papiso
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 391
- 230
Salam wanajamvi na vijana wenzangu wa dar ambao ni wamiliki wa nyumba. Leo nimeandika hili na nimeonelea bora nipate kidogo maoni yenu hili niweze kusonga mbele. Kwa kifupi nina wapangaji zaidi ya kumi na wote ninaishi nao kwa amani na upendo ila kuna mmoja kati yao akaanza kubadilika. Pale unamsihi juu ya jambo flani kama baba mwenye nyumba anakuwa mkali na kutoa lugha chafu.
Tabia hii ilipokomaa huyu mtu nikampa notice. Sasa siku nampa notice ndio akanivulia uvivu kabisaaa na akaanza kuniporomoshea matusi tena mazito mazito ya nguoni ilihali mpangaji huyo ni mdogo kwangu kiumri kiuwezo kielimu hadi kifedha na hata nikisema nichukuwe hatua ya kumpiga nitamuumiza vibaya.
Baada ya kupokea matusi yale akili ikanituma nielekee kituo cha polisi moja kwa moja na kweli nilifika nikapewa barua ya kumuita mtu huyu.
Sasa naomba ushauri, niendeleee ama nisiendeleee. Asanteni