Nimelipanda mwenyewe.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimelipanda mwenyewe....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Magulumangu, Jun 18, 2011.

 1. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Milima linaipanda,sekenke hata kitonga,
  Wami kona kuzipinda,likielekea tanga,
  kamwe silipi mnada,hata uwe kiti nanga,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  Sio la Yakuonea,alojuta kulipanda,
  kamwe sijaliotea,mwanakijiji kupanda,
  mkokoteni semea,yeye alishaupanda,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  Sipidi yake hatari, hata gavana halina,
  Aisi ndani mahiri,madirisha ni hamna,
  za mbali zake safari,usiku hata mchana,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  yale maswali hayapo,ulikuwa wewe wapi,
  linapandisha mapepo,asipirini u wapi,
  Ginesi watakuwepo,kulipa hadhi si kopi,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  Halianzii na moja,mbili gea ni yake,
  tano sita kwa pamoja,kuchemsha kamwe kwake,
  Litakutia kioja,taka umiliki wake,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  Wengi walolipanda,mwisho wake hushukru,
  hata wa kiparang'anda,lishawahi kunusru,
  madenti wengi kupanda,watokeapo kisuru,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  Sishauri ulipande,kama hutorishuka,
  Sitake chake kipande,walahi hutonasuka,
  nasema hata kwa mande,nyie mlo na hulka,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,

  klorokwini mtu wangu,hata sinyoshe mkono,
  acha liende marangu,maana si konokono,
  lasafiri ka mawingu,lisije vunja kiuno,
  Nimelipanda mwenyewe,sitamani kulishuka,
   
Loading...