Serikali ya kijiji CCM yahamia Chadema
Na Anceth Nyahore
15th September 2010
Yumo Mwenyekiti na wajumbe wake sita
Hivi ukiwa CCM unakuwa huna akili? madhalani Abbasi Mtemvu alikuwa upinzani alikuwa ana akili ashakum si matusi... sasa hivi yupo CCM hana akili? mie mbona sielewi inakuwajekuwaje?All i can see ni kwamba watu wa kijiji hicho wana akili sana!
Serikali ya kijiji CCM yahamia Chadema
Na Anceth Nyahore
15th September 2010
Yumo Mwenyekiti na wajumbe wake sita
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mwabagimu, Kata ya Bukundi, Wilaya ya Meatu, mkoani Shinyanga, amekihama chama chake na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mwenyekiti huyo, Kitungulu Gwandi, alichukua hatua hiyo siku chache baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willibroad Slaa, kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.
Aliihama CCM Septemba 10, mwaka huu na kukabidhi kadi yake yenye namba 206803 na kupewa kadi ya Chadema yenye namba CDM 0296155 na uongozi wa chama chake kipya wilayani Meatu.
Gwandi pia amesomba wajumbe sita wa serikali ya kijiji hicho waliokuwa wanachama wa CCM ambao pia waliamua kujiunga na Chadema.
Kuondoka kwa kiongozi huyo wa ngazi ya serikali ya kijiji na baadhi ya wajumbe wake, kumesababisha kijiji hicho kutokuwa na uongozi na hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kulazimika kutangaza uchaguzi mdogo ndani ya kipindi kifupi tangu kufanyika kwa chaguzi za serikali za mitaa nchini.
Wakati hayo yakitokea, Chadema yenyewe wilayani Meatu imetamba kuwa hizo ni cheche za mikutano ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho muda mfupi baada ya kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Fumbuka Manunda, ambaye aliwekwa kando na CCM kwenye uteuzi wa kura za maoni.
Manunda alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea kiti cha udiwani katika Kata ya Bukundi kwa tiketi ya chama hicho, lakini alienguliwa pamoja na aliyekuwa diwani wa kata hiyo aliyeongoza katika kura za maoni na kuchukuliwa mshindi wa tatu, Baby Simon.
Akitangaza kujiengua CCM, Manunda alisema huo ni mwanzo tu kwa baadhi ya wanachama ambao hawaridhiki na mwenendo ndani ya chama hicho na kwamba wapo wengi wakiwemo wenyeviti wa vitongoji kadhaa katika baadhi ya vijiji vinne vya kata hiyo wanaojiandaa kukihama pia.
Gwandi ni mwenyekiti wa pili kuihama CCM na kujiunga na vyama vya upinzani. Hivi karibuni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mshikamano wilayani Meatu, Joshua Kalondos, alijiengua na kujiunga na Chama cha United Democratic (UDP).
Katika mikutano yake ya kampeni kwenye viwanja vya Chini ya Mti Kata ya Bukundi, Dk. Slaa aliwaomba wananchi kufanya mabadiliko na wasidanganyike ili wajiletee maendeleo haraka iwapo tu wataichagua Chadema ikililinganishwa na CCM.
CHANZO: NIPASHE
Hivi ukiwa CCM unakuwa huna akili? madhalani Abbasi Mtemvu alikuwa upinzani alikuwa ana akili ashakum si matusi... sasa hivi yupo CCM hana akili? mie mbona sielewi inakuwajekuwaje?
Tatizo njaa mjomba.
Bora hata Mtenvu. Unamkumbuka mzee wa propaganda?
Alipokuwa CUF alifika mbali kiasi cha kuapa heri kufanya 'nanihii' na mama yake mzazi kuliko kurudi CCM? Leo yuko CCM. Hapo inakuwajekuwaje mjomba?
sasa unamuona Mrema ana akili?........akili zikiisha ndo unarudi ccm!Hata Mrema aliapa hatatoka CCM kaka leo hii anatafuta mlango wa kurudia hauoni
Hivi ukiwa CCM unakuwa huna akili? madhalani Abbasi Mtemvu alikuwa upinzani alikuwa ana akili ashakum si matusi... sasa hivi yupo CCM hana akili? mie mbona sielewi inakuwajekuwaje?
Ukiwa CCM huna haki ya kuongea mpaka unayotaka kuongea yahakikiwe na viongozi katika kulinda maslahi ya chama,wanaumia kimoyomoyo huku wakiwa hawana la kufanya na kujikuta wanakuwa WANAFIKI zaidi ya walivyokuwaHivi ukiwa CCM unakuwa huna akili? madhalani Abbasi Mtemvu alikuwa upinzani alikuwa ana akili ashakum si matusi... sasa hivi yupo CCM hana akili? mie mbona sielewi inakuwajekuwaje?
Ukiwa CCM huna haki ya kuongea mpaka unayotaka kuongea yahakikiwe na viongozi katika kulinda maslahi ya chama,wanaumia kimoyomoyo huku wakiwa hawana la kufanya na kujikuta wanakuwa WANAFIKI zaidi ya walivyokuwa
Ukiwa CCM huna haki ya kuongea mpaka unayotaka kuongea yahakikiwe na viongozi katika kulinda maslahi ya chama,wanaumia kimoyomoyo huku wakiwa hawana la kufanya na kujikuta wanakuwa WANAFIKI zaidi ya walivyokuwa
ukiwa ccm unakuwa huna akili coz u can't think outside the box....