Nimemzimia Lisa...

Wiyelelee

JF-Expert Member
Nov 9, 2012
1,071
347
Wana JF, habari za siku nyingi...

Napenda niseme ukweli wa moyo wangu. Leo nimebahatika kuonana na kuongea na Lisa! Nilivyomuona tu, moyo wangu ukaridhika kwamba macho yamelenga penye mvuto mkali!. Ahh mtoto wa watu kaumbika, mcheshi na anaushauri mzuri. Nilimsogelea ili nimfahamu vizuri (si unajua taaluma zetu hizi zinatupa advantage fulani!).

Baada ya kukaa nae kama dakika arobaini hivi, tukaongea mambo ya social media. Nikapata nafasi ya kuuliza social media anazozipenda na alinitajia JF kwamba yeye ni mchangiaji mada tu. Tukaongea mengi, hadi kufikia wakati wa ku share majina tunayoyatumia hapa JF.

Nilivyojitambulisha kwamba naitwa WIYELELE, Lisa hakuamini. Alijua li WIYELELE ni jitu fulani maana picha aliyokuwa nayo ya WIYELELE ni tofauti na alivyoniona! Amenichekesha sana hadi basi maana ni muda nilikua sijacheka!

Kusema kweli, nadhani ningekuwa na Lisa kama mke wangu, au mke wangu angekuwa kama Lisa, haa hizo kelel zote za msingeziskia! Angekuwa hajaolewa, yaani angekuwa ka "portable air conditioner ka Wiyelele". Lisa, aliyekupata ana bahati, na akutunze mtoto wa watu ulieumbika! Nimekuzimia!
 
Mpendezeshe ili awe kama Lisa.
Usione vyaelea kaka........................

Kusema kweli, nimejitahidi sana na anapendeza sana mke wangu, tatizo ni mdomo... Pia hanijali, mfano, hamfulii nguo, na kuniwekea chakula mezani. Nguo na chakula vinaandaliwa na wadada wa kazi. Je niache kulalamika?
 
May be Lisa ni wa thamani sana kwako kwa kuwa yupo na mwingine, ila nina mashaka kwamba once akiwa na wewe sifa zote ulizompa ataambulia chache km sio kukosa yote!

"i may not be true"

Mi naona penye uzuri mtu asifie, na penye ubaya napo tulonge.... Lisa ni mzuri, mcheshi na anaushauri mzuri. Naona mke wangu kuna sifa anakosa, ni jeshi...
 
hongera lisa kwa sifa hzo ulopewa...................
....other factors remain constant plzzzzzzzzzzzzzzz

na ndani uwe kama nje usije kuwa gumegume.
 
Mi naona penye uzuri mtu asifie, na penye ubaya napo tulonge.... Lisa ni mzuri, mcheshi na anaushauri mzuri. Naona mke wangu kuna sifa anakosa, ni jeshi...

pole sana!

mara nyingine sio kila mbio lazima ushinde, by now just make sure upo salama na maisha yako na maisha ya familia yako kwa ujumla, mengine yaache yapite tu!

again pole sana!
 
May be Lisa ni wa thamani sana kwako kwa kuwa yupo na mwingine, ila nina mashaka kwamba once akiwa na wewe sifa zote ulizompa ataambulia chache km sio kukosa yote!

"i may not be true"
Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!11 Mbona unataka kunirushia kandege kangu sasa acha wivu bwana.
 
hongera lisa kwa sifa hzo ulopewa...................
....other factors remain constant plzzzzzzzzzzzzzzz

na ndani uwe kama nje usije kuwa gumegume.
sasa Blueprint umenza kunisingizia , mm ni mzuri muulize hata kaka yangu, Mtambuzi analijua hilo
 
Wiyelele una vituko sana wewe!!!! sikutegemea kama utakuja anzisha thread hapa Loh! ningejua ningekukatalia kuwa mm si Lisa, Ila usipate shida sana Onana na Mtambuzi, Asprin, Kaizer, Babu Dc watakuelewesha ni jinsi gani ya kufanya ili uweze kunipata, na kwa upande wa wanawake a kwanza Maddame B, kapipi, mamndenyi, gfsonwin, Lara kubwa la maadui. na wengine sikuweza kuwataja. ukiwaona hao aaaaaahhhhhhhhh mambo yako yatakuwa shwariiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!
 
Kusema kweli, nimejitahidi sana na anapendeza sana mke wangu, tatizo ni mdomo... Pia hanijali, mfano, hamfulii nguo, na kuniwekea chakula mezani. Nguo na chakula vinaandaliwa na wadada wa kazi. Je niache kulalamika?
Kaanza hivi karibu au tangu uchumba?
Unajua wakati mwingine sisi wanaume huwa tunayaanzisha mambo wenyewe.
kuna rafiki yangu mmoja, kabla hajaoa, alikuwa anajipikia, na mkewe huyu alikuta jamaa anapenda sana kupika, yeye akajifanya hajui kupika ili jamaa aendelee na zoezi la kupika.
Walipooana huu utaratibu ukaendelea.
Wakitoka kazini, mkewe anakuja jikoni kumpigisha story huku jamaa yuko tumbo wazi anapika.
Siku moja akatualika kwenye sikukuu moja pale kwake,
tulipomaliza kula tukashukuru na kumsifia shemeji yetu kwa chakula kitamu.
Shemeji akajibu "asanteni, ila chakula hiki kapika BABA JULIE, mie sijui kupika".
waalikwa wakaangaliana, ila shemeji yangu hakushtuka kwa kuwa alijua anamsifia mumewe.
ilinibidi nibadili topic haraka kwa kuwa wageni wengine walikuwa hawajui kamchezo haka ka huyu rafiki yangu.
Up hapo?
 
Uneniable , kwa nn unasema hivyo? yeye kanisifia tu , ila sidhani kama atakuwa anamaanisha vingine, Au????????

Nimemsifia kutoka moyoni, na kwamba iwapo atapata shida yeyote na mme wake, nitakuwa tayali kuwa na wewe Lisa, na kukuvisha taji mpya!
 
May be Lisa ni wa thamani sana kwako kwa kuwa yupo na mwingine, ila nina mashaka kwamba once akiwa na wewe sifa zote ulizompa ataambulia chache km sio kukosa yote!

"i may not be true"
Wiyelele amemjua lisa kwa kuongea naye tu.
Ukiongea na mtu ni tofauti sana na kuishi nae.
Ndiyo maana wakati mwingine unaweza ukamlaumu mtu kwa kusema "Haa, yaani jamaa kamuacha mke mzuri hivi" bila kujiuliza ni kwanini kamuacha.
Anayejua uzuri wa kiatu ni yule aliyekivaa, kwa kuwa ndiyo anayesikia maumivu kiatu kikimbana, na kero kiatu kikimpwaya.
 
Last edited by a moderator:
Nimemsifia kutoka moyoni, na kwamba iwapo atapata shida yeyote na mme wake, nitakuwa tayali kuwa na wewe Lisa, na kukuvisha taji mpya!
Is this love or obsession?
Mbona unatamani aachwe!
utaweza kumpa anachokipata au ili mradi uwe naye?
Na je, uwe naye kwa ajili ya kuipoza nafsi yako au kwa ajili ya kuwaonyesha watu kuwa una mke mzuri.
 
Nimemsifia kutoka moyoni, na kwamba iwapo atapata shida yeyote na mme wake, nitakuwa tayali kuwa na wewe Lisa, na kukuvisha taji mpya!

Weeeeeeeeeeeeeeeee!!! Wiyelele usiseme hivyo, namuomba Mungu kila siku ndoa yangu isiwe na migogoro, na nampenda Mume wangu, so nakuomba usiombee hayo Pls, kama unanijali. Nakushauri wewe mpende tu mkeo atabadilika siku moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom