Nimechoka kunyongwa usiku wa manane, tafadhali msaada wa haraka

ndugu huo ni mtihani unapimwa je na ww utaenda katika mambo ya kishirikina kutatua tatizo ama utamuomba mungu. Lakini mbali na yote kiboko yao ni kufukiza bangi tu, au ivute.....
mambo ya ushirikina siyaamini kabisa ndugu yangu'
 
tatizo unamwomba mungu huku unawaza kukabwa!!!mkuu weka imani yako kwa mungu pekee na si mashetani wa kukukaba.napata picha kuwa imani yako kwa mungu ni haba sana.kama ni hivyo lala na kipande cha nyama ya nguruwe ama lala huku umevaa chupi umeigeuza.:target:
 
tatizo unamwomba mungu huku unawaza kukabwa!!!mkuu weka imani yako kwa mungu pekee na si mashetani wa kukukaba.napata picha kuwa imani yako kwa mungu ni haba sana.kama ni hivyo lala na kipande cha nyama ya nguruwe ama lala huku umevaa chupi umeigeuza.:target:
haya mapya
 
Mahali nimefika nimekata tamaa kabisa kwa maana sioni nafuu ya tatizo langu. Ninafanya maombi kwa sana kila siku kabla ya kulala lakini cha kushangaza huwa nanyongwa na watu usiku na kulishwa vitu ambavyo sivijui. Sasa naona bora nitumie njia za kienyeji kuliko kuendelea na maombi. Wana bodi ninavyoandika hapa sina raha kabisa katika ujana wangu kutokana na vitu vinavyotokea usiku nikiwa nimelala. Hivyo kama kuna anayejua njia mbadala ya kukabiliana na wachawi pamoja na wanga anipe japo hata namna ya kufanya ili niwe na amani. Nawasilisha


unatakiwa kutupa majibu ya maswali yafuatayo-
1. je wewe umeokoka?
2. Je wewe unazingatia/unaishi sawasawa na neno la Mungu?
3. Je unasali wapi?
4. Je unatumia marashi ya aina yoyote au mapambo gani?
5. Je unaomba kwa jina la nani?
 
unatakiwa kutupa majibu ya maswali yafuatayo- 1. je wewe umeokoka? 2. Je wewe unazingatia/unaishi sawasawa na neno la Mungu? 3. Je unasali wapi? 4. Je unatumia marashi ya aina yoyote au mapambo gani? 5. Je unaomba kwa jina la nani?[/QU Mimi ni mkatoliki! ninaishi maisha ya kawaida! Ninaomba kwa Mungu baba katika jina la Yesu kristo!
 
unatakiwa kutupa majibu ya maswali yafuatayo- 1. je wewe umeokoka? 2. Je wewe unazingatia/unaishi sawasawa na neno la Mungu? 3. Je unasali wapi? 4. Je unatumia marashi ya aina yoyote au mapambo gani? 5. Je unaomba kwa jina la nani?[/QU Mimi ni mkatoliki! ninaishi maisha ya kawaida! Ninaomba kwa Mungu baba katika jina la Yesu kristo!

Nakushukuru kwa majibu yako mazuri,

Ili upate ushindi kamili dhidi ya mapepo ziko njia mbili, ya kwanza ni kuombewa na watu waliookoka, hii ina ushindi wa muda mfupi tu na ya pili kuombewa na kuokoka hii ina ushindi ulio kamili. zaburi 103.3, ndio hata Yesu alipomtoa mtu pepo mchafu alimwambia angalia umekuwa mzima usitende dhambi tena.

Jinsi ya kuokoka, tunatakiwa kujua kuwa sisi sote wanadamu ni wenye dhambi kwa kuzaliwa na kutenda zaburi 58.5, warumi 5.12, warumi 3.23. Kutokana na kufanya dhambi tumepungukiwa na utukufu wa Mungu. Biblia inasema kila aendaye dhambi ni wa ibilisi. Ikiwa tumekuwa tukisema uongo,kutukana na kutukanana, kusengenya, wivu, uchoyo, waoga,waasherati,wazinzi n.k tujue tumekuwa tunaishi maisha yanayomchukiza Mungu. Biblia inasema kila atendaye dhambi akifa katika dhambi zake atakwenda zake katika moto wa milele(ufunuo 21.8, mathato 25.41). Tunapaswa kujua Yesu kristo alipokuja duniani alileta wokovu, hivyo wokovu sio dini mpya kama watu wengine wanavyojaribu kutupotosha bali ni mpango kamili wa Mungu kwetu kwa ajili ya kutufanya watoto wake na kutupatia uwezo wa kushinda dhambi ili hatimaye tukifa tuweze kwenda mbinguni. mathayo 1.21, Luka 19.10- Yesu alilea wokovu kwa ajili yangu na wewe.

Tunaita kuokoka kwasababu tusipotubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha na kufanyika watoto wa Mungu hatuwezi kuuridhi ufalme wa Mungu bali tukifa katika dhambi tutakwenda zetu katika moto wa Milele.Ndio maana Yesu alimwambia Nikodemo hawezi kuuridhi ufalme wa Mungu hadi azaliwe mara ya pili, yaani aokoke.Yohana 3.

Ili tuokoke tunatakiwa kujua sisi ni wenye dhambi, Yesu alimwaga damu yake pale juu msalabani kwa ajili ya kusafisha dhambi zetu, kwamba kwa nguvu zetu hatuwezi kushinda dhambi bali kwa uwezo wa Mungu pekee, kisha kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha ndipo tutafanyika watoto wa MUNGU. kumbuka tunatakiwa kutubu dhambi zetu zote kwa kumaanisha kuziacha ndipo tutapokea uwezo wa ki-Mungu wa kushinda dhambi. ikimaanisha nn? kama tulikuwa walevi, wazinzi, waasherati,tuna girlfriend/boyfriend,watukanaji n.k. tudhamirie kuacha kila uovu tuliokuwa tunaufanya zamani ndipo tutapewa uwezo wa kushinda dhambi.

Ukishaokoka unafanyika kuwa mtoto wa Mungu, kama mbinguni kusivyo na pepo hata moja na kwako hakuna hata pepo mmoja atakayekuwa na haki ya kukaa na kukusumbua. tambua kuwa mtu anapoishi maisha ya dhambi anampa haki shetani ya kumuonea kwa njia mbalimbali iwe magonjwa au mapepo n.k. ukishaokoka una haki ya uzima na kuwa mbali na mapepo yote zaburi 103.3.Je uko tayari kuokoka sasa?, najua uko tayari, ebu sema maneno haya, Mungu Baba mimi ni mwenye dhambi, kwa kuzaliwa na kutenda, ninaomba unisamehe dhambi zangu zote, nishafishe dhambi zangu zote kwa damu ya Yesu Kriso aliyoimwaga pale juu msalabani,ulifute jina langu katika vitabu vya hukumu na uliandike katika kitabu cha uzima, unifanye kuwa mtoto wako kaika jina la Yesu Kristo, Amen.

Hongera kwa kuokoka, sasa una haki ya kuitikia salaamu ya Bwana Asifiwe kwani umefanyika kuwa mtoto wake. Kumbuka uamuzi uliouchukua ni wa busara sana wala hautaujutia katika maisha yako yote. Kumbuka pia kuwa uamuzi wako umemfurahisha sana Mungu na mbinguni malaika wanafanya shangwe na sherehe kuu kwa kuamuzi wako. ni furaha ilioje kuona hata malaika wanasherehekea uamuzi wako.

Ili uweze kuukulia wokovu unatakiwa kuhudhuria katika ibada za makanisa ya watu waliookoka kwasababu wana imani sawa na wewe hivyo ni rahisi wao kukufundisha mambo mengi yanayohusu mapenzi ya Mungu na kukutia moyo kusonga mbele katika imani ya wokovu uliyoipokea leo. Kwani ndivyo biblia inavyotuagiza

Pia kumbuka sasa kumkemea shetani na mapepo yanayokusumbua kwa Jina la Yesu Kristo nayo yataondoka kwako kwani umepewa Amri na mamlaka dhidi ya shetani, mapepo yake na nguvu zote za yule mwovu ibilisi.kwa mfano unaweza kukemea kwa kusema: Kwa jina la Yesu Kristo enyi pepo hamna uwezo wa kunitesa kwa ndoto an chochote kile kibaya. kila kazi zenu na mipango yenu yote naihaibu kwa jina la Yesu Kristo, na kila ndoto na maono yenu ya kutisha ninayafuta na kuyakomesha kwa jina la Yesu Kristo,siyataki wala siyahitaji tena, nafunga milango na ndoto mbaya na kufungulia ndoto za mbinguni katika jina la Yesu, n.k. Kisha nyunyiza damu ya Yesu Kristo katika chumba chako na uinywe kwa imani baada ya hapo lala, utashangaa hutaona vitu hivyo. hakikisha kila unapoomba malizia na neno Amen kwani linamaanisha imekuwa, ndivyo ilivyo, neno la Mungu ni kweli na amini na limehakikishwa na lazima litatimia

kumbuka ukifika kanisani kwa watu waliookoka watakupa maarifa mengi zaidi ya jinsi ya kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kuwa mtakatifu kama Mungu mathayo 5.48

Mungu wa milima na tambarare akubariki sana wewe na familia yako

Ninakutakia jumatatu njema na kazi njema yenye baraka tele kwako
 
Ndugu utapata mashauri mengi kutoka kwa wanadamu. Mimi hiyo hali ilinianza nikiwa form three upepo wa kishundo ulivuma toka nje nikia hosteli usiku wa manane,usingizi ambo sikuwahi kuujua ulinivaa mara sikuweza kuinua mguu wala mkono,nkasema ngoja nikemee ulimi ulibanwa sikuelewa nilichokitamka ndani ya dakika chache niliachiliwa nakurukia bible nikitafakari ni kitu gani na kwanini. Hapo ndo ilikuwa mwanzo wa mateso kama yako yaliyodumu kwa miaka saba mfululizo. Nilisali sana niwezavyo badaye nkawa nakata tamaa kama wewe. Siku moja nlilipata ujasili wa ajabu nikasema kwa jina la Yesu wa nazareth nakubali mateso na nitapigana bila kakata tamaa nikiamini kataka imani yangu ya kilristo bila kwenda kwa mganga kubadili dini wala kutafuta mlokole wa kuniombea. Mapambano yalianza nikiwa na nguvu mpya,sasa nikawa nasikia chumbani kwangu ---- watu zaidi ya mmoja nkianza tu kusikia ule udingizi nakemea kwa imani nakujiami mara nasikia kama upepo unaruka kwa nguvu na ile ngu ya ajabu inaniachia nalala kwa amani,mashambulizi yalienda hibyo. Sikumoja ilinitokea ikanibana sana maneno yakawa hayatoki kwa dakika nyingi kidogo,nilivopata mwanya wa kutamka yalinitoka maneno saba tu na kwa haraka na kwa hasira. Nilisema"NDIO YESU NI MWANA WA MUNGU" ukitoka upepo wa hatari na me nilihema sana najasho likitoka. Kuanzia siku hiyo mpaka sasa nalala kwa amani hata nikisema kwa imani asante Mungu kwa siku ya leo nkakabidhi usikuu huu basi. Usingizi wangu mwanana. Kwanza kubali kwamba umeumbwa kama jeshi la Mungu kua utapigana kiroho ili kumuinua Mungu wa mbingu,amini Yesu yupo na anaponya,amini hakuna awezaye yeyote kutoa uhai wa roho yako isipokuwa Mungu pekee. Amini kwa msaada wa Yesu christo wa nazareti hakuna nguvu yoyote ya giza itakayo kuba aisha. Kila usikiapo hiyo hali taja jina la Yesu kwa imani bila kuhisi kuwa unateswa. Muda mchache utayashinda. Mimi ni mkatoloki pia.
 
huna iman,sasa yakupasa amin kuwa hutokabwa tena na yakupasa b4 hujalala piga sala na kulala na endapo itatokea taja jina la YESU KRISTO na kuomba damu yake ikufunike.nami ilishawah nitokea na nilitaja jina la yesu krsto na kukemea na baada ya muda mfup kuona kiza kikitokomea.eebwana toka cku ile cjakabwa tena,halafu ucpend kulala sehem yenye kiza sana jaribu kuwasha hata mwanga wa simu yenye torch ifunike kdogo japo papatkane kamwanga flan kisha sali sala zako halafu uone.fanya hivyo ndugu uje kutupa feed
 
ndugu kingne unapolala jaribu kuacha ndoo yenye maji wazi hapo unapolala na pia sali sala yako.ndo hayo mkuu,fanya hivyo uone miujisa
 
tiba yako unayo mwenyewe, acha kulala chali halafu funga kula usiku, na usifanye maombi kabla ya kulala, wewe lala weka alam ikifika saa saba na nusu au nane amka. anza kwa kusoma zaburi, sura zisizopungua kumi na uendeleee bila kuchanganya au kuruka ruka. soma kitabu kimoja kimoja kwenye biblia hadi kiishe kwa utaratibu huo wa kila siku ukiamka kufanya maombi ,na ukiamka baada ya kusoma neno kwa kutafakari bika kukimbia kimbia huku ukizingushia kalamu unapoguswa sali kwa kuongea na Mungu kuitia jina la Yesu umuombe akupe nguvu, fanya toba ya utakaso kwa damu ya Yesu kama dakika kumi ili upewe nguvu za kuvunja hizo roho, usiwamwambie Mungu/Yesu naomba unisaidie ukaishia hapo. Hapana wewe omba upewe nguvu halafu attack mwenyewe utashangaa. hatua hiyo ya pili ni kuomba kwa kuvunja na kukemea uendelee kwa angalau muda wa saa moja muda wa siku tatu halafu wakienndelea ni PM. Unaweza kukemea kwa kunong'ona si lazima umuamshe jirani ila hakikisha umesimama na unatembea tembea humo ndani. nimejifunza faida za kuomba huku unatembea by Mwakasege. Omba yAani kama unagombezana na mtu huku ukiamrisha in personal sio kusema Yesu vunja. taja taja chochote tu. utashangaa Mungu wetu ni wa imani hata walio vunja kuta za Yeriko walizunguka tu. ila katika kutaja kwako lazima uchomeke common words kama DAMU YA YESU, NAVUNJA MAMLAKA YA GIZA, ROHO ZA UCHAWI, MAMLAKA YA KUZIMU SHINDWA, KWA JINA LA YESU, ROHO MTAKATIVU, JEHOVA huku ukichanganya na scenario ya tatizo lako. utashangaa Mungu atakachofanya tena ukikomaa kiimani huhitaji hata mtu akuombee na hapo nguvu za Mungu zinafanya kazi sana. Utashangaa. Ila hakikisha unalala kifudi fudi. kufunga sio siku zote funga moja moja kula mlo wa usiku kabla ya kulala ili ulimwengu wa roho uwe wazi. maji waweza kunywa. omba kati ya saa nane na saa saa tisa, yaani zamu ya tatu usivuke hapo lala ili ile mida ya zamu ya nne yaani saa kumi hadi saa kumi na mbili Mungu akuonyeshe what is in the basket in the time ahead. ulimwengu wa roho una raha sana ila kwanza mpaka uwe mjinga fulani. mwanzoni wachawi watapersist sana lakini ni katika kujaribu kutumia ujanja wao wote ila haufikagi mbali within a week watachemsha. kumbuka Farao kupitia waganga na wachawi alidemostrate miujiza yote ambayo Mngu aliyofanya mpaka walipoingia muujiza wa tano kama sio wa nne ndo akachemsha. pia wakati mwingine Munug anaweza kuamua kwanza maombi yako yawe ineffective ili kuona imani yako. ukishawaza mambo ya waganga Mungu hawekwagwi for test. ni katika perseverance and endurance ndo tunapokea vitu vya koroho. Ina maana unahisi wachawi wana mzidi Mungu? kinachokusumbua ni principles ndo hujazijua. we fuata huo muongozo wewe mwenyewe utasema

Pia pale unapokua umewahiwa ukajikuta hiyo hali imekuvaa ng'ang'ana mpaka utamke YESU. Ina evaporate immediately. mimi huwa wachawi wakija popote pale nilipo na mimi huwa naamka hukohuko usingizini tunakutana huku nikiwa nimelala kabisa.
 
Jaribu kuangalia aina ya maisha unayoishi nikiwa na maana kuwa ni je ni mtu wa mawazo sana au una mambo ambayo yanakufanya uwaze sana? Je utaratibu wako wa kula kabla ya kulala ukoje? Kama ni mtu wa mawazo sana au kuna mambo yanayokusumbua na bado hujayapatia ufumbuzi jaribu kukabiliana nayo kwa njia nyingine tofauti na kuwaza sana. Jitahidi kula mlo mwepesi wakati wa usiku na kaa mda kiasi kabla ya kwenda kulala.Niliwahi kufikwa na hali kama ya kwako na nilishauriwa kufanya hayo niliyoandika hapo juu TATIZO lilipungua kidogokidogo hadi leo hii ni historia sijawahi kuhisi tena hali kama ile. Pole sana mkuu
 
Mahali nimefika nimekata tamaa kabisa kwa maana sioni nafuu ya tatizo langu. Ninafanya maombi kwa sana kila siku kabla ya kulala lakini cha kushangaza huwa nanyongwa na watu usiku na kulishwa vitu ambavyo sivijui. Sasa naona bora nitumie njia za kienyeji kuliko kuendelea na maombi. Wana bodi ninavyoandika hapa sina raha kabisa katika ujana wangu kutokana na vitu vinavyotokea usiku nikiwa nimelala. Hivyo kama kuna anayejua njia mbadala ya kukabiliana na wachawi pamoja na wanga anipe japo hata namna ya kufanya ili niwe na amani. Nawasilisha

Achana kabisa na mambo ya uganga yatakumalizia pesa kama iman yako ipo kwa mungu bas iwe kwel na kama kwa waganga pia nako uwe kwel, acha kuwa vuguvugu ndio maana hata hayo majini hayakuelew, wakuweke kundi gan????pia shetan anatumia neno la bibilia kudanganya watu hivo kuwa makini.
 
Achana kabisa na mambo ya uganga yatakumalizia pesa kama iman yako ipo kwa mungu bas iwe kwel na kama kwa waganga pia nako uwe kwel, acha kuwa vuguvugu ndio maana hata hayo majini hayakuelew, wakuweke kundi gan????pia shetan anatumia neno la bibilia kudanganya watu hivo kuwa makini.[ Sawa mkuu!
 
Nakushauri njoo uonane nami nikupe dawa ya kuondokana na tatizo hilo siku moja tu majinamizi hayatukufuata na kukukosesha usingizi wako ambao Mungu amekupa ulale unono wao wanakuwangia hovyo wewe niPM tu nitakupa dhana ya kuondokana nayo ilo tatizo yuko mmoja anayeweza kuondosha matatizo hayo ukimwamini yeye utakuwa huru tena huru kwelikweli niPM TU nitakukwambia namna ya kufanya best
Mahali nimefika nimekata tamaa kabisa kwa maana sioni nafuu ya tatizo langu. Ninafanya maombi kwa sana kila siku kabla ya kulala lakini cha kushangaza huwa nanyongwa na watu usiku na kulishwa vitu ambavyo sivijui. Sasa naona bora nitumie njia za kienyeji kuliko kuendelea na maombi. Wana bodi ninavyoandika hapa sina raha kabisa katika ujana wangu kutokana na vitu vinavyotokea usiku nikiwa nimelala. Hivyo kama kuna anayejua njia mbadala ya kukabiliana na wachawi pamoja na wanga anipe japo hata namna ya kufanya ili niwe na amani. Nawasilisha
 
tatizo unamwomba mungu huku unawaza kukabwa!!!mkuu weka imani yako kwa mungu pekee na si mashetani wa kukukaba.napata picha kuwa imani yako kwa mungu ni haba sana.kama ni hivyo lala na kipande cha nyama ya nguruwe ama lala huku umevaa chupi umeigeuza.:target:
Tunaacha kumuangalia Mungu tunaangalia matatizo tulio nayo;
katika Hes21:4-9 watu wanang'atwa na nyoka kwa kosa lao wenyewe. Hata hivyo Bwana anawataka waache kuangalia majeraha yao na badala yake watazame juu ili wapate kuishi. Hii ni picha ya Ebr12:2 ambapo yesu tunatakiwa kuacha kuangalia ugonjwa na badala tumwangalie yesu. Hatuwez kuangalia sehemu 2 wakat m1 (mganga na Mungu) kama kinyonga. Yatupasa kuchagua; ama tuangalie magonjwa yetu au tuangalie ahadi ya Mungu.
Pia Daudi anatutahadharisha tusijesahau kuwa moja ya fadhila za Bwana ni kutuponya magojwa yetu yote (zab 103:1-5)
unamwomba Mungu huku unawaza kwa mganga sasa huko si ndo unaenda kuyaongezea,Tatzo lilipo hapa ni imani ndogo hata punje ya mchicha kubwa!!
 
Back
Top Bottom