Nimehudu TANESCO miaka nane bila kuajiriwa

MtanzaniaMzalendo

New Member
Dec 25, 2015
1
0
Katibu Mkuu Wizara Ya Kazi Na Ajira
S.L.B. Dar es Salaam, Tanzania
KK
Katibu Mkuu Kiongozi,
KK
Katibu Mkuu Nishati na Madini
Habari za kazi Mh.Katibu/Kamishna mkuu wizara ya kazi
Mimi ni kijana wa miaka 28,niliehitimu masomo yangu chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka 10 iliyopita. Nilipata kuhudumu katika shirika la umeme Tanesco kwa miaka 8 bila kuajiriwa (STE) lakini kwa sasa nimefukuzwa bila sababu za msingi, lakini pamoja na kwamba nimefukuzwa lakini naamini ninayo fursa ya kukueleza mabaya yaliyo ndani ya Tanesco hasa katika ngazi za chini, kwa bahati mbaya sitaongelea mazuri kwani kwa miaka nane niliyohudumu kama STE (KIBARUA) mabaya yalikuwa mengi na yaliyafunika mazuri yote niliyokutanana nayo,
1)Vibarua wananyanyasika sana na mbaya zaidi malipo yao ni madogo sana kiasi kwamba watu wanafanyia kula na nauli tu.
2)Watu wanafanya kazi miaka 10 bila kuajiriwa bali huhudumu kama vibarua tu,mimi sipo tena ndani ya shirika lakini naamini watu waliohudumu ndani iya shirika kwa miaka 5, walipaswa kuajiriwa kwa namna yeyote ile, nachelewa kuamini kama watu zaidi ya 20 walotoka katika chuo kikuu cha DSM,DIT nk. katika fani mbalimbali wanaweza kuachwa na wasipewe ajira na wakawa vibarua kwa muda wa miaka 8, halafu wakaajiriwa watu wengine kutoka katika vyuo kama hivo au vingine na wakawa juu ya wale waliohudumu kwa miaka mingi bila kuajiriwa huku ikiwa waloajiriwa wana uzoefu kiduchu au hawana kabisa na mbaya zaidi wanafundishwa kazi na wale vibarua (STE), hapa sina ushahidi lakini akili yangu ya kuzaliwa inatosha kunusa harufu ya rushwa, kujuana na upendeleo katika sekta ya ajira, nina mifano ya wazi na ninaweza kuwataja watu ,kwa majina na muda waloingia kazini na watu walowaingiza kazini,na pia vituo vyao vya kazi ila nitakuwa sikuwatendea haki kwani walotunyima haki si waloletwa bali walowaleta. Na hapa kuna udhaifu katika sekta yote yarasilimali watu,
Madhara ya suala hili ni makubwa katika utendaji wa shirika, kwani vibarua ndiyo watendaji wakubwa katika operation za miradi mipya, ya zamani na huduma za siku hadi siku, hawa ndiyo hupokea malamimiko ya wateja, ndiyo hukutana na wateja katika shughuli za ugani ( site) na kwa kuwa hawa wana malipo madogo, wanakuwa arahisi kulihujumu taifa, pia watu hawa hawaijui kesho yao hivyo ni ngumu kuwekeza katika dhima (Vision) ya kampuni, mwisho ni rahisi wale wasio waaminifu kurubuniwa na wateja wasiolitakia mema taifa letu.
Rejea vijana walofukuwa hivi karibuni Tanesco ILALA, wote wamehudumu kwa takribani miaka 5.
Rejea Idara ya Rasilimali watu ILALA inayoongozwa na akina mama wawili hawa ni vinara wa unyanyasaji wa vibarua, kushawishi vibarua kupewa mkataba wa miezi 6,na pia kuwaingiza watu bila kufuata utaratibu.
Rejea Meneja aliyehamishwa toka Kigamboni na kuhamishiwa Viwandani, jinsi anavyonyanyasa vibarua na kuwafukuza bila hata uchunguzi kwa taarifa za makosa yao yanayoripotiwa,
Nilipata kuhudumu Tanesco Kurasini,viwandani, Ilala na baadae Mbagala haya ninayosema nayajua vema.
Mheshimiwa nina imani na watendaji wako wizarani, na pia nina matumaini mapya na shirika hili la Tanesco japo kwa maisha yangu ya kila siku,familia yangu na uhai wa taifa hili katika kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati na nchi ya viwanda, lakini nina wasiwasi kwani wanaopaswa kutufikisha huko ni watu sahihi wenye fikra sahihi na waliojengwa katika misingi ya usawa na uwezo wa kutazama kesho ya
taifa letu hivyo ninaomba, ulitazame hili kwa yakini ili hawa watanzania wasiendelee kuwa utumwani katika nchi yao,
Na hawa wanaopoka haki za watanzania wasomi watizamwe kwa jicho la tatu la kimaendeleo na usawa unaotembea juu ya haki,
Kwa maendeleo ya Taifa letu nina imani utachukua hatua ili kuifikia dhima ya kuwa taifa la viwanda.
Pia niombe radhi kama sera ya kuhudumu kama kibarua kwa miaka 5 au zaidi ni sera au mwongozo wa shirika toka wizarani nami nitakuwa nimeenda kinyume na mwongozo wa wizara hapo napaswa kuomba radhi .
Akhsanten
 
Una miaka 28 na umehitimu chuo kikuu miaka10 uliopita ni kweli ulimaliza chuo ukiwa na miaka 18 kihesabu mbona haiji mbona inamaana ulianza shule ya msingi ukiwa una miaka 4 au 5
 
Inawezekana sana tena sana, meaning yako std 2 na anamiaka 6 Leo. Namshukuru mungu she is very bright. Sasa piga mahesabu yako
 
Vibarua (STE) kwa kawaida hufanya kazi kwa mkataba maalumu; sasa hiyo ajira unayong'ang'ani ni Ipi? Umemaliza chuo kikuu alafu unachimba mashimo?
 
Inawezekana sana tena sana, meaning yako std 2 na anamiaka 6 Leo. Namshukuru mungu she is very bright. Sasa piga mahesabu yako
Labda unataka tubishane tu aisee, kwa Tanzania kumaliza chuo kikuu kwa miaka 18 sidhani
 
Katibu Mkuu Wizara Ya Kazi Na Ajira
S.L.B. Dar es Salaam, Tanzania
KK
Katibu Mkuu Kiongozi,
KK
Katibu Mkuu Nishati na Madini
Habari za kazi Mh.Katibu/Kamishna mkuu wizara ya kazi
Mimi ni kijana wa miaka 28,niliehitimu masomo yangu chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka 10 iliyopita. Nilipata kuhudumu katika shirika la umeme Tanesco kwa miaka 8 bila kuajiriwa (STE) lakini kwa sasa nimefukuzwa bila sababu za msingi, lakini pamoja na kwamba nimefukuzwa lakini naamini ninayo fursa ya kukueleza mabaya yaliyo ndani ya Tanesco hasa katika ngazi za chini, kwa bahati mbaya sitaongelea mazuri kwani kwa miaka nane niliyohudumu kama STE (KIBARUA) mabaya yalikuwa mengi na yaliyafunika mazuri yote niliyokutanana nayo,
1)Vibarua wananyanyasika sana na mbaya zaidi malipo yao ni madogo sana kiasi kwamba watu wanafanyia kula na nauli tu.
2)Watu wanafanya kazi miaka 10 bila kuajiriwa bali huhudumu kama vibarua tu,mimi sipo tena ndani ya shirika lakini naamini watu waliohudumu ndani iya shirika kwa miaka 5, walipaswa kuajiriwa kwa namna yeyote ile, nachelewa kuamini kama watu zaidi ya 20 walotoka katika chuo kikuu cha DSM,DIT nk. katika fani mbalimbali wanaweza kuachwa na wasipewe ajira na wakawa vibarua kwa muda wa miaka 8, halafu wakaajiriwa watu wengine kutoka katika vyuo kama hivo au vingine na wakawa juu ya wale waliohudumu kwa miaka mingi bila kuajiriwa huku ikiwa waloajiriwa wana uzoefu kiduchu au hawana kabisa na mbaya zaidi wanafundishwa kazi na wale vibarua (STE), hapa sina ushahidi lakini akili yangu ya kuzaliwa inatosha kunusa harufu ya rushwa, kujuana na upendeleo katika sekta ya ajira, nina mifano ya wazi na ninaweza kuwataja watu ,kwa majina na muda waloingia kazini na watu walowaingiza kazini,na pia vituo vyao vya kazi ila nitakuwa sikuwatendea haki kwani walotunyima haki si waloletwa bali walowaleta. Na hapa kuna udhaifu katika sekta yote yarasilimali watu,
Madhara ya suala hili ni makubwa katika utendaji wa shirika, kwani vibarua ndiyo watendaji wakubwa katika operation za miradi mipya, ya zamani na huduma za siku hadi siku, hawa ndiyo hupokea malamimiko ya wateja, ndiyo hukutana na wateja katika shughuli za ugani ( site) na kwa kuwa hawa wana malipo madogo, wanakuwa arahisi kulihujumu taifa, pia watu hawa hawaijui kesho yao hivyo ni ngumu kuwekeza katika dhima (Vision) ya kampuni, mwisho ni rahisi wale wasio waaminifu kurubuniwa na wateja wasiolitakia mema taifa letu.
Rejea vijana walofukuwa hivi karibuni Tanesco ILALA, wote wamehudumu kwa takribani miaka 5.
Rejea Idara ya Rasilimali watu ILALA inayoongozwa na akina mama wawili hawa ni vinara wa unyanyasaji wa vibarua, kushawishi vibarua kupewa mkataba wa miezi 6,na pia kuwaingiza watu bila kufuata utaratibu.
Rejea Meneja aliyehamishwa toka Kigamboni na kuhamishiwa Viwandani, jinsi anavyonyanyasa vibarua na kuwafukuza bila hata uchunguzi kwa taarifa za makosa yao yanayoripotiwa,
Nilipata kuhudumu Tanesco Kurasini,viwandani, Ilala na baadae Mbagala haya ninayosema nayajua vema.
Mheshimiwa nina imani na watendaji wako wizarani, na pia nina matumaini mapya na shirika hili la Tanesco japo kwa maisha yangu ya kila siku,familia yangu na uhai wa taifa hili katika kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati na nchi ya viwanda, lakini nina wasiwasi kwani wanaopaswa kutufikisha huko ni watu sahihi wenye fikra sahihi na waliojengwa katika misingi ya usawa na uwezo wa kutazama kesho ya
taifa letu hivyo ninaomba, ulitazame hili kwa yakini ili hawa watanzania wasiendelee kuwa utumwani katika nchi yao,
Na hawa wanaopoka haki za watanzania wasomi watizamwe kwa jicho la tatu la kimaendeleo na usawa unaotembea juu ya haki,
Kwa maendeleo ya Taifa letu nina imani utachukua hatua ili kuifikia dhima ya kuwa taifa la viwanda.
Pia niombe radhi kama sera ya kuhudumu kama kibarua kwa miaka 5 au zaidi ni sera au mwongozo wa shirika toka wizarani nami nitakuwa nimeenda kinyume na mwongozo wa wizara hapo napaswa kuomba radhi .
Akhsanten

Pole sana mkuu.natumaini siku za hao wanyanyasaji zinahesabika

Nimeona humu wengine wanakudhihaki .hao nao ni wale wale wasiojua kitu. Unachosema uko sahihi sana .nami nina ndugu wa karibu anamaumivu kama yako.nakubaliana 100% .hapo Tanesco bado kuna vimungu watu
 
Back
Top Bottom