kuwa katika harakati za kisiasa. Lakini sasa ni tofauti.Natamani kuwa na chama na kuwa mwanasiasa.

Ndiyo maana nilijipa muda wa kusoma Katiba,Kanuni,Ilani na Sera za vyama mbalimbali hapa nchini ili nichague chama cha kujiunga nacho. Kwa weledi wangu wa sheria,nimesoma kwa makini na kuelewa ipasavyo. Pia,nimehudhuria mikutano ya vyama tofauti hapa nchini ili kusikia kauli na hotuba zao. Kuna chama kimenivutia.

Hicho chama kina Katiba nzuri;Kanuni zilizo wazi;Ilani inayolenga mema kwa watanzania; na wanachama wanaokipenda chama chao bila kificho. Ni chama kinachoamua kikaamua;kusema kikasema;na kupanga kikapanga.Kimenivutia sana. Nami najiandaa,hata kama hakutakuwa na viongozi wa kitaifa na vyombo vya habari,kujiunga nacho.

Nikishajiunga, weledi wangu wa sheria nitautumia kukiimarisha chama na kukitangaza. Kukifanya chama kiimarike zaidi na kuaminiwa.Chama nitakiheshimu na kukilinda-chama na wanachama wake. Nitaanza na heshima na kumaliza na shukrani. Najua nitaaminika. Kama uongozi hata mimi nimewahi kushika shuleni,chuoni na Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo(Law School of Tanzania).Uongozi una miiko yake,mipaka yake na taratibu zake kuupata. Nikiutaka,nitazingatia hayo kwanza.

Kiukweli kabisa, chama hiki nakiona kama chama chenye dira na makini.Kinalenga watu wa aina na madaraja yote. Ni mdomo wa kila mtanzania. Nakaribia kujiunga na chama hiki. Taratibu za kuletewa kadi hata sehemu yangu ya kazi au nyumbani zinaendelea. Sibaki tena nyuma. Najiunga na wenzangu. Kwa ajili ya nchi yetu.

Nitajiunga kabla ya kuisha kwa mwaka huu. Waungwana,mtajua hapahapa chama nilichokichagua. Nadhani nitaungwa mkono kwa uchaguzi wangu na wengi wenu.

Asanteni kwa sasa!
 
UNAKARIBISHWA CHAMA CHA WATU, Watu wanaoweza kuthubutu kuchukua hatua pindi inapobidi, chama cha watu ila kimeingiliwa na siafu lakini tayari wameshaonwa na kuangamizawa. Karibu sana mkuu
 
Tangu kuzaliwa kwangu,zaidi ya miaka 30 iliyopita, sijawahi kuwa na chama cha siasa. Ingawa nimekuwa mfuatiliaji wa siasa tangu shuleni na chuoni,sijawahi kuwa na kadi ya chama chochote cha kisiasa. Sababu ni moja:sikuwa nimejiandaa kuwa katika harakati za kisiasa. Lakini sasa ni tofauti.Natamani kuwa na chama na kuwa mwanasiasa.

Ndiyo maana nilijipa muda wa kusoma Katiba,Kanuni,Ilani na Sera za vyama mbalimbali hapa nchini ili nichague chama cha kujiunga nacho. Kwa weledi wangu wa sheria,nimesoma kwa makini na kuelewa ipasavyo. Pia,nimehudhuria mikutano ya vyama tofauti hapa nchini ili kusikia kauli na hotuba zao. Kuna chama kimenivutia.

Hicho chama kina Katiba nzuri;Kanuni zilizo wazi;Ilani inayolenga mema kwa watanzania; na wanachama wanaokipenda chama chao bila kificho. Ni chama kinachoamua kikaamua;kusema kikasema;na kupanga kikapanga.Kimenivutia sana. Nami najiandaa,hata kama hakutakuwa na viongozi wa kitaifa na vyombo vya habari,kujiunga nacho.

Nikishajiunga, weledi wangu wa sheria nitautumia kukiimarisha chama na kukitangaza. Kukifanya chama kiimarike zaidi na kuaminiwa.Chama nitakiheshimu na kukilinda-chama na wanachama wake. Nitaanza na heshima na kumaliza na shukrani. Najua nitaaminika. Kama uongozi hata mimi nimewahi kushika shuleni,chuoni na Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo(Law School of Tanzania).Uongozi una miiko yake,mipaka yake na taratibu zake kuupata. Nikiutaka,nitazingatia hayo kwanza.

Kiukweli kabisa, chama hiki nakiona kama chama chenye dira na makini.Kinalenga watu wa aina na madaraja yote. Ni mdomo wa kila mtanzania. Nakaribia kujiunga na chama hiki. Tratibu za kuletewakadi hata sehemu yangu ya kazi au nyumbani zinaendelea. Sibaki tena nyuma. Najiunga na wenzangu. Kwa ajili ya nchi yetu.

Nitajiunga kabla ya kuisha kwa mwaka huu. Waungwana,mtajua hapahapa chama nilichokichagua. Nadhani nitaungwa mkono kwa uchaguzi wangu na wengi wenu.

Asanteni kwa sasa!
Nami mkuu nina mpango kama wako ... nimeng'amua pasipo shaka kuwa chama nlichokuwa nakitafuta ni chadema ... twende zetu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maamuzi mazuri ndugu..nafahamu uwezo wako na weledi wako kitambo natumai jamii itafaidika na maamuzi yako hasa jamii lengwa ya wasio na sauti..Viva La Amistad
 
Kama chama hicho ni kati ya ccm, cuf au nccr mkuu I will highly discourage you!

chama ni moja tu pipooooozzzzzz
 
Karibu sana kijana, utasutwa lakini unauamuzi murua kabisa...ndicho chama cha watanzania, sio kama kile chama cha rangi ya kijani..real devils
 
image.jpg Usijiunge kwa warusha mawe .....
 
Wakaribishwa kwenye chama makini tena makini sana .........Chama hicho si kingine ni Chama dume Chadema...
 
Karibu chama makini,chenye maamuzi magumu,hakimuogopi mtu hata kama ni kiongozi ukisaliti au ukiwa fisadi unashughulikiwa ipasavyo,karibu chama cha watu makini...
 
UNAKARIBISHWA CHAMA CHA WATU, Watu wanaoweza kuthubutu kuchukua hatua pindi inapobidi, chama cha watu ila kimeingiliwa na siafu lakini tayari wameshaonwa na kuangamizawa. Karibu sana mkuu
Asante Mkuu.Kama upo chama hicho nitakaribia
 
Maamuzi mazuri ndugu..nafahamu uwezo wako na weledi wako kitambo natumai jamii itafaidika na maamuzi yako hasa jamii lengwa ya wasio na sauti..Viva La Amistad
Asante Mkuu.Viva la Amistad entrelos publeos de Cubay Tanzania. Ni kibao cha Ruvu Sec hicho Mkuu
 
Asante Mkuu.Kama upo chama hicho nitakaribia

Ila uje umeshajiandaa psychologically kwamba huwezi kuwa mwenyekiti wa Chama, labda tu utumie tricks za kumwoa mtoto wa Mbowe kama yupo ili baadae wewe uwe mwenyekiti huku Mbowe ameshika remote.
 
MACCM yakisoma hivi roho zinawauma sana.....MRIE TU!!! Watanzania wenye uwezo wa kutafakari wamewashtukia na chama chenu cha wauza unga.

Nami mkuu nina mpango kama wako ... nimeng'amua pasipo shaka kuwa chama nlichokuwa nakitafuta ni chadema ... twende zetu.
 
Ila uje umeshajiandaa psychologically kwamba huwezi kuwa mwenyekiti wa Chama, labda tu utumie tricks za kumwoa mtoto wa Mbowe kama yupo ili baadae wewe uwe mwenyekiti huku Mbowe ameshika remote.

Too low
 
Karibu Kamanda kama uko kijiji CHADEMA HABARI YA WANAKIJIJI

Na kama uko mjini CHADEMA HABARI YA MJINI yamkini siafu walioingia wanaondolewa kwa ajili yako na wengine

Hivyo CHADEMA YATOSHA NA NDO OKSJENI YA MTANZANIA kwenye SIASA na siasa ndo kila kitu.
Chama cha nguvu ya umma na umma hutaki wasaliti ndo maana watu wakiongea bila kutaja CHADEMA mazungumzo hayaeleweki.
Kwenye jamvi na vyombo vya habari haiwi habari mpaka utaje CHADEMA YATOSHA
 
Back
Top Bottom