Kwema ndugu zangu watanganyika? Kutokana na mimi kupitia changamoto za kifedha kwa sasa, nilimuomba Wife tupunguze gharama za uendeshaji wa maisha yetu kwa kujibana sana, pendekezo langu la kwanza nilipendekeza Wife anyoe nywele zake alizosuka, akajitetea kwamba nywele zake katumia karibia miaka 10 kuzifikisha hapo zilipofikia hivyo hatoweza kuzinyoa na akaongezea kuwa akinyoa yeye huwa ana kichwa kibaya hivyo hatokua comfortable.
Basi mimi nikajaribu kupitia kwenye baadhi ya pages za wadada wenye saloon huko Instagram nikaja na pendekezo moja kuwa Wife awe anasuka style fulani hivi ya nywele ambayo ni affordable kwani ni elfu 5 tu ila mwenzangu nilipomshirikisha hivyo akaishia kunisunya na kunibinulia midomo kuwa hayuko tayari.
Mpaka sasa kaninunia ila mimi msimamo wangu uko pale pale sitotoa zaidi ya elfu 5 ya kusukia.
Asanteni
View attachment 2044854

Huo msuko unaoitwa mkataba ndo upi weka picha tuuone wengine hatuufahamiBora umwambie asuke mkataba 55,000 anakaa nao mwaka gharama ni 10,000 kuosha na kubadilisha style ukichoka
Mkataba ni nickname msuko waitwa afrokinkyHuo msuko unaoitwa mkataba ndo upi weka picha tuuone wengine hatuufahami
Okay thanksMkataba ni nickname msuko waitwa afrokinky
KaribuOkay thanks
Mimi sina dhiki ndogondogo mkuuWe ndie unaendana na mshkaji, bora mlianzishe tu!!
hizo dhiki ndogondogo ndio zilizomfanya mwenzio aonekana mzigo, sasa wewe unaeweza kukabiliana nazo mwenyewe huoni ukiwepo hapo amani inaweza kupatikana!?Mimi sina dhiki ndogondogo mkuu
duuhAta abane miaka 40 kwangu atakuwa best tu