Habari wa jukwaa letu la lfdoctor?
Jamani nimekata tamaa ya kupona macho, nimetembea kwenye hospital nyingi tu naambiwa hawaoni tatizo wananipa tu ushauri wa kula vyakula na matunda na pia kutumia miwani ili kurekebisha uono hafifu, hii ina maana kuwa hospital hakuna tiba ya macho zaidi ya kupewa miwani tu.
Mimi binafsi sipendi kutumia miwani bali ni kupona kabisa tatizo la macho, niliwahi kuambiwa nimechezewa lakini hata tiba za jadi hazijanisaidia zaidi ya kufuja pesa. naombeni ushauri wadau nifanyeje?