malundatz255
Member
- Jan 24, 2017
- 49
- 31
Kwanza kabisa poleni kwa majukumu wakuu naomba niende moja kwa moja kwa moja kwenye mada... Naombeni ushauri wenu ndugu zangu kuhusu hili swala lililonitokea jana tarehe 23 march ili nijuwe nini cha kufanya kupata haki yangu. Ishu nzima ipo hivi me nina line yangu ya voda ambayo huwa naitumia kwaajili ya mpesa tu kwani huwa siitumii kuwasiliana na watu kutumia hyo line. Sasa nimekuwa nikiweka na kutoa pesa kwenye hiyo line kwaajili ya biashara zangu ambazo nafanya na kwa mara zote huwa nafahamu kuwa kwenye mpesa yangu kuna kiasi fulani na hiyo line nakuwaga nayo mwenyewe mda wote namaanisha masaa yote... sasa baada ya kufanya muamala wangu wa mwisho juzi tarehe 23 march mida saa 2 usiku nikiwa nyumbani Kwenye mpesa yangu kulikuwa na salio kama Tsh678000 kitu cha kushangaza jana nikawa nimeweka Tsh100000 tena kwenye hiyo line kama kawaida lazima nitumiwe meseji kuwa salio langu jipya ni kiasi fulani ila kitu cha kushangaza baada ya salio langu liwe Tsh778000 nimekuta Tsh378000 kumaanisha kuwa Tsh400000 imepunguwa kama kawaida nikaamuwa niwapigie simu ili nifahamu nini kimetokea baada ya kuwapigia wakaniambia kuwa pesa imetolewa jana mida ya saa 3 asubuh kwa wakala fulani wakanitajia jina la huyo wakala nikawa nimewaomba wanitajie mahali anapopatikana huyo wakala ili nipime ukweli wa hiyo taarifa yao wakawa wamegoma kunipa hyo taarifa na wakaniambia kuwa niende voda ili nikaonane nao.
Sasa kuna maswali ambayo najiuliza kuhusu hili swala ...
1. Je kuna uwezekano wa mtu kutowa pesa kwenye simu ya mwingine bila kuwa na line husika au simu husika.
2. Mtu anawezaje kutowa pesa bila kuwa namba yangu ya siri ambayo ni siri yangu mwenyewe.
Naombeni msaada wenu ili nijuwe ni nini cha kufanya kabla sijaenda kuonana nao.