Nimekuwa emotionless, cold

TheGodfather95

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,764
Reaction score
1,836
Hello,

Mimi ni last born katika familia yetu kwa bahati mbaya mama alifariki nikiwa mdogo (6years) hadi hapa nilipofika nimelelewa na ndugu upande wa mama.
Makuzi yangu hayakuwa na upendo kama ambao ningepata kutoka kwa mama.

Nimepitia mengi lakini sidhani kama ni jambo jema kuyaweka yote hapa lakini nimepitia misoto mingi masimango nilikuwa nakuwa wa kwanza darasani hadi nikajikuta uwezo unapungua kila nikipanda madaraja lakini namshukuru Mungu mwenyezi nimemaliza masomo yangu ya elimu ya juu.

Sasa kutokana na hali hiyo nilijikuta naweka nia nitafute pesa kwa hali na mali ili nije lipa visasi. Honestly ni mtu nayeweka vitu moyoni sivitoi na nikishakusudia jambo lazima nilifanye hata mda mrefu ukipita.

Hii hali imenifanya kuwa mtu nisiye na hisia sipendi mtu akinipenda namuumiza yani sipendwi kupendwa nimeumiza watoto wa watu of which I'm guilty nimewapotezea mda kutokana na mimi kutokuwa na hisia.

Hii hali imenifanya nijue nilimpenda mtu mmoja tu maishani mwangu (mama) yani nafanya vitu vingi ili nilete heshima kwa jina lake maana alifariki akiwa mtu mwenye heshima na mali. Nimekuwa nikifanya vitu kurudisha heshima ya mama nirudishe mali zake na heshima.

Kitu kinachoniumiza ni kuwa tofauti na watu wengine sina hisia niko kama robot mimi furaha yangu ni pesa tu pesa ndio inanipa furaha na amani ya moyo.

Najiuliza ni kukosa malezi ya upendo ama ni maisha yalivo ni shape ama nakuwa gaidi bila kujijua?

Natamani kupata therapy niondokane na huu ubaridi.

Mwenye msaada naomba.
 
Pesa ndio sabuni ya roho, hayo mengine ni kiherehere!!
 
pole sana...ila mwachie mlipaji(Allah)
 
Kutambua tatizo ni hatua pia, cha msingi dhamiria kutoka moyoni kutokutenda yale ambayo yataumiza wengine, tafuta amani na watu wote (samehe waliokukosea na wewe omba msamaha kwa uliowakosea).Muhimu kabisa jitahidi kuomba kwa imani yako na shirikisha viongozi wa dini yako, Mungu ni mwema atakusaidia tu.
 
Huo ndo ukidume..dunia ya saizi ni ya kuwaza pesa tu ..kwa sababu siku iz mapenz pesa..sasa unatapatapa nini jomba...
 
In short wewe ni mlemavu.
 
Samehe kwanza ndo utapata amani, bila hivo utaishi maisha ya shida, pesa sio kila kitu, jitahidi kusali na kuhudhuria vipindi vya dini, na usipobadilika unakuja kujuta baadae
 
Samehe kwanza ndo utapata amani, bila hivo utaishi maisha ya shida, pesa sio kila kitu, jitahidi kusali na kuhudhuria vipindi vya dini, na usipobadilika unakuja kujuta baadae
Aksante Dada angu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…