Nimekutana na changamoto hii nikifuatilia passport, naombeni ushauri

Kabadili Nida. Cha muhimu cheti cha kuzaliwa kifanane na Nida. Leaving certificates achana nazo.Sema uliishia la saba.
 
Ok, nenda mahakama ya ardhi ukaape kisha wakupe deed poll certificate.
Au nenda kwa msajili wa vizazi na vifo ukaombe cheti cha kuzaliwa 1993, kisha utalipia 10 after 7 days unaenda kukichukua.

Shukran mkuu kwa ushauri.
 
Kabadili Nida. Cha muhimu cheti cha kuzaliwa kifanane na Nida. Leaving certificates achana nazo.Sema uliishia la saba.

Cheti cha kuzaliwa ninacho mkuu ndio hicho hicho nilikitumia kupata namba za nida bila usumbufu issue ni kwenye hicho cheti cha kuzaliwa jina la baba mzaa mama(babu yangu mimi) halipo ndio maana immigration wakakikataa wanataka nikatafute cheti kingine.
 
Kwa hiyo mama yako hana Baba?Kwa nini cheti hakina jina la Baba wa mama yako?
 
Halafu si utengeneze affidavity ya Baba.Maana uhamiaji tunapeleka affidavity ya mzazi mmoja tu.
 
Sasa kwenye cheti cha kuzaliwa Mama yako hana Baba,then kwenye affidavity yake ana Baba.Hapo haikubaliki. Ila kama Baba yako yeye ana Baba kwenye cheti cha kuzaliwa.Si upeleke Affidavity ya Baba.Maana Jina la Mzazi kwenye cheti cha kuzaliwa linatakiwa liendane na affidavity yake.
 
Affidavit ya mama niliambatanisha pia kwenye fomu mkuu ila bado wanasumbua.
Ndo kosa kubwa.Maana kwenye affidavity ana jina la Baba,kwenye cheti chako cha kuzaliwa hana Baba.Hapo Passport hutatengenezewa hata aje Yesu. Halafu uzuri Uhamiaji wanataka affidavity ya mzazi mmoja tu.Si upeleke ya Baba? AU Peleka ya Mama ila usiweke jina la Baba yake kama ilivyo kwenye cheti chako.
 
Nchi ya kitu kidogo, nchi ya watu wadogo
 

😂😂
Ulimpa Rushwa sio??

Ni muhimu documents zako zifanane hata kama hufuatilii Jambo lolote lile.
 
Nchi hii bila Rushwa Mambo hayaendi. "RUSHWA NI ADUI WA HAKI" Wakati wewe unahangaika kwenda RITA etc Kuna mtu hapo katoa elfu 50 tu haulizwi hata swali ..fomu inapitishwa fasta anasubiria kupigwa picha ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…