mtu asiye na akili timamu labda ndo anayeweza kusamehe na kusahau...tunasamehe tu ila hatusahau
Taahira tu na mwenye mtindio wa ubongo ndio anaweza kusamehe na asisahau. Mwenye akili timamu husamehe na kusahau au kutokusamehe na kutokusahau. Umesamehe alafu husahau ya nini umesamehe.
Hilo neno tunasamehe hatusahau wewe na nani? Kama wewe unasamehe ila husahau sema wewe sio kujumlisha watu wote. Wengine tuna akili timamu na hatuma matatizo ya mtindio wa ubongo.
Kusamalehe na kusahau ni kama kidonda kugeuka kovu. Unaweza samehe na roho isikuume ukikumbuka, hapo ni sawa na kidonda kugeuka kovu, unaliona kovu ila halikuumi tena maana liliisha pita. Ukubwa wa kovu hutegemea na kidonda kilikuwaje..
mmh kusahau na kusamehe vinauhusiano gani?
Hivi kusamehe ni kujisahaulisha unacho kumbuka?
Habari ndugu zangu wa Jf,
Hili ni jambo ambalo linanitatiza kidogo hivi kumsamehe mtu maana yake ni nini hasa? Na ukimsamehe mtu lile jambo alilokutenda ni lazima ulisahau? Na vipi umemsamehe lakini bado unalikumbuka na linakuumiza si msamaha huo?
Naombeni expirience yenu mliowahi kuwasamehe watu waliowaumiza kama ni kweli unasamehe na kusahau? Binafsi nasamehe sana ila sisahau nilichotendwa.
Naombeni msaada kama na mimi ninaweza kusamehe na kusahau au kutokusahau lililoumiza ni tatizo la kila mtu nami niendelee kusamehe na nisisahau.