Nimeanza ujenzi ili nisipange tena

mozambiqueone

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
232
119
Nimeanza ujenzi ili nisipange tena. Ila gharama inataka kuharibu ka- lengo kangu hako. Nyumba yenyewe ni mita 13 x mita 15.
Mtaalamu asaidie idadi ya bati zinazohitajika. Lakini pia ....

Kwa wanaofahamu, bati hizi za kawaida, gauge 28 ziko recomended sana hadi katika majengo ya serikali. Sijajua endapo hizi za gauge 30 ni tatizo sana ukizitumia kwa maana kwamba zinachakaa haraka, au kero nyingine kubwa ambayo sijaifahamu. Ni mkoani simiyu huku....

Nataka kusema gharama imekuwa kubwa kwangu kiasi kwamba ninataka kuchagua kutumia bati za gauge 30, nitakuwa nimeharibu kwa kiasi gani.
Asanteni.
 
Kama utakuja kukaguliwa ndo ujengee bati za gauge28, ila Kama ni kwako mbona gauge30 ndo mpango wa mjini...kwa dimension zako nunua bati 110. HAyo mambo ya gauge 28 ni mapendekezo ya serikali wanapokuwa wanajenga mamiradi yao.
 
Hongera sana;
Inategemeana na muezeko wako mkuu, kama ni kuezeka ili mradi utatumia badi chache lakini kwa muezeko wa kisasa bati lazima ziongezeke!
 
Umeamua kujenga ukitegemea vyanzo vingapi vya pesa ambavyo ni endelevu? Usikope!
 
Back
Top Bottom