Nimelikoroga naombeni msaada; Nimeingilia mawasiliano ya mpenzi wangu

Anna pita

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
227
425
Nimelikoroga nisaidieni jinsi ya kulinywa ninampenzi wangu alipata uhamisho alipokua anafanya kazi gafla kuna dada alikua anafanya nae kazi yakaibuka mazoea mawasiliano ya mara kwa mara si asubuhi, mchana , jioni mpaka usiku.

Nilipohoji nikaambiwa hii nikutokana tulikua tumezoeana kukaa wote sasa tunamisiana sawa nikaelewa ila mazoea yakazidi ikafikia hatua jamaa akiamka asubuhi cha kwanza amjulie hali yule bibie.

Anaweza mpigia hata mara 10 simu wanachart mpaka saa 6 usiku sasa kwa akili ya binadamu nikaingia wasiwasi nikawa nimeinstall app kwenye simu yake ya kupata mawasiliano take.

Hapa ndipo nilipokosea maana niliweza kujua kila kitu walikua wanawasiliana sometimes ananipigia ananiambia kachoka ananiaga kulala anakaa dakika 10 anampigia yule dada wanaongea mpaka saa 8 usiku nikihoji naambiwa just friend japo nilochogundua walikua hawajaanza kudate ila walikua na interest nilimwambia sipendi ukaribu wao akaomba msamaha atajirekebisha alichofanya wakabadilisha namba nayo nikaifahamu.

Kuna siku jamaa akanipa hela nimpikie chakula flan walikua anakipenda na alikua katoka safari ajabu jioni akaenda kula kwa yule dada kaja saa 5 usiku na kudai kashiba ilinikwaza sana ikabidi nimwambie matendo yake yote ila nikamwambia kuna mtu kachukua simu ya yule dada ndio inanipa taarifa.

Jamaa kwamwambia mdada kua nimehack simu yake hint tangu jana anataka kunipeleka police mimi nimemuelewesha kua sijashika simu yake kakataa kachukia kampigia jamaa anamtukana jamaa kachukia kwanini nimesababisha rafiki ake kachukia.

Nimemuomba msamaha mpaka nimechoka jamani anakubali kanisamehe ila ndio hapigi simu wala meseji nikimpigia anajibu kwa ukali sana naombe ushauri nafanyaje juu ya hili
maana nitajibu nini wakati anawiki 2 tangu ametoka kujitambulisha nyumbani tena mbele ya baba nikiwaza natetemeka mwil mzima
 
Hilo ndilo ulilokuwa unalitafuta, sasa kwa kuwa wewe ndio umemkosea, japo mkosaji ni yeye, ila kwa sasa ili akusamehe jamaa atataka umpe channel O, utakubali? punguzeni kuwapeleleza wapenzi wenu sio wewe tu karibia wote hii tabia mnayo.
 
Sasa siume sha prove kwenye chat zao kuwa wanatongozana on your back sasa wao sindio waliotakiwa kuwa wapole inakuwaje wanakugeuka wewe na wewe una kuwa mpole badala ya kuwa mkali.

Uyo mtu kama anafanya hayo yote mkiwa hamja oana mkiona utajuta yani hiyo ni ishara hakupendi hawezi fanya ujinga huo wazi wazi kihivyo dada jitafakari kujitambulisha kwa baba siyo issue just wambie wazazi huyo mtu umeamuona kuna vitu haviko sawa so ume amua kuachana naye utaishi maisha ya mateso sana mkifikia kuwekana ndani
 
Kwa sababu umelikoroga mwenyew inabidi ulinywe tu uwe mvumilivu
 
Mama kusoma hujui hata picha nayo huoni ninachoweza kukwambia ni pole, badala ya kumfikiria huyo jamaa wako, tumia huo mda kufanya mambo mengine mfano kudili na shughuli zako n.k

mwanaume hachungwi, utakufa presha.
 
Mbona kosa bado liko kwa jamaa we ndo unahaha

Labda tumuulize umri kwanza, is she that desparate kuolewa? na kwanini asiwe na maamuzi magumu? "ya kuachana of course"

Kweli mapenzi yanaua/kuumiza but asije subiri kidonda kikakua ndo achukue maamuzi
maamuzi ni sasa na shuhuda ziko nyingi humu

Ila pole kwa mtoa mada maana inaonyesha anampenda sana jamaa na hizi ndizo fadhila za kupenda kupitiliza
 
Maanaume wako ana kosa lakini approach yako sasa ndio umekosea kiufupi jamaa anachepuka na huyo dada, na tena mpaka anampigia mara 10 ina maana amehamusha hisia huko.

Sasa dada wewe toa taarifa kwa ndugu na wazizi wake kuhusu tabia ya mwenzio, baada ya hapo jiweke pembeni wala usijiusishe nae
 
Hata kama ni upendo best umepitiliza yaan yaani mtu mda wote wanachat alafu we kama mke mtarajiwa kuuliza umeonekana kama unawaingilia mambo yao maana yake hupaswi kujua in &out kuwahusu wao yupi mwenye thamani sasa kati yako na huyo mke mwenzio , yes mke mwenzio maana kwa kawaida wao ndo walitakiwa wawe wapole na wajishushe

Kataa kuwa mjinga
Kuwa na msimamo
Kujitambulisha sio solution ya kukudhalilisha kiasi hicho kwa limtu la nje ngoja niishie hapo kwanza
 
Hata kama ni upendo best umepitiliza yaan ,, yaan mtu mda wote wanachat af we kama mke mtarajiwa kuulza umeonekana kama unawaingilia mambo yao maana yake hupaswi kujua in &out kuwahusu wao .... yupi mwenye thamani sasa kati yako na huyo mke mwenzio , yes mke mwenzio maana kwa kawaida wao ndo walitakiwa wawe wapole na wajishushe ...

Kataa kuwa mjinga
Kuwa na msimamo
Kujitambulisha sio solution ya kukudhalilisha kiasi hicho kwa limtu la nje
NGOJA NIISHIE HAPA KWANZA.....
na kweli ishia kwanza hapo
 
Binadamu bhana nilichogundua wakihisi, awe mwanaume/mwanamke kuwa unapenda kupita maelezo lazima akuumize tu na sisi sasa ambao tumeshajua haya hatuendelezi hayo maisha kabisa

Tunajisaidia na kamsemo kanakosema LOVE DOES NOT EXIST (na haka kamsemo lazima ukapende baada ya kutendwa na kupona) basi roho swaaaafi unajipenda mwenyewe na maisha yanaenda hii mambo ya kumpenda binadamu mwingine zaidi ya unavyojipenda ni hatari kwa afya ya mhusika (mhanga of course)
 
Back
Top Bottom