Nimeibiwa Cards za Bank

Nimeibiwa Cards za Bank

Hvi mtu anaweza kuchukua fedha kwa ATM bila kujua No yako ya Siri? Manake me no yangu ya Siri hata ujaribu Mara 100 huwezi patia.
 
Heshima kwenu wakuu,

Me Mtanzania mwenzenu nimepatwa na janga la aina yake! Kwa hapa nilipo, nipo nje ya nchi, wakati naondoka nilimwacha wife nyumbani, baada ya kukaa kdg kwa kua wife ni mjamzito alienda nyumbani kwetu. Pale home kulibaki mama mwenye nyumba na wapangaji wenzangu, so week tatu sasa yapita wezi waliingia wakabeba vitu kama Radio, Tv, Home theater n.k. ila basi wapangaji wenzangu wakampa taarifa wife na wife akanijuza mimi.

Sasa cha ajabu ni nini, nimepigiwa simu leo wife anadai ATM Cards hazioni pale tuwekapo na zoote ni zangu mie. Nipo nimeshindwa nifanyaje kwani nahis ziliibwa pia, naogopa kama n nitakuta hamna kitu kwenye akaunti zangu na wakati huu mgumu.

Nisaidieni nifanyaje jamani

Toa taarifa polisi kwanza, then peleka RB kwa benki, watakupa majibu yako yote ikiwa ni pamoja na kupewa kadi nyingine mpya...!
 
Lijitu na sharubu zake nyingi tuu linakalisha kalio chini na kupost story za uongo.
 
Hvi mtu anaweza kuchukua fedha kwa ATM bila kujua No yako ya Siri? Manake me no yangu ya Siri hata ujaribu Mara 100 huwezi patia.

Ni kweli mkuu ila kwa card yangu ni kama nilikosea kwani sikuweza badiri mumber za siri zaidi ya ile ya mwanzo ambayo ni mwaka wa kuzaliwa mimi na kinachonipa shaka ni uwizi kufanyika baada ya mimi na wife kutokuwepo hii inanifanya nihisi ni mtu anae nijua murua kwamba mimi ni nani lakini sio tabu me nipo nakuja kesho asubuhi nitakua home asnteni kwa ushauri na nyongeza jf
 
Feedback

Wakuu nashukuru sana kwa maoni yenu na mashauri nilifika jana na nilipitia bank NBC nikawapa taarifa baada ya mda kidogo zikaletwa card zile zinazo mezwa na Atm na yangu ikitolewa maelezo kwamba alikuja mdada wa kati ya miaka 28 to 30 alikua anataka kutoa pesa kwa cachier lakini alikataliwa na baada ya siku mbili alikuja tena kijana wa kati ya miaka 16 to 20 lakini alipofika kwa cashier alijieleza kama ametumwa na mwenye card lakini wafanyakazi wakamtilia shaka na kumuuliza kwanini hakuenda kutolea kwa Atm mashine? Akasema amesahau password wakamwambia aende kumwita mwenye card basi kijana mpaka kesho hakuwahi kuonekana

kwa ile ya crdb mpaka sasa ipo kwenye taratibu ya kunitengezea mpya na masalio yapo salama asanteni
 
Hofu yako ilikuwa bure tu. ATM card inapotumika kwenye mashine ikakosewa PIN no. mara 2 au 3 kadi inavutwa ndani ya mashine. Ili kuipata inabidi uiombe urudishiwe kwenye tawi la benki ulikofungulia acc. (CRDB) au makao makuu ya benki au main branch ya benki husika.
 
and anyway,pia unaweza wapigia simu kuwaambia card imeibiwa wafunge matumizi ya kadi mara moja,wanaweza kukusaidia pia...pole
 
Back
Top Bottom