Nimekumbuka wimbo wa Chidi Benz uitwao 'Mmenisoma?'

Kuna verse moja alisema '' Namanisha tendo sio lazma basi japo hakupige hataa busu''

GooD poinT!!
 
Ni rahisi kuona tu kwa wenzio lakini inasikitisha sana..Siku moja nilimuhagi binamu yangu Karume akiwa anapiga debe nikampa na pesanikiwa ndani ya hijab watu walinishangaa sana,lakini hivi ndio nilivyokua nikifanya akiwa mzima nae akiniona anaanzisha kunikumbatia..Hili swala linaniumizaga sana.
 
Kitu kimoja najua. Ipo siku radio zote, zitapiga ngoma zote za Chidy masaa yote.
 
Huu wimbo ulinifanya nimuheshimu sana Chid.

Beat nzuri kutoka kwa Goodfather P.Funky Majani ilibebwa na sauti nzito yenye mamlaka kutoka kwa Chid Benzino.
Verse anazungumzia starehe tu na kujiachia viwanja na hata wenye dawa mfukoni anawapa ruksa wanyonge fresh tu.

Ila verse ya pili na ya tatu anabadilika kabisa kama sio yeye anazungumzia UKIMWI kwa namna ya kipekee kabisa ambayo itakuacha na mstuko.
Mtu aliekwambia muende club,kuruka majoka na kuvuta bange anakuhusia kuhusu ukimwi.

ukiondoka Alikufa kwa Ngoma ya FA na Starehe ya Feroos Huu ndio wimbo bora zaidi wa UKIMWI kwenye bongo flava.

Kwangu Huu ndio wimbo bora zaidi kutoka kwa Rashidi pembeni ya Dar es Salaam stand up na Hasira za nini


mzaramo sikiliza "Homa ya Dunia" kutoka kwa Solo Thang na "A.K.A. Mimi" ya Albert Mangwea (RIP) kisha uje kubadili kauli zako hapa.
 
uswahilini Matola..kosa la marehemu hakuvaa condom...ndio Kali zaidi
 
Back
Top Bottom