Kwa maoni yangu: pale kwenye kampuni kuna watu wamefanya kazi muda mrefu sana. Ulizia kwa wafanyakazi mtu anayeijua sana kampuni. Chagua kama watu watano wa namna hiyo. Waulize njia muafaka za kufanya ili kampuni ipae, iwe juu kwa kufanya vizuri, kwa kufanya maajabu, isipate hasara. Utapata majibu ambayo washauri wabobezi kutoka popote hawawezi kukuambia. Linganisha majibu ya hao watu, ili uyaondoe ya watu woga na yasiyofaa. Ubaki na majibu mazito ya mtu makini asiye mwoga na ni mkweli. Utapata majibu bora na mazuri. Hapo kampuni itapaa kwa kutumia elimu pevu ya pale pale bila gharama kubwa. Halafu unaweza kuwatuza watu hao kwa njia unazozijua. Fimbo ya mbali haiui nyoka.