Nimedukua Mawasiliano ya Mke wangu- Weka Mbali na watoto!

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,251
4,638
Habarini za mihangaiko!

Mimi nimeoa yapata miaka 7 iliyopita na tumebarikiwa na mtoto mmoja mpaka sasa.

Mahusiano yetu hayajawa na utelezi japo natambua ni kawaida kuwa na milima na mabonde Ila kuna kiasi. Mimi nimeoa Unyamani-Uzunguni kwa maana hiyo. Toka tunaanza mahusiano wakati huo, mpenzi wangu amekuwa akibadilika taratibu mpaka leo hii hali siyo nzuri kwa kweli.

Mara ya kwanza kuna siku tulitoka out usiku tukaenda kiwanja kimoja kipo karibu na Ubalozi wa Uganda Oysterbay ndo vurugu zilipoanzia. Mimi sinywi pombe, sinywi wine, sivuti aigara kwa kivupi, situmii kilevi chochote kile na haya ni maamuzi yangu lakini pia yanachangiwa na familia yangu. Mzee wangu ni mtumishi wa Mungu (Askofu) so nimelelewa kwenye Biblia zaidi.

Pamoja na msimamo wangu huo, sina shida kabisa mpenzi wangu au mke kupiga gambe kama anaweza kuicontrol ili isiniathiri kwa maana ya kuzaa mengine katika mahusinao. Sasa siku hiyo tupo Mimi, mpenzi wangu na mgeni wetu alikuja kututembelea ndo nilikuwa dereva coz wao watoe wanapiga gambe.

Muda ulivyoenda niligundua mpenzi ameanza kulewa na kule kucheza na mambo mengine niaona tuondoke. Kama dereva nilimsihi mara kadhaa akagoma, nilichokifanya nilimuomba mgeni tuondoke na kweli tuliondoka tukapitia Kona Bar kununua nyama pale moto mpaka home. Tulikuwa tunaishi karibu na Whitesands hotel.

Ile nafika getini nasubiri mlizi anifungulie mpenzi wangu naye akawa amefika na Taxi Ila alipandisha mzuka balaa akaanza kunifokea mara huyo kanirukia, nilichezea vitasa vya hapa na pale matusi nini mbele ya mgeni wangu na mlinzi Ila sikufanya chochote zaidi ya kumdhibiti alafu nikambeba tukaingia ndani tena nikampandisha ghorofani kwa kumbeba.

Kesho yake nikamkalisha kwa maongezi yenye akili sana Ila nikamalizia kwa kusema yeye ndiye aliyeleta ugomvi wa kupigana kwenye mahusiano yeto so asije akalalamika ikitokea huko mbele ya safari. Ni kweli baada ya hapo amewhi tena kuninasa vibao vya hapa na pale na mimi sikumbania kila ilipobidi nilimkumbusha kwa vitasa.

Ishu ya leo iko hivi, baada ya kuingia kwenye ndoa, mke wangu alibadilika japo siyo sana but tumekuwa na ugomvi ambao anauanzisha yeye, siyo mke mwenye kusema anaweza kuongea na wewe kwa heshima. Ni mtu wa kufoka, kutukana na hakuna sekunde unaweza kusema sasa tuna enjoy maisha. Kuna wakati hata kwenye kugegedana katikati anaweza kuanzisha varangati.

Nikawa nimechoka nikapata mchepuka so stress zikiwa nyingi nipo town na mtoto wa kibongo maisha yakawa yanasonga. Ila kwa sasa ni muda tumehamia Unyamwezini long time kidogo ndo kabisaaaaaaaa mambo yameharibika mpaka yeye mwenyewe akaanza kwenda kwa washauri wa ndoa baadae akanishawishi tukawa tunaenda wote.

Juzi kati nilirudi bongo likizo kidogo nikaruka majoka nini basi ilimradi burudani. Ila kwa kipindi kirefu mwenzangu anahubiri divorce mimi nakataa kabisa.

Siku moja tumekaa mezani akanipa simu yake nimrekebishie kitu nikazama mpaka kwenye WhatsApp, loh! Nikakuta kuna njemba anawasiliana naye mambo ya mapenzi duh! Ila sikuonyesha kushtuka nikamwambia tu kwa kucheka "aisee kumbe na wa kuchukua nafasi yangu ushampata?" Nikatumia akili ndefu sana kumuondoa wasi wasi baadae alifunguka hasa akaniambia kila kitu kuhusu jamaa maana nilimuambia naona ni muda wa divorce so akafurahi kwamba atakuwa na huyo njemba.

Nilikuja kugeuza kibao pale alipoanza sasa kufanya kama anataka kuharakisha hiyo divorce kwasababu ni kweli hapa nipo tayari Ila kuna mambo naweka sawa so sikutaka hiyo haraka alafu nilitaka nimsogeze dogo (mtoto) angalau afiikishe umri fulani so nikampiga biti baadae yule jamaa ilibidi amuandikie stop notice coz walikutana kwenye dating websites which nilikuja kugundua alijiunga since last year.

Hapo nikaanza kutafuta namna ya kunusa anachokifanya ndipo nilipoamua kudukua mawasiliano yake ya WhatsApp mpaka leo kila kitu ninacho kiganjani yapata miezi miwili ila sijawahi kuonyesha hata dalili kwamba ninajuwa chochote.

Hatua nyingie huyu bibie akafungua tena email address kama tatu tofauti tena za umafia wake sasa ambacho hakijui ni kwamba najua patern yake ya kufungua simu so huwa anaweza kuacha simu home akaenda zake kidume nikapata nafasi ya kumnusa zaidi Ila dalili sionyeshi.

Katika kunusa huko nikaingia kwenye email moja nikakuta mawasiliano yake na wanaume kama watatu hivi nikapiga screenshots za kumwaga nikatumia WhatsApp yake kujitumia then nikazifuta kwenye chat na kwenye galary so ushahidi ninao mimi japo napanga kuingia tena kwenye email yake nifanye settings kwamba kila email ije kwangu kwa bcc (Black Carbon Copy) ili niya nyake mubashara mawasiliano yake ya email.

Ifahamike kwamba natambua tunaachana ila wazee hawanielewi na siwaambii madhaifu ya mke wangu coz naamini katika kumlindia heshima pamoja na matatizo meeengi mfano Leo ni mwaka wa tatu najipikia mke hanipikii kwasababu amekataa. Huu ushahidi ntatumia kwa faida yangu.

Muda si mrefu ntarejea bongo nikajitafutie mke atakayenifaaa.

Wewe ungefanyanje?
 
Pole sana, mm ningeachana na mambo ya kumfuatilia mtu ambae najua tunaachana soon. I will just let her leave her own life while m looking for my own..

Nimekubaliana na hali japo kitendo hiki familia inakuwa na maslahi makubwa pia so najaribu kutafuta namna ya kujenga hoja
 
Mkuu unaweza chukua fursa hata hapahapa Jf, skuhizi post za wadada kutafuta waume wa kuwaoa zimeongezeka sana.

Ni kweli nitazama chimbo nikutane nao
 
Kwani unadhani wao siyo binadamu mkuu
Najua ninachoongea kamanda! Uliza hata mabinti 100 kati yao 98 wanataka waolewe na mzungu, swali ni why jibu ni kuwa wazungu akiwa na ww ni ww tu hageukiii mwingine! Hiyo kasumba ipo vichwani mwa wengi, sasa hawa wakianza kufumbua hivi watu wanatupunguzia ubishi
 
Najua ninachoongea kamanda! Uliza hata mabinti 100 kati yao 98 wanataka waolewe na mzungu, swali ni why jibu ni kuwa wazungu akiwa na ww ni ww tu hageukiii mwingine! Hiyo kasumba ipo vichwani mwa wengi, sasa hawa wakianza kufumbua hivi watu wanatupunguzia ubishi

Tatizo ni kwamba wazungu wanachagua habari za kuweka hadharani so mara nyingi ni vigumu sana kuwaelewa kiurahisi labda upate bahati ya kukaa nao kwa muda mrefu Ila ujue ni wapuuzi tu pamoja na kiwango chao cha civilization
 
Hapa nimejua point ya mtu fulani kutopenda kuoa wazungu.

Pole wazungu wazuri kwa ku date tu ndoa hapana, maana ni wazuri kuwahonga.

Hauko peke yako kuna mwenzako yupo huko anasema kuanzia chakula, kufua nguo, usafi wa ndani ni yeye, mwanamke ni tv, kuchati na kulala inshort anaendeshwa kama gari bovu,

kinachomuuma zaidi akiendaga ukweni hakuna heshima . Alisema "ukweni wanamuthamini paka wao kuliko mimi, care anazozipata paka ni zaidi yangu"

ushauri fanya maamuzi magumu.
 
Hapa nimejua point ya mtu fulani kutopenda kuoa wazungu.

Pole wazungu wazuri kwa ku date tu ndoa hapana, maana ni wazuri kuwahonga.

Hauko peke yako kuna mwenzako yupo huko anasema kuanzia chakula, kufua nguo, usafi wa ndani ni yeye, mwanamke ni tv, kuchati na kulala inshort anaendeshwa kama gari bovu,

kinachomuuma zaidi akiendaga ukweni hakuna heshima . Alisema "ukweni wanamuthamini paka wao kuliko mimi, care anazozipata paka ni zaidi yangu"

ushauri fanya maamuzi magumu.

Ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom