Mulimila dole
JF-Expert Member
- Jul 15, 2016
- 226
- 266
Habari zenu wanajamii,
Kuna binti mmoja wa kidato cha 3 ameachishwa shule kwa kukosa ada. Ni kweli wapo wengi ambao hushindwa kuendelea na shule kwa sababu mbalimbali lakini kilichonigusa ni jinsi huyu binti alivyoanza shule na kuishia njiani.
Huyu binti alitolewa kwao Tanga kuja hapa Dar kama mfanyakazi za ndani lakini kwa huruma ya yule baba wa familia aliona amsomeshe elimu ya sekondari hivyo kamtafutia shule moja wapo ya sekondari iliyopo hapa Dar Wilaya ya Ilala.
Akiwa kidato cha pili mwaka jana yule baba alifariki Dunia na kumwacha huyu binti akiwa na mama mwenye mji ambaye anadai kuwa hana uwezo tena wa kumsomesha hivyo hata ada ilisimama. Mmiliki wa shule nae alivumilia mwaka mzima bila ada lakini mwaka huu aliamua kumfukuza shule kwani haoni dalili za kupata malipo ya ada tena kutoka kwa huyo binti.
Mbaya zaidi baada ya mimi binafsi kuguswa na kutaka kuona namna ambavyo ningeweza kumsaidia baada ya kusikia habari hizo niliongea na Mwalimu wake nae akanipa namba ya simu ya huyo mama (Bosi wake).
Huyo mama anadai kuwa ni kweli hana tena uwezo wa kumsomesha hivyo anatafuta nauli amrejeshe kwao Tanga. Huyu binti anasoma na mwanangu darasa moja yeye ndiye alianza kunipa masaibu ya binti huyu na jinsi ambavyo alikuwa akilia siku zote kwa kuona dalili za kuikosa elimu ya sekondari.
Najaribu kujiuliza umasikini wa mama yake mzazi kule Tanga ndicho kiini cha kuja Dar kutafuta kazi za ndani, je akirudi kwao si ndio utakuwa mwisho wa kusoma? Kwa taarifa nilizo nazo toka kwa Mwalimu wake wa darasa huyu binti anafanya vizuri sana darasani licha ya changamoto alizonazo.
Binafsi kama ningekuwa na uwezo wa kumlipia ada ningefanya hivyo ila uwezo wangu kiuchumi sio mzuri sana wa kuweza kuubeba huo mzigo peke yangu.
MAOMBI
(1)Kama kuna Mwanajamii ambaye anajua ni wapi au kwa nani huyu binti anaweza kusaidiwa ajitokeze kwani itakuwa tumeokoa yeye na uzao wake.
(2) Kama kuna mtu mwenye shule yake ya sekondari au Kituo cha elimu (Education center ) atajitolea kumsomesha bure au kwa namna yoyote ile utakuwa msaada mkubwa kwake.
(3) Kama kuna mwana jamii ambaye anawazo mbadala litakalomwezesha huyu binti kuendelea na masomo nitashukuru pia.
Nakaribisha maoni pia nisingependa maoni ya kumkejeli huyu binti.
Nawasilisha
Kwa maoni na ushauri nitafute 0656136607