jasinta hny
Member
- Jan 29, 2016
- 18
- 12
Hi guys,
Mimi na mtu wangu tulikuja states kutafuta maisha miaka 9 iliyopita, tumekua tukiishi pamoja bila ndoa kwa kipindi chote hicho, tuna mtoto mmoja wa miaka 5, tangu tumekuja hapa states shughuli zetu ni kubeba box, I mean blue colar jobs, nadhani nimeeleweka nikisema hivyo.
Kwa kweli pesa ya kula na huduma zingine tunapata ingawa ni katika mazingira magumu, tangu tumefika hapa hadi sasa hakuna kitu cha maana tunachoweza kuonesha kwamba tumepata, zaidi ya kula, kuvaa na kulipia pango, pesa yote inaishia kwenye mahitaji, basic needs, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya mtoto, tumekua under pressure na wazazi kwamba kama vipi turudi, wazazi wetu wanafaamiana, na wanajua tunaishi pamoja.
Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa nimekua nikimsihi mwenzangu kuwa turudi tu nyumbani Tanzania tukafutie maisha huko, tukichanganya pamoja akiba zetu ingiwa si nyingi sana tunaweza kurudi home tukaanzisha biashara hata ya kawaida tu, lakini hataki kusikia, anataka tuendelee kupiga mark time huku huku, tumekua ugomvi mkubwa juu ya suala hili, wakati flani alidunduliza kiasi kingi cha pesa na kumtumia mdogo wake ili amjengee nyumba, yule dogo akakimbia na hela zote hajulikani yuko wapi hadi sasa, hivyo amekata tamaa ya kukusanya tena hela hasa baada ya mkataba wa hiyo kazi iliyokua ikimlipa vizuri kuisha, ingawa ilikua ni ya kubeba box.
Kilichonifanya niombe ushauri kwenu ni kwamba, kuna jamaa kutoka Tanzania alikuja huku mwaka jana june kikazi, anafanya kwenye shirika la kimataifa hivyo anakuja huku sana, amekua akiniomba anioe tukaishi wote TZ, nilimueleza kwamba nina mtu naishi nae nina mtoto pia, akadai si shida, yupo tayari aende kwetu kujitambulisha kama siamini, nikaomba anipe muda, ilikua june last year, akawa amerudi Dar, tukawa tunaongea kwa simu bila mtu wangu kujua mawasiliano hayo.
Nikamuunganisha na mdogo wangu wa kike nikampa namba nikitegemea ni lazima watatongozana tu wawe wapenzi then aache kunisumbua, cha ajabu akamuomba mdogo wangu ampeleke home ana shida na wazazi, akapelekwa, akawaeleza nia yake, ni kama vile mama akawa amekubaliana nae, tangu hapo familia nzima wananisumbua nirudi nifunge ndoa na mshikaji, wanasema achana na huyu jamaa hana muelekeo, jamaa wa Dar yupo tayari kunitumia nauli anytime, na amekua akinitumia pesa sana.
Ndugu zangu nipo njia panda, baba wa mtoto wangu tumetoka nae mbali ndie alienileta states, yeye alitangulia kuja kisha akanitumia pesa za kushughulikia visa na baadae nauli, hata hivyo malengo yetu yaliyotuleta huku hayajatimia, hata shule tu tumeshindwa kusoma, malengo ya awali kabisa ilikua ni kila mmoja apate degree, lakin imeshindikana, pesa zote zinaishia kwenye matumizi, wakati mwingine akawa hataki tu tusome bila sababu
Nimeona bora nimkimbie nirudi home TZ nisome, niendelee na maisha yangu, maana huku pia tunagombana sana, na hakuna wazee hata wa kupeleka malalamiko kila mtu na mambo yake, hivyo mtu unaweza kubaki ndani unalia kutwa nzima.
Naombeni ushauri wenu