Nimechoka kunyongwa usiku wa manane, tafadhali msaada wa haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimechoka kunyongwa usiku wa manane, tafadhali msaada wa haraka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Apolinary, Mar 3, 2012.

 1. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mahali nimefika nimekata tamaa kabisa kwa maana sioni nafuu ya tatizo langu. Ninafanya maombi kwa sana kila siku kabla ya kulala lakini cha kushangaza huwa nanyongwa na watu usiku na kulishwa vitu ambavyo sivijui.

  Sasa naona bora nitumie njia za kienyeji kuliko kuendelea na maombi wana bodi ninavyoandika hapa sina raha kabisa katika ujana wangu kutokana na vitu vinavyotokea usiku nikiwa nimelala.

  Hivyo kama kuna anayejua njia mbadala ya kukabiliana na wachawi pamoja na wanga anipe japo hata namna ya kufanya ili niwe na amani.

  Nawasilisha
  Inaendelea
  Ikiwa kama miezi kadhaa numetulia bila kukabwa sasa hivi karibuni mwezi wa tisa nimeanza kukabwa tena bila kukoma hata usiku mmoja.

  Mchungaji kiongozi Gwajima alikuja arusha katika viwanja vya relli nilienda pia lakini cha kushangaza nilirudi home hali ikawa ni ile ile.

  Ndugu wadau siamini katika giza lakini hali niliyofikia sina budi.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  angalia jinsi unavyolala
   
 3. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 4. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Pole sana.. Ushauri wangu..weka maisha yako kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu kupitia imani au dhehebu lako. Mwangukie Mungu kwa Moyo wako wote na hata ukisali hakikisha unasali toka moyoni na siyo kuimba sala kama shairi. Jenga imani hadi uone unamwomba Mwenyezi Mungu kuwa kama yeye anataka wewe uendelee unyongwe kila siku na iwe hivyo..lakini si kama wewe unavyotaka.

  Kama unasali na unayo imani kwa Mungu basi haukuwa na haja ya kuhama ile nyumba ya kwanza. Pia kumbuka kama bado unaamini nyumba ya sasa bado ina mikosi basi hiyo ni dalili ya kuwa imani yako bado ni ndogo...

  Endelea kusali kwa dhati na Amini Mungu atakusaidia..otherwise, utaendelea kupigika na kusaga meno..
   
 5. M

  MYISANZU Senior Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani unanyongwa halafu tena bado u mzima! Wewe ni noma.
   
 6. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 7. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 8. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Pole sana ndungu, kitu cha kwanza jikabidhi maisha yako na kazi zako mbele ya MUNGU wako kwa muda wote kulingana na imani yako. Pili, jitahidi kupunguza vyakula vizito wakati wa usiku au kula mapema masaa 3-4 kabla ya kulala. Tatu, jaribu kubadili staili ya ya ulalaji wako kwa kufanya majaribio tofauti.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Acha kulala umefunga madirisha na milango hadi hewa inaisha.

  Hata kama unafungua kidogo, basi unajifunika gubigubi na mwisho unaishiwa hewa.

  Pia angalia mto (Pillow) unayotumia maana inaweza kuwa ndogo na ukilala, unajibana kifua.

  Ushauri wangu tu huu. Nenda kwa Dr. na usianze sana kuweka Mungu na Uchawi katika hili mara moja.

  Mungu nisaidie na wewe unakimbia. Ila usiende kwa Sangoma bana.
   
 10. wizaga

  wizaga Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MSAADA MKUBWA NI KUMUOMBA MUNGU KAMA WALIVYOSHAURI WENGINE,UKIENDA KWA DAKTARI HALI HIYO HAITIBIWI ZAIDI YA KUKUPA DAWA ZA WAGONJWA WA AKILI LAKINI PIA HUYU ALIYESEMA Mungu nisaidie na wewe unakimbia NILIPOWEKA ALAMA NYEKUNDU,MUNGU HAWEZI KUKUSAIDIA NA WW UNAKIMBIA NI MANENO POTOFU ,TENA MANENO YA UHUNI.KWANI HUWEZI UKAWANASEHEMU YA KUJISAIDIA NA SEHEMU NYINGINE MUNGU ANAKUSAIDIA.MUNGU HUFANYA JAMBO PEKEE HAHITAJI MSAADA.TOTAL HELP
   
 11. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  usikute unabugia sana chakula usiku tumbo linakuwa kama pakacha.....unabakia kulala chali....na pia jaribu kufanya mazoezi mara kwa mara.....
   
 12. Angel Nylon

  Angel Nylon JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 4,471
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  pole sn, fanya uombewe na we mwenyewe sali na kusoma dua sn.
  Lkn c vibaya pia if u see a doc.
  Au angalia hilo tatizo limeanza lini na linarelate na tukio gani lililowahi kukupata.
  Possible ni msongo wa mawazo, muone Dr
   
 13. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  dah!pole mkuu! Cha muhimu ni kumtegeme Mungu pekee!!
   
 14. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,770
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  Lala na bibilia pembeni.
   
 15. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Tafuta mfupa wa kitimoto uuweke chini ya mto unaolalia...mauzauza yote yatakwisha!
   
 16. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Apolinary inaelekea una tatizo la kitibabu, mwone daktari ili akushauri mambo ya metabolism.
  Kwa kawaida mlo mzito unaleta usingizi na mwili kukosa nguvu maana damu yote inaenda sehemu ya matumbo ili kusaidia kuyeyusha na kuchukua virutubisho vinavyo tolewa kwenye chakula.
  Inaelekea hii process ina matatizo ambayo yaneweza kurekebishwa ukimwona daktari.
  Zaidi ya hapo rndelea kusali sana na Mungu atasikia kilio chako ili mwili ufanye kazi kama kawaida.
   
 17. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 18. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,983
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Ndugu pole sana kwa yanayokukumba, wapo wengi ambao wameteseka kwa namna hiyo ila walipochukua hatua ya kubadili life style ya maisha yao wamewekwa huru kabisa.
  Piga moyo konde chukua hatua zifuatazo na kwa kumaanisha ndani ya moyo wako utawekwa huru kabisa.

  1.Amini katika Jina la YESU, Yohana 1:12, tubu dhambi zako zote popote pale ulipomkosea Mungu yeye ni mwaminifu atakusamehe kabisa, Isaya 1:18, Isaya 43:25, Zab 103:3,11,12, Mkaribishe ROHO MTAKATIFU awe ndani yako na kuyaongoza maisha yako, Wagalatia 4: 6,

  2. Kwa kumwamini Bwana YESU, kutubu dhambi zako zote, na kumwalika Roho Mtakatifu kuwa ndani yako, unayo mamlaka na nguvu za Mungu kushinda ulimwengu wote wa giza. Muda wowote utakapo jisikia hiyo hali tumia mamlaka ya JINA LA YESU kukemea hizo nguvu za giza wala hazitakuwa na uwezo juu yako. LUKA 10:19, MARKO 16:17-18,

  3. Jiwekee utaratibu wa kusoma na kutafakari neno la MUNGU ndani ya Moyo wako popote pale utakapokuwepo. Kumbuka ibilisi atakuletea hofu ya kukunyonga kama kawaida yake, chukua hatua ya kukemea hiyo roho ya hofu, na mtafakari Mungu na uweza wake katika Jina la YESU badala ya kuwaza hizo hofu za ibilisi. Wakolosai 3: 1-2.

  4. Ukifanya maombi usifanye maombi legelege, fanya maombi ya vita ya kujikomboa kutoka katika utawala wa shetani, tumia silaha zote za UFALME WA MUNGU kumpinga na kumpiga shetani ili asikufuatilie. Uhuru haupatikani kilegelege ni kwa vita ndugu. 2-Wakorintho10: 4-5

  5. Acha dhambi yoyote ile inayokuzinga ambayo ibilisi anaweza kuitumia kama njia ya kuendelea kukushambulia. Kumbuka MUNGU ni Mtakatifu na anawatetea wale wote wanaoishi katika njia zake. Wagalatia 5:20-21.

  6. Hakikisha unahudhuria vipindi vya maombi na kujifunza neno la Mungu katika kanisa linalohubiri Injili ya kweli na kuamini katika karama zote za ROHO MTAKATIFU na si ubabaishaji.

  Ndugu, Bwana Yesu akusaidie na kukuweka huru kabisa.

   
 19. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
   
 20. ossy

  ossy JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 877
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Well said mkuu!
   
Loading...