MPALESTINA MWEUSI
Senior Member
- Jun 6, 2012
- 140
- 117
sitira yake nafuu,mwambie lilo na sahihi
ajue pate fahamu,ajue mali na sio mahari
jipe kazi ya mwalimu,mjuze apate akili
naamini kwako si gumu,mjibu na ajue hili.
Habari wana JF! Mimi ni mwanaume, nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi (mchumba na mali nimetoa kwao) na mdada mmoja hivi kwa muda wa miaka mitatu sasa, yeye ni mwanachuo hapo UDSM na kwa sasa ndo anamalizia degree yake. Last weekend niliamua kumtembelea huko hostel kwake bila kumjulisha, ilikuwa jumamosi nikiwa na lengo la kwenda kumchukua ili tutoke kidogo! Cha ajabu huyo binti sikumkuta, nilipo jaribu kumuuliza mwenzake anaeishi nae chumba kimoja kasema aliondoka tangu jana yake jioni (ijumaa) na hakurudi hadi mida ya saa 10 jioni ambayo mimi nilipofika pale! Nikaamua kumpigia simu, kwavile yeye alikuwa hajui kama mimi nipo pale hostel, akawa ananidanganya eti yupo hostel na tena ameboreka sana, analalamika eti nimemtosa hata simu kutwa nzima sijampigia na mambo mengi! Mimi niliamua kuondoka huku nikiwa nimekasirika sana bila kumwambia kama mimi nimefika pale hostel! Jumapili aliporudi hostel akaambiwa kuwa mimi nilifika na nilimpigia simu nikiwa pale, binti amechanganyikiwa, analia hovyo na anaomba msamaha, tena amemwambia hadi mama yake na dada yake, leo jioni dada yake anataka kuonana na mimi, wadau mnanishaurije? Nimpotezee huyu dada? Kwani mimi nimesha amua kumwacha kabisaa huyo binti, na mali niliyotoa kwao nipo tayari kusamehe!
Ahsanteni wana JF kwa ushauri wenu, nitamwacha rasmi leo na dada yake nitamwambia hilo, na pia ninawaachia mahari yote wabaki nayo!
mkuu nipe mimi basi nibutue, we si unaachaahsanteni wana jf kwa ushauri wenu, nitamwacha rasmi leo na dada yake nitamwambia hilo, na pia ninawaachia mahari yote wabaki nayo!
Namchukia mtu muongo, namchukia mtu asiye muaminifu. Kwa vile roho yako ishaingia kinyongo, basi ni vyema umuache; kipindi cha uchumba maana yake ni kuchunguzana tabia so mshukuru Mungu kwa kukuonesha tabia ya mchumbao.
piga chini bwana.kwanini mtu asitulize k yake.
kwanini ulishwe haramu? kwanini mtu asikitulize,piga chini tena kapime afya yako ujue moja..
I bet to differ
Yawezekana kabisa hakuwa popote pabaya labda kwa rafki yake na aliona akikwambia ungemkatalia coz wanaume wengine mnapenda sana mapenz ya kugandana,somtimes you may need a break to do silly things with your friends,,,so hapo kosa lake ni kukudanganya na kutokukuaga.....ambayo sio makubwa ya kuvunja uchumba,don't reckon with any advice bila kufanya upembuzi yakinifu baba
Better the devil you know than the angel you don't know
Ahsanteni wana JF kwa ushauri wenu, nitamwacha rasmi leo na dada yake nitamwambia hilo, na pia ninawaachia mahari yote wabaki nayo!
Ukiona mwanamke au mwanaume amekubali kutenda tendo la ndoa kabla ya ndoa basi huyo ni mzinifu, na hawezi kuwa mwaminifu kamwe, kama unabisha anza uchunguzi kwa watu wote waliozini kabla ya kuoa au kuoana utaona sio waaminifu. Labda mtu aamue kumrudia mungu kiukweli hapo anaweza badilika lakini hakuna mabadiliko kama mtu hana dini ya kweli, ukioa au kuolewa na mtu asiye na dini ya kivitendo hakuna uaminifu hapo. Sasa sijui wewe sinai unaleta hoja gani hapa kama mliweza kushiriki tendo la ndoa kabla ya ndoa basi jua uaminifu hakuna hapo. Oa tu kama fashion lakini sio kumiliki peke yako