Nimeipenda hii... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeipenda hii...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ilulu, Sep 15, 2010.

 1. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali ya kijiji CCM yahamia Chadema

  Na Anceth Nyahore
  15th September 2010


  [​IMG]
  Yumo Mwenyekiti na wajumbe wake sita

  Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mwabagimu, Kata ya Bukundi, Wilaya ya Meatu, mkoani Shinyanga, amekihama chama chake na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

  Mwenyekiti huyo, Kitungulu Gwandi, alichukua hatua hiyo siku chache baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk. Willibroad Slaa, kuhutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.

  Aliihama CCM Septemba 10, mwaka huu na kukabidhi kadi yake yenye namba 206803 na kupewa kadi ya Chadema yenye namba CDM 0296155 na uongozi wa chama chake kipya wilayani Meatu.
  Gwandi pia amesomba wajumbe sita wa serikali ya kijiji hicho waliokuwa wanachama wa CCM ambao pia waliamua kujiunga na Chadema.

  Kuondoka kwa kiongozi huyo wa ngazi ya serikali ya kijiji na baadhi ya wajumbe wake, kumesababisha kijiji hicho kutokuwa na uongozi na hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kulazimika kutangaza uchaguzi mdogo ndani ya kipindi kifupi tangu kufanyika kwa chaguzi za serikali za mitaa nchini.

  Wakati hayo yakitokea, Chadema yenyewe wilayani Meatu imetamba kuwa hizo ni cheche za mikutano ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho muda mfupi baada ya kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Fumbuka Manunda, ambaye aliwekwa kando na CCM kwenye uteuzi wa kura za maoni.

  Manunda alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea kiti cha udiwani katika Kata ya Bukundi kwa tiketi ya chama hicho, lakini alienguliwa pamoja na aliyekuwa diwani wa kata hiyo aliyeongoza katika kura za maoni na kuchukuliwa mshindi wa tatu, Baby Simon.

  Akitangaza kujiengua CCM, Manunda alisema huo ni mwanzo tu kwa baadhi ya wanachama ambao hawaridhiki na mwenendo ndani ya chama hicho na kwamba wapo wengi wakiwemo wenyeviti wa vitongoji kadhaa katika baadhi ya vijiji vinne vya kata hiyo wanaojiandaa kukihama pia.

  Gwandi ni mwenyekiti wa pili kuihama CCM na kujiunga na vyama vya upinzani. Hivi karibuni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mshikamano wilayani Meatu, Joshua Kalondos, alijiengua na kujiunga na Chama cha United Democratic (UDP).

  Katika mikutano yake ya kampeni kwenye viwanja vya Chini ya Mti Kata ya Bukundi, Dk. Slaa aliwaomba wananchi kufanya mabadiliko na wasidanganyike ili wajiletee maendeleo haraka iwapo tu wataichagua Chadema ikililinganishwa na CCM.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. k

  karisti Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado! tusubirie makubwa zaidi hapo siku za usoni,
  wananchi wamechoshwa na ubabe na ufisadi wa SISI EM.
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,840
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Incredible still watu wanasema wapinzani hawajafika vijijini wakati kijiji kizima kinahamia upinzani kwa siku moja huu mwaka kama wakitoka tunawasachi.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  All i can see ni kwamba watu wa kijiji hicho wana akili sana!
   
 5. Davis

  Davis Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Namuunga mkono PakaJimmy, hao watu wameonyesha ukomavu wa kisiasa.
   
 6. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Umeipenda kwakuwa wamehamia Chadema?
   
 7. comp

  comp Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people
  all the time.......
  So now we see the light, We gonna stand up for our rights!.. ha ha ha... bob marley huyo, way back. wananchi ndo hivyo tena, wameshasema `enough is enough` jamani
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi ukiwa CCM unakuwa huna akili? madhalani Abbasi Mtemvu alikuwa upinzani alikuwa ana akili ashakum si matusi... sasa hivi yupo CCM hana akili? mie mbona sielewi inakuwajekuwaje?
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Hiyo imetulia kama biriani ya Eid El Fitr...............

  Hizo ni rasharasha tu........................
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Tatizo njaa mjomba.

  Bora hata Mtenvu. Unamkumbuka mzee wa propaganda?

  Alipokuwa CUF alifika mbali kiasi cha kuapa heri kufanya 'nanihii' na mama yake mzazi kuliko kurudi CCM? Leo yuko CCM. Hapo inakuwajekuwaje mjomba?
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hata Mrema aliapa hatatoka CCM kaka leo hii anatafuta mlango wa kurudia hauoni
   
 12. D

  Dick JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengine watoka Chadema na kuhamia CCM, nayo tuisemeje?
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  sasa unamuona Mrema ana akili?........akili zikiisha ndo unarudi ccm!
   
 14. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,469
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  sukari itashuka kwa jmk punguzeni spidi uchaguzi usije uka......................
   
 15. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ukiwa ccm unakuwa huna akili coz u can't think outside the box....
   
 16. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ukiwa CCM huna haki ya kuongea mpaka unayotaka kuongea yahakikiwe na viongozi katika kulinda maslahi ya chama,wanaumia kimoyomoyo huku wakiwa hawana la kufanya na kujikuta wanakuwa WANAFIKI zaidi ya walivyokuwa
   
 17. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Thank u Joseph
  Nafikiri wewe....., nasema wewe kwakuwa umeona mbali zaidi ya wengine. Hapo umenena kitu kizuri na kikubwa bila kujijua. Infact hapo ndipo kilipo kiini cha ubadhilifu wa hawa watu. Kulinda maslai ya chama zaidi kuliko uhuru na haki za raia wake. Ndio maana wanathamini sana chama (katiba ya Chama, Ilani ya chama, Sera za chama, mahitaji ya chama tena kwa faida ya wachache) bila hata kujali taifa kama taifa lina changamoto gani na linahitaji nini katika wakati husika.

  Ndio maana huwezi kukuta sehemu yoyote ile inayoainisha uwezo binafsi wa mgombea wa CCM katika kupambana na kero za wananchi.

  Ikumbukwe chama, au sera za chama bila ya uwepo wa watu shupavu na makini, hakiwezi kufanikisha jambo lolote hata kama kingekuwa na sera zilizojitosheleza 100 kwa 100.

  Moral;
  ....We first believe in our individual abilities toward changes, then we keep our trust in the means that can make us attain that changes we want.....
   
 18. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wengi wako CCM kisare (kijani/njano) lakini mioyo yao iko upinzani.
   
 19. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Do u mean kina Mkapa, Mzee Mwinyi, Maprof wote waliopo CCM ni mapoyoyo? mie nadhani kina Mziray na kina Slaa ndio wanastahiki kuwa kwenye hilo fungu wanadhani kuendesha nchi ni kama kuendesha familia. Kwa Chadema kuongoza nchi ni kama vile kuukumbatia mbuyu tena ule wa toure drive
   
Loading...