Abti
Senior Member
- Feb 27, 2025
- 101
- 182
Mimi sio mjuzi wakuandika uzi JF hii ndo mara yangu ya kwanza na inaweza kuwa ya mwisho kama kuna makosa jitahidini kuelewa.
Niende moja kwa moja kwenye mada, nahisi leo inaweza kuwa siku yangu ya mwisho kwenye huu uso wa dunia ila nitakuua nimeacha maumivu makubwa sana kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.
Najua nina makosa mengi sana nitakuwa nimefanya niliowakosea naomba radhi mnisamehe kwa dhati na mniombee kwenye safari yangu.
Kosa langu kubwa ni kushindwa kuelezea mambo nayopitia, kiukweli nimeshajaribu kujitoa uhai zaidi ya mara nne lakini ikashindikana na kuona Mungu ana kusudio na mimi ila bado kwa upande wangu nimeshindwa kukaa sawa mpaka nahisi kuwa nina shida ya akili ama kuna kitu kingine
Sijui napoenda kama kuna mapumziko ya kweli ama laa, umri bado ni mdogo miaka 29 naingia ila sina uelekeo wala utulivu wa akili kutokana na wakati mgumu naopitia akili mwangu na moyoni mwangu.
Nimeona hata ikitokea nimeondoka kwenye hii dunia niache uzi huu nikiondoka nitakuwa nimeacha binti yangu mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne aliyeanza kuita baba na mama tu atakuta historia ya baba yake kwa namna tofauti kwamba hakua jasiri ama kifo kilimshinda.
Ndugu jamaa na marafiki binti huyu ni dhamana yenu nawaomba uangalizi wenu kwake akiwa mdogo na hata akikua.
Watu wa mzaha nitaona ni kawaida hii ila mwisho mtakuta habari tu yalioadikwa yametimia japo namuomba Mungu anitie nguvu kuniepusha na hili tendo nawapenda sana wote.
Kama kuna mtu amebarikiwa kunipa ushauri utakaogeuza mawazo yangu nipo hapa kwa masaa machache kupokea jitihada zako.
Asanteni sana DEPRESSION IS REAL.