Nimekuwa na uraibu wa pombe! Natubu 🙏🏽

Nimekuwa na uraibu wa pombe! Natubu 🙏🏽

Naungama

New Member
Joined
Feb 11, 2026
Posts
1
Reaction score
20
Salam,

Kwanza nianze kwakudeclare mimi ni member mtiifu wa JF since 2011, ila nimeamua kuja na utambulisho huu mpya ili niweze kuwa huru zaidi kueleza yanayonisibu na kupata msaada, mimi ni kijana wa makamo, on my 30's lakini kwa zaidi ya muongo na nusu nimekuwa mteja wa pombe, yes "uteja". Hapo mwanzo wakati naanza sikuona kama ni tatizo kwangu kwasababu sikuwahi kuona madhara yake na niliona nisehemu ya ujana na ukuaji.

Lakini kadri umri ulivyokuwa unakwenda nilianza kuona madhara ya moja kwa moja yaliyotokana na pombe, karibia changamoto zote za kimaisha zilizonitokea zilisababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe, naomba ieleweke, sipo hapa kufanya watu waache starehe ya pombe sababu kila mtu anakunywa kwa sababu zake na mimi ni shahidi wa watu wengi ambao wanakunywa na bado wanafanya mambo yao responsibly.

Kikubwa kilichonifanya nilete uzi huu hapa jukwaani ni issue personal ambayo imekaa kiimani zaidi na natumaini wapo wajuzi zaidi wenye kuelewa haya mambo, kama ambavyo nimeeleza hapo awali baada ya utumiaji wangu wa pombe kwa kipindi kirefu mambo yalianza kunibadilikia mfano riziki ikaanza kuwa ngumu kwangu (mimi ni mfanya biashara) kila kukicha kazi zinaharibika sababu kubwa ni pombe, issue za kuchelewa kufika kwenye appointments, au kufika nikiwa "mtungi" na kusababisha kupoteza deals mbali mbali, ajali mbalimbali na injuries za kila kukicha, kugombana kwenye mahusiano mpaka kupelekea kuachana na wapenzi wangu n.k haya yote yamekuwa yakinitokea mara kwa mara ni kama kuna kitu kinaniambia niachane na lifestyle yangu hiyo lakini wapiii nikikaa mwezi mmoja na zaidi mambo yananinyookea ila nikirudi kwenye pombe huwa narudi kwa kasi ya ajabu na matokeo yake matatizo yanarudi upya.

Kuna muda nasema labda nijaribu kujifungia ndani ninywe bia mbili tatu nilale ila tatizo huja pombe ikianza kuingia kichwani nitatoka kwenda kutafuta viwanja hata kama ni saa nane usiku ili niendelee kulewa na badala yake kinachofuata huwa ni majuto kila kukicha.

Nimejaribu kuonana na viongozi wa kiroho na nimekuwa nikifanyiwa counseling na maombi na huwa natulia lakini siku nitaposema niguse hata pombe kiasi basi inakuwa ni non stop na hakuna turning back mpaka nitapopata majanga.

Hali hii imekuwa ikinisumbua sana na kunifanya nikose raha na majuto kila kukicha, nimepoteza marafiki wengi wa muhimu kisa ulevi, nimepoteza deals na connections muhimu kwenye utafutaji wangu kisa ulevi sijui nifanyeje nijitoe kwenye hii laana inayoniandama.

Baba yangu alikuwa mlevi sanaa mpaka akapoteza kwenye maisha, kabla babu yetu (baba yake) hajafa alimuachia maneno ya laana "usipo acha pombe, usije kunizika" na mpaka anakufa alikuwa bado anatumia kilevi ila baada ya maziko ndio ikawa mwisho wake kunywa, sitaki kuamini kuwa yale maneno ya babu kwa mwanae (baba yangu) has something to do na ninachokipitia lakini all in all natamani kubadilika natamani kuanza upya maisha bila ulevi lakini siku zote nimekuwa nikijiambia hili baada ya kupata majanga ila baada ya kukaa sober hata mwezi kuna siku tu ni kama pepo linaniingia najikuta nimekuwa katika hali ya ulevi hata wiki nzima (overly drinking) na sometimes nazima kabisa plus majanga lazima yanikute,

Mficha maradhi kifo humuumbua nimekuja mbele yenu ndugu zangu mnisaidie, huku mtaani ndugu jamaa na marafiki mpaka viongozi wa kiimani washaniona i'm a joke sababu kila siku natoa ahadi ya kuacha lakini baada ya muda narudi kule kule, nachukia hali hii, nahitaji msaada 🙏🏽.

N:B Sina mke wala mtoto na hapa mjini (Dar) sina ndugu wa karibu sana zaidi ya jamaa tuliojuana ukubwani, wazazi wote wapo mkoani.
 
Tunafanana sema mimi ugomvi wangu nikishakunywa siwezi kula hivyo nauchosha mwili wangu kwa muda mrefu kisha naujenga kwa muda mfupi kisha nauchosha tena... Hapa nilipo nahisi figo na maini vinanizomea 😪

Hebu jitahidi uoe mwanamke asiyependa ulevi alafu ndio tukushaurit
 
Pole sana..umelithi kwa baba bilashaka!! Ngojea waje kukupa ushauri! Sisi wenzio sio walevi,kwa mwezi tunakunywa mara mbili tu! Tena pombe laini zisizodhidi beer nne au tatu for refreshment,na pombe haijatutawala......

shetani ni adui wa mwanadamu aliye dhahiri
 
Tunafanana sema mimi ugomvi wangu nikishakunywa siwezi kula hivyo nauchosha mwili wangu kwa muda mrefu kisha naujenga kwa muda mfupi kisha nauchosha tena... Hapa nilipo nahisi figo na maini vinanizomea 😪
Kuna kisa kimoja kilitokea..
Jamaa alikua anasumbuliwa sana na uraibu wa pombe, siku aliyotaka kuacha alinunua sumu ya panya na konyagi ndogo.
alimimina Ile konyagi kwenye glass mbili. Glass ya kwanza akaweka Ile sumu ya panya, glass ya pili akanywa yeye bila kuweka sumu. Tukamuuliza kwanini iyo glass nyingine umeamua kuchanganya konyagi na sumu ya panya akajibu nataka konyagi nayo ionje joto la sumu maana imenitesa sana😁.
Jamaa aliacha pombe kwa style hiyo mwakawa pili sasa
 
Kuna andiko linasema maisha ya faa nini bila pombe? pombe ni nzuri kwa kiasi na wakati wake. Kunywa kiasi na kwa wakati, kula ushibe ndipo unywe, kunywa maji mengi, zingatia matunda na mazoezi. Tenga muda wa kunywa na wakupumzika baada ya kunywa. Tumia walau saa 4 kupumzika mf kulala ndipo ufanye shughuli na uwapo kazini usinywe pombe.
 
Nshawahi kupitia the same situation.....nakumbuka kilchonsaidia ilkua siku nloamua kukesha sku tatu mfululizo kansan ....bora hata wewe ulkua unaweza kusimama hata mwezi....m within 4yiaz consecutively skumbuki kama zilshawah kupita hata siku tatu bila kugusa kileo......its possible ukiamua....iponye roho kwanza then mwili utajiponya automatically
 
Back
Top Bottom