Sir M.D.Andrew
JF-Expert Member
- Jul 30, 2012
- 201
- 0
Nafanya mazoezi sana,nimejinyima chakula nikaambulia madonda ya tumbo,asali,maji ya uvuguvugu,ndimu vyote nimetumia mwaka sasa unaisha,matunda mboga mboga mpaka zimenichosha-jana nimepandwa na ugonjwa wa ghafla nimepimwa naambiwa presha juu,uzito wangu sasa ni kilo 98 ukilinganisha na urefu wa futi 5.4 tu,umri mdogo miaka 27 tu lakini naonekana baba wakati bado! Nimeamua kitu kimoja tu wana jf,mnisaidie kupata contacts za hebalists au clinic wanapouza dawa za kupunguza unene/kitambi...nahitaji kubaki na uzito wa kawaida! Naombeni mnisaidie