Nimedukua simu ya mke wangu, Simu zetu zina siri nzito, nakufa mimi

kuna application unadownload tu, kama unatumia android au ios, zinaweza kukuletea sms zote, call logs, zingine zinarecord mpaka calls unaweza kuskiliza baadaye, inakupa geolocation ya simu kwa wakati husika, unaweza kuwasha microphone ya simu yake hata kama ameiweka mezani ukaskiliza maongezi yanayoongewa offline bila yeye kujua, unaweza kuwasha camera ukaona kila kitu, unaweza kuangalia picha alizopiga, unaweza kukamata login details za kwenye mitandao ya kijamii na sehem zingine, kiufupi simu yake unakuwa na access nayo wakati wowote inapokuwa on bila yeye kujua, na hiyo application wala haionekani ukishaiweka inapotea kabsa!
Inaitwaje mkuu hiyo aplication?
 
At least now i get the story
Kumbe ndivo ilivyoishia

Kwanza pole, pili nakushaur ku delete mawazo ya mapenzi anza fikra mpya za kuwa bilionea au kuwa na akili nyingi..jitahidi kupenda vikongwe na watoto na wanyama hilo litakusaidia mno.. na litakusahalisha mengi... Soma sana vitu vya kujiendeleza kiakili au uchumi... Hakikisha unakuwa mshaur mzur kwa kila mtu..na popote pale kwa kufanya hivyo utapata furaha na aman ya milele....
Ni hayo tu
 
**********-**************&
u have a point mkuu ila kuhusu hili nakiona kifo kama part of my life currently yani sijisikii woga sijui kwa nn...
aniue sawa

Wewe ni wa thamani sana usijichukie hivyo,jipende,naelewa sana jinsi gani ambavyo umeumia ni maumivu makali mno na umeona dunia si kitu tena kwako,maisha hayana thamani tena kwako pamoja na haya yote jua bado Mungu anakupenda,anakuthamini sana na anakuhitaji uwe ni mwalimu bora kwa wengine,kupitia hili na wengine wapone. Wewe ni wa thamani sana machoni pa Bwana,fanya ibada Mungu ndiye faraja ya kweli,upendo wake umekuzunguka,yeye asiyemwangusha amchaye jifungamanishe na yeye tu,Neema yake yakutosha,usitafute amani kwa wanadamu wataendelea kukuumiza tu.

Kuna kitu nataka nikwambie mahali ulipokosea,samahani kidogo kama nitakukwaza mpendwa . Umefunguka vizuri sana jinsi gani ulivyokuwa unaishi na mkeo,kweli mlikuwa na upendo wa hali ya juu hamna mfano,yeye kuchukua simu yako na ww kuchukua simu yake kisha kila mtu anaenda kwenye shughuli zake pasipo shaka yoyote si jambo la kawaida,mkapeana na password zenu za kila mahali ulikuwa ni uaminifu wa hali ya juu.

Katika safari yenu hiyo ya amani,upendo na uaminifu wa hali ya juu wewe ukaweka mashaka ati hapana hii safari siyo embu nijaribu kujiridhisha kidogo kama ndo yenyewe,tatizo umeliumba mwenyewe,Biblia inasema mtu atakula matunda ya midomo yake mwenyewe,uliweka mashaka hatimaye umevuna matokeo ya mashaka yako,umepanda wazo ovu umevuna uovu.

Jinsi ulivyokuwa unaishi kwa upendo na mkeo kitendo cha kuweka hiyo program kwenye simu yako wakati mkeo ni mwaminifu kwako tayari spiritual iliumba kitu fulani,wewe mwenyewe uliumba hicho kitu na hatimaye kimekutokea kweli,kulikuwa hamna haja ya kuweka hiyo app kwa mtu ambaye hakuwa na dalili hata moja ya kukosa uaminifu.Kusitasita si kuzuri hata Mungu mwenyewe anasema anachukia mtu mwenye nia mbili na anasema mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisitasita roho yangu haina furaha naye.

Mkeo ni mke mwema kabisa,ila wewe mwenyewe uliumba kitu kwake na hatimaye kimekuwa kweli,umempa nafasi shetani wewe mwenyewe kuivuruga ndoa yako,sasa basi limeshatokea samehe yote,Msamehe mkeo,samehe jirani,jisamehe na wewe mwenyewe,anayetafutwa kuangamizwa na shetan si jirani bali ni wewe mwenyewe na kizazi chako,ndo maana umefika mahali umejichoka huoni tena thamani ya kuishi,mke tena naye haoni thamani ya kuishi pasipo wewe fikiri nini kitafuata kwa mwanao?

Hapa si mwisho wa maisha,maisha yanabidi yaendelee,una nafasi ya kuinuka tena,WEWE NI WA THAMANI SANA,una uwezo wa kuijenga ndoa yako tena na ikawa bora zaidi ya mwanzo,inuka kijana tusonge mbele,ni wakati wa kumwambia adui yako kwamba ninaweza kusimama tena,kung'uta mavumbi tusonge mbele,inabidi tufike nchi ya ahadi yenye maziwa na asali,ni marufuku kuishia jangwani,inuka, inuka you can make it again.Mungu akutie nguvu.
 
Mimi hapa nalilaumu hilo li App tena wala sitaki nilisome mahali popote.
Isingekuwa hiyo App wala usingepata taarifa yoyote juu ya mahusiano ya mkeo na huyo jamaa. Usingemhisi mke wako, usingefuata usiku, usingempiga wala usingemuabisha mkeo mbele za watu.
Hiyo app imekufanya umeweka jeraha kwenye ndoa yenu ambayo hata likipona kovu lake litaendelea kuuma siku likipata baridi maisha yenu yote.
Hiyo App imekufanya umeenda kumvua mama wa watu nguo hadharani.
Isingekuwa hiyo App ungekuta bado unampenda mkeo, unamthamini mkeo na mnafurahiana sawa sawa na mkeo.
Ona sasa hiyo App imewasababisha hampendani tena, hamfurahiani tena, hammisiani tena na baya zaidi nina uhakika miaka michache ijayo mtaachana.
Ulipomuoa huyo mwanamke uliapa kuwa utampenda, lakini sasa haumpendi tena sababu ya hiyo App.
Usikae hata siku moja ukadhani kwamba hilo tukio limemuondolea "ubibadamu" wake huyo mkeo. Binadamu tungekuwa tunakomeshwa na "matukio" ukimwi ungekuwa historia. Mkeo atakuwa anaendeleza ubinadamu wake kama kawaida na hako kamtego ka App ulikomuwekea keshakashtukia. Kubali tu hayo ndiyo maisha ya kawaida ya binadamu na wala usisononeke moyo. Kama unadhani hayakufai basi kaoe malaika...
Mimi naishi maili zaidi ya elfu 10 toka alipo mke wangu kwa sasa... tunapendana, tunafurahiana, tunamisiana na nikipata likizo nikarudi home tunafurahishana kama njiwa. Hii ni kutokana na kwamba mimi sijaweka App kwenye simu yake ingawa ningeweza kufanya hivyo. Na nikirudi nyumbani sishiki simu yake kusoma msg au call log, hata simu yake ikiita hayupo sipokei.
Nafanya hivyo sio kwa sababu simpendi, bali kwa sababu mimi kama binadamu niko 100% responsible kwa furaha ya maisha yangu na sitapenda mtu nimekutana nae ukubwani, hata ukoo nae sina eti akacompromise furaha yangu. Mimi kama binadamu ninayo mapungufu yangu ikiwemo kukosa uaminifu kwa mke wangu, nashukuru hajawahi kufahamu hivyo sijacompromise furaha yake ktk hilo. Najua yeye pia kama binadamu anayo mapungufu yake, na sijui kama la kukosa uaminifu ni mojawapo na kamwe SITAKI nifahamu hilo kwani nathamini sana furaha yangu na ya familia yangu...
 
kuna application unadownload tu, kama unatumia android au ios, zinaweza kukuletea sms zote, call logs, zingine zinarecord mpaka calls unaweza kuskiliza baadaye, inakupa geolocation ya simu kwa wakati husika, unaweza kuwasha microphone ya simu yake hata kama ameiweka mezani ukaskiliza maongezi yanayoongewa offline bila yeye kujua, unaweza kuwasha camera ukaona kila kitu, unaweza kuangalia picha alizopiga, unaweza kukamata login details za kwenye mitandao ya kijamii na sehem zingine, kiufupi simu yake unakuwa na access nayo wakati wowote inapokuwa on bila yeye kujua, na hiyo application wala haionekani ukishaiweka inapotea kabsa!

Wawwww nami ngoja nikaiweke kwa wangu inaitwaje? bro
 
*****ENDELEENI****
Kabla sijawaambia nini kilitokea dar, naomba niwape primary indicator za huu usaliti kabla ya kufika hapo tulipofikia.
1. mke wangu alikuwa akimsifia jamaa kwamba ni mpenda mungu hivo ana mungu ndani yake kwa vile mke wangu nae anajihusisha sana na hayo mambo sikupata shaka.

2. kupigiana simu, yani jamaa kwa vile anajua tunaaminiana kama family friends hivo alikuwa anagonga simu mara kwa mara nikiwepo, ila niliwah kuhoj why always simu...nikajibiwa punguza wivu beb hivi kwel naweza tembea na yule m-bab@? ok nikapotezea....kwa hiyo kama una mke wako afu anawasiliana na mtu ukimuuliza akakujib hivi usilidhike na hilo jibu tia nguvu zaidi
3. simu ya mpenzi wako kuwa busy mara kwa mara isivokawaida....kwan mke wangu sawa simu ake inatumika ila ikawa too much busy hivo ukiona nawe wako imeaanza kuwa busy sana unapomtafuta stuka, hii najua ni sababu penzi bado changa hivo mwanaume hutumia muda mwingi kuendelea kumuweka karibu muhanga
4. kupunguzavinterval za kupigiwa simu.
yani mke nilikuwa nimezoea hata kabla sijaamka kwenda kazini ile saa 12 au moja asubuh ashapiga simu na kuniamsha na kunitakia kazi njema ila ikafika hatua anapiga saa 2 mara 3 siku zingine hadi saa 5 asbh ndo akawa ananitafuta
ukiziona dalili hizi jua kuna mabafiliko moyoni mwa mtu si unajua moyo hauwezi kupenda vitu viwli equally kwa wakat mmoja....hivo lazima utaanza kuegemea upande mmoja...hii nayo ni dalili iliyojitokeza in process nikiwa naendelea kumutrack
5. ukimuuliza mke wako endapo simu yake ulilikuwa busy akakujib fresh muulize tena kwa mara nyingine ukikuta ipo busy kama hamna wizi atakujib kimahaba tu na utamuelewa ila ukiona anakujib kiukali yan hapend umuhojihoji ujue anatumia huo ukali kama zana usiendelee kumfuatilia fuatilia masuala yake ya simu aendeleze dhambi zake.
6.ukiona mke wako anamhurumia saana mwanaume fulani apatapo tatizo yani yupo tayari kumsaidia hata fedha za ndani kulitatua tatzo lake ujue anampenda kimapenzi huyo mtu.....hii ilitokea pia katika huu mchakato.
7. jambo la mwisho tendo la ndoa
endapo una mke wako kitandani ukamuomba akakupa lakini utaona hakuenjoy kama kawaida ake....kukupa kila uambapo anakupa ila furaha ya usoni kufurahia tendo inakuwa huioni kama kawaida ake ujue kuna mme mwenzako ndo anafurahiwa kwa muda huo.....

Daaah!! kweli kabisa hizi dalili zilikuwa kwa girlfriend wangu kipindi fulani na kweli alikuwa amepata kababa flan ila nikafanikiwa kuwakomesha..
 
Daaah hili jambo na liwatokee wengine yaani mimi na uhehe wangu huu namfyonza mtu uongo kisha naenda kujinyonga au nakimbilia mbali"''
 
Pole sana ndugu kwa yaliyo kupata, muombe Mungu akupatie moyo wa kusamehe, pamoja ya kuwa hilo suala ni gumu kusamehe jipe moyo. Ningekuwa ni mimi ningekata uume wa huyo mzee ili hasira zangu ziishe.
 
Mimi hapa nalilaumu hilo li App tena wala sitaki nilisome mahali popote.
Isingekuwa hiyo App wala usingepata taarifa yoyote juu ya mahusiano ya mkeo na huyo jamaa. Usingemhisi mke wako, usingefuata usiku, usingempiga wala usingemuabisha mkeo mbele za watu.
Hiyo app imekufanya umeweka jeraha kwenye ndoa yenu ambayo hata likipona kovu lake litaendelea kuuma siku likipata baridi maisha yenu yote.
Hiyo App imekufanya umeenda kumvua mama wa watu nguo hadharani.
Isingekuwa hiyo App ungekuta bado unampenda mkeo, unamthamini mkeo na mnafurahiana sawa sawa na mkeo.
Ona sasa hiyo App imewasababisha hampendani tena, hamfurahiani tena, hammisiani tena na baya zaidi nina uhakika miaka michache ijayo mtaachana.
Ulipomuoa huyo mwanamke uliapa kuwa utampenda, lakini sasa haumpendi tena sababu ya hiyo App.
Usikae hata siku moja ukadhani kwamba hilo tukio limemuondolea "ubibadamu" wake huyo mkeo. Binadamu tungekuwa tunakomeshwa na "matukio" ukimwi ungekuwa historia. Mkeo atakuwa anaendeleza ubinadamu wake kama kawaida na hako kamtego ka App ulikomuwekea keshakashtukia. Kubali tu hayo ndiyo maisha ya kawaida ya binadamu na wala usisononeke moyo. Kama unadhani hayakufai basi kaoe malaika...
Mimi naishi maili zaidi ya elfu 10 toka alipo mke wangu kwa sasa... tunapendana, tunafurahiana, tunamisiana na nikipata likizo nikarudi home tunafurahishana kama njiwa. Hii ni kutokana na kwamba mimi sijaweka App kwenye simu yake ingawa ningeweza kufanya hivyo. Na nikirudi nyumbani sishiki simu yake kusoma msg au call log, hata simu yake ikiita hayupo sipokei.
Nafanya hivyo sio kwa sababu simpendi, bali kwa sababu mimi kama binadamu niko 100% responsible kwa furaha ya maisha yangu na sitapenda mtu nimekutana nae ukubwani, hata ukoo nae sina eti akacompromise furaha yangu. Mimi kama binadamu ninayo mapungufu yangu ikiwemo kukosa uaminifu kwa mke wangu, nashukuru hajawahi kufahamu hivyo sijacompromise furaha yake ktk hilo. Najua yeye pia kama binadamu anayo mapungufu yake, na sijui kama la kukosa uaminifu ni mojawapo na kamwe SITAKI nifahamu hilo kwani nathamini sana furaha yangu na ya familia yangu...

Nimejifunza kitu kipya kwa hii post yako. Thanks mkuu.
 
Lakini jamaa amenilet down bana, amemlegezea mzee mpaka ametimka mbio, hata kushika tak0 tu hajashika?..hajaitendea haki nafsi yake ndiyo maana bado haijasamehe, angempasulia hata yai tu basi nafasi ingeridhika na ikasamehe kabisaa!

Bora tu huyo mdingi alivyotimka, maana hata hivyo hiyo hasira aliyokuwa nayo jamaa na hapo hapo watu wengine 2 wapo pembeni wanaona hiyo scene huyo jogoo angewezaje kuwika jamani, hata hilo yai lingewezaje kupasuka katika mazingira hayo! Mmmh!
 
Iko hiv!
Usimchunguze kabisa mwenza usiye tayari kuachana naye!NEVER!
Ona unavyohangaika maskini!
 
Na nani aliwaambia ndoa inafanya tuache kuwa wanadamu?
Ambao majaribu na kuanguka ni ukamilifu wa maumbile yetu?
Aaaargh!
Umeharibu kiiiiila kitu!
Hukuwahi kusengenya!hukuwahi kutukana?hukiwahi kuacha kutoa zaka!?
Nakuonea huruma maana hii ndoa inakwenda na maji ukiwa unampenda mkeo,ukiwa unamhitaji sana!
Af mbaya zaidi hata kuvunjika kwa ndoa hiyo halitakuwa suluhisho la amani ndani ya moyo wako!
BELIEVE ME YOU!
 
....asante kwa mlioniombea...
nimeota mambo mengi sana usiku wa leo na kikubwa ni God relaleted dreams..
i was takin jf for granted ila nahisi kuna hali isio kawaida siriously...

Hili ni jepesi tu ukiacha uheal kiroho na toka ndani!
Kibinadamu huwezi"
 
Back
Top Bottom