Nimekumbuka wimbo wa Chidi Benz uitwao 'Mmenisoma?'

kabisa,huo wimbo ulikuwa wimbo wa taifa enzi hizo tv pekee ni ITV
Hahahaha shooting nyuma kuna kitambaa cha bluu kimetandazwa na ndiyo background hiyo hiyo.

Jela ya Fm Academia (Wajela jela) na yenyewe shooting yao ilikua hivi.
 
Hahahaha shooting nyuma kuna kitambaa cha bluu kimetandazwa na ndiyo background hiyo hiyo.

Jela ya Fm Academia (Wajela jela) na yenyewe shooting yao ilikua hivi.
Shooting ilikuwa inafanyika hapohapo studio na nyimbo zinakuwa za Taifa, sahivi video hadi ibambe sharti utumie Red Camera kwa Hanscana ama uende kwa Madiba, maisha yanaenda kasi
 
Shooting ilikuwa inafanyika hapohapo studio na nyimbo zinakuwa za Taifa, sahivi video hadi ibambe sharti utumie Red Camera kwa Hanscana ama uende kwa Madiba, maisha yanaenda kasi
Sana aisee, 2 eyez production na royal production ndiyo walikua wanashindana.

Mwananchi video production alibase kwenye muvi ila ile video ya Nakupenda ya Abby Skills, Zahrani na Dully ikawa imeleta kitu chenye msisimko sana
 
Hapa tunasubiria ulimwengu uanze shule yake maana hakunaga namna nyingine hapo
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Ongezea na hizi;
Fad-moyoni naumia
Shetta-Mdananda
Solid Ground Family-Mechi Kali
Jebby-marehem kaacha orodha
Joslin-mshkaji mmoja
 
Hii nyimbo aliitoa baada ya kuchukua tuzo mbili za hip hop kwenye KTMA na watu kumdisi sana kuwa hakustahili kwa kuwa hakuwa hajulikani sana. Jibu lake ndo hilo 'MMENISOMA'
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Mkuu nilisema kwangu mimi...that's means kila mtu Ana mtazamo wake.

Narudia tena kwangu mimi huu ni wimbo bora kuhusu janga la ukimwi pembeni ya starehe na Alikufa kwa ngoma hizo ulizotaja wewe zitashika nafasi ya 4 na kuendelea ila tatu bora yangu ni Alikufa kwa ngoma,Starehe na Mmenisoma.

Kama natengeneza top 5 nitaiongeza Zawadi ya Late Mangwea na ngoma ya Solid Ground Family inaitwa Mechi Kali.
Hivyo yaani.
 
View attachment 453493

Chid Benz
Mkali toka ILALAAAAA dah amenikumbusha mashairi ya HIT SONG Mmenisoma.
Ndani ya ngoma kuna sehemu CHUMA ana ghani.... "mwenye dawa mfukoni nyonga tumeze".

Pia mbele kidogo anasema "hawezi kujibana, nataka ni ule ujana kwa nia njema bila kufanya laana.
Kinga madhubuti na kuepuka vishawishi kwani anajua akiteleza ANA ANGUKIA MAZISHI"

Chid anasema ruka utakavyo, jiachie uwezavyo ila JALI UHAI MARA NYINGI UONAVYO!... baadaye anatuasa hivi "Mkumbushe Mwenzio kama hujapatana nae, kama somo halimwingii MPOTEZEE achana nae kisha ana malizia kwa kusema JIACHIE RUKA MAJOKA, RUKA STYLE ZOTE UNAZO PENDA, UWANJA WAKO, MUDA WAKO CHEZA VILE UNAVYOWEZA, Ila DUNIA CHAFU KUWA MWANGALIFU USIFUATE MGUU UNAPOKWENDA.

Ubeti mwingine ana anza hivi "akili ishalegea, wengi wanapotea hasa waliofumba macho wakahisi wanatembea, maneno yao UTASIKIA NA_TAKE CARE

Mvuta Bangi ana kamatwa!
Mnywa gongo anakamatwa
Kwanini Watumia madawa ya kulevya
Wasikamatwe?

Nimeichomoa Facebook
Ile freestyle ya matusi mazito mazito hujaikumbuka? Uhai, mafanikio na afya huwa vinatupumbaza sana waja tunasahau kavitoa nani!
 
Ujafa ujaumbika inasikitisha MTU aliesimama vizuri kwenye sanaa Leo anakuwa teja, tumuombee arudi hali ya kawaida,yeye nae hakuwahi tukana watu kwenye kampeni Leo ye mgonjwa walotukanwa wazima,tusiringie afya ni ya Mwenyezi Mungu
 
Mpiga Debe - Mzimuni Family, Msinitenge - Prof Jay, Sukari na Pilipili - SoloThang, kuna nyimbo nyingi kali za ukimwi bila kusahau ile ya ngwea ft TID -Bado Nimo
Brother huu wimbo wa Mpiga Debe unao unisambazie upendo Mkuu?

"Kupiga debee kwangu ilikuwa poa, fani katika maisha ikaja kuniokoaaaa... Kwa hadhi ya wazazi kijijini nika oa......."
 
Back
Top Bottom